Pages

BRAND NEW MUSIC

metty magese

metty magese

Listen & Download

http://mdundo.com/a/32626

Monday, March 25, 2013

WEMA SEPETU AMNUSURU KAJALA KWENDA JELA MIAKA 5


HUKUMU ya kesi iliyokuwa inamkabili staa wa filamu za Kibongo, Kajala Masanja na mumewe imetolewa leo na Hakimu Sundi Fimbo katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, jijini Dar. 

Katika hukumu hiyo Kajala amehukumiwa kwenda jela miaka mitano au kulipa faini ya shilingi milioni 13 na mumewe kwenda jela miaka saba au kulipa faini ya shilingi milioni 200.

Kajala alikuwa anakabiliwa na kesi ya kuuza nyumba iliyowekwa kizuizini na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) baada ya mumewe, Faraji Agustino kukumbwa na msala wa kutakatisha fedha haramu.


 Mrembo wema sepetu ndo ameweka dau hilo mezani kumnusuru kajala asiendelee kusota kwa kesi ambayo ilikuwa imefikia tamati ya hukumu hiyo.

DAXX AGAIN...NOW ON 410 MAGAZINE OF S.A

Photo: Daxx again on Exclusive interview with the famous 410-magazine of S.A..New issue of April 2013Daxx again on Exclusive interview with the famous 410-magazine of S.A..New issue of April 2013.

Thursday, March 21, 2013

MWANAMKE ACHINJWA KAMA MBUZI HUKO KAHAMA

HUU ni ukatili kwa 100%! Martha Charles (22), mkazi wa Nyahanga wilayani hapa ambaye ni mtumishi wa Halmashauri ya Mji wa Kahama ameuawa kinyama kwa kuchinjwa shingoni na mume wake

Marehemu Martha Charles baada ya kuchinjwa shingoni na mume wake.
Kaimu Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Shinyanga, Afande Onesmo Lyanga alisema tukio hilo lilitokea katikati ya wiki iliyopita ambapo pia alimtaja mume anayedaiwa kutekeleza unyama huo kuwa ni Asack Nzolela (29), mfanyabiashara wa bucha la nyama ya ng’ombe.

Afande Lyanga alisema mtuhumiwa alimchinja  mkewe wakiwa wamelala chumbani kwenye nyumba ya wazazi wa mwanaume huyo na baada ya kufanya ukatili huo alikimbia. 


Habari za uhakika zilizopatikana kutoka katika familia ya marehemu zilisema chanzo cha mauaji hayo ni ugomvi wa kifamilia ambapo mtuhumiwa alianza kwa kumlaumu mama yake mzazi kwa kitendo cha kumtafutia kazi mkewe katika Halmashauri ya Mji wa Kahama wakati yeye alikuwa hataki mkewe afanye kazi.

Habari zilizopatikana eneo la tukio kutoka kwa mmoja wa ndugu anayeishi na familia hiyo, Paul Edward alisema mbali na kuchinjwa shingoni pia marehemu alikatwakatwa sehemu mbalimbali za mwili wake.

Marehemu Martha Charles (kulia) enzi za uhai wake akiwa na rafiki yake.

Edward alisema usiku wa tukio akiwa amelala katika moja ya chumba ndani ya nyumba hiyo, alisikia kelele za ugomvi kutoka kwenye chumba cha wanandoa hao hali iliyomfanya apige kelele zilizowafikia majirani ambao walifika kutoa msaada.

Akasema majirani hao sanjari na yeye walimkuta mtuhumiwa ameshamchinja mkewe kwa kisu na kutoweka kusikojulikana. 

Nao majirani waliokwenda kutoa msaada ambao hawakupenda majina yao yatajwe gazetini, walisema walikuta mwili wa Martha ukiwa kitandani huku amekatwa na kitu chenye ncha kali katika eneo lote la shingo, ndipo walipomchukua na kumkimbiza hospitali lakini tayari alikuwa ameshakata roho.

Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa, Noel Mkisi alisema baada ya muuaji huyo kutoroka usiku huohuo jitihada za kumsaka zilianza.

 Isack Nzwalile aliyemchinja mkewe, Martha Charles.

Tukio la kuchinjwa kinyama kwa mwanamke huyo limetokea siku chache baada ya hivi karibuni, mchuna ng’ombe Musa Petro (27) naye kumuua kwa kumchinja kwa kisu mpenzi wake, Jessica Elialinga (19). 

Naye Mwenyekiti wa Wafanyabiashara wa Maduka ya Nyama Kahama, Faraji Mohamed akiongea na mwandishi wetu alisema Petro ni mfanyakazi wa Nzolela katika duka lake la nyama (bucha) ambapo alishangaa kusikia Nzolela amemchinja mke wake kama alivyofanya mfanyakazi wake, Petro.

Wakati tunakwenda mitamboni habari zilizopatikana kutoka Kituo cha Polisi cha Wilaya ya Kahama na kudhibitishwa na OCD George Simba zilisema mtuhumiwa huyo amekamatwa.
Mpekuzi blog.

MAMA LINEX APINGA MWANAE KUOA MZUNGU

Sunday Mangu ‘Linex’ akiwa na mchumba wake Suvi Rikka.
SIKU chache baada ya Mbongo Fleva, Sunday Mangu ‘Linex’ kumvisha pete ya uchumba demu wake mtasha, Suvi Rikka, mama wa staa huyo, Imelda Barnabas ameibuka na kumchana mwanaye kuwa haitambui pete wala mchumba huyo kwa kuwa kitendo hicho hakina baraka zake wala za familia.


Linex alipoulizwa juu ya sakata hilo, alifunguka:
“Yah! Bi mkubwa amenijia juu ile mbaya, ila najitahidi kumuomba msamaha, hope atanielewa.”

Wednesday, March 20, 2013

KILI EXTREME DEEJAYS ILIVYOTOA TOP VIDEO NDANI YA MAISHA CLUB DAR


Visura wakiwa na top video zao kutoka kwa kili xtreme deejayz MAISHA CLUB majuzi

Salma  akiwa na dvd yake ya top video

Esma Platinum na Ladynaa wakiwa wamepozi na Top Video zao.

Matukio uk

MSANII BONGO MOVIE AHUSISHWA NA KESI YA UJAMBAZI JIJINI DAR

                                                                 
 STAA wa filamu za Kibongo, Lungi Mwaulanga hivi karibuni aliswekwa lupango katika Kituo cha Polisi Oysterbay jijini Dar baada ya kuzushiwa kesi ya ujambazi na mpangaji mwenzake .

Akizungumza na waandishi wetu, Lungi aliyesota mahabusu kwa siku mbili alisema hivi karibuni usiku wa manane aligongewa mlango nyumbani kwake na watu asiowafahamu, alipotoka alikutana na askari waliomchukua na kumwambia kwamba anatuhumiwa kwa ujambazi.

Hata hivyo, Lungi alisema kuwa baada ya kuwauliza askari ni wapi dada huyo amevunjiwa  au kitu gani alichoibiwa, askari walimbadilishia kesi na kumwambia kuwa amemtukana. Mpaka sasa, Lungi yuko nje kwa dhamana.

JE WAMJUA KING MAJUTO?

Amri Athumani, anayejulikana pia kama King Majuto, amekuwa mwigizaji wa vichekesho kwa miaka 55, Mtanzania huyu mwenye umri wa miaka 65 anaweza kuonekana nchini kwake kote na anatambuliwa kimataifa.
  • Amri Athumani, anayejulikana zaidi kama King Majuto, amekuwa muigizaji wa vichekesho Tanzania kwa miaka 55. [Na Francis Peter Machibya] Amri Athumani, anayejulikana zaidi kama King Majuto, amekuwa muigizaji wa vichekesho Tanzania kwa miaka 55. [Na Francis Peter Machibya]
Zaidi kuhusu kazi yake, King Majuto amelenga katika kutetea amani na kukuza umoja wa taifa. Katika shughuli za umma, vipindi vya redio na sinema ambazo anaonekana, anakuza jamii iliyo salama, utawala bora, heshima ya binadamu na maisha mazuri kwa wote.
King Majuto alizungumza na Sabahi kuhusu mapenzi yake kwa kufanya sanaa na jinsi ya kuimarisha jamii.
Sabahi: Lini ulianza kuigiza?
King Majuto: Nilianza kuigiza mwaka 1958 nikiwa na umri wa miaka 10. Niliuwa katika Shule ya Msingi ya Msembweni, na nilikuwa na uzoefu ambao ulinihamasisha kuwa mwana sanaa.
Mlevi mmoja alikuwa anapita karibu na shule yetu huku akipiga ngoma kwa nguvu huko nje. Mtoto mmoja akajiunga kucheza ngoma kwa sababu yule mtu alikuwa anapiga mdundo mzuri. Mwalimu wetu alikasirika na kumtuma mwanafunzi mwingine kumfukuza yule mtu. Badala ya kumkimbiza, mwanafunzi yule naye akajiunga na ngoma.
Mimi nilikuwa darasa la pili. Mwalimu wetu akatoka nje ya darasa kwa kishindo na kwenda kumfukuza yule mlevi. Sote tulikuwa kimya huku tunamwangalia mwalimu wetu kwa dirishani. Wakati mwalimu alipokuwa anamkaribia [yule mtu], akaanza kutingisha mabega yake kufuatisha mdundo. Kwa mshangao, badala ya kumfukuza mlevi, mwalimu naye akajiunga na ngoma... baada ya muda mfupi, shule nzima ilikuwa inacheza ngoma.
Sabahi: Tena iliishia vipi?
King Majuto: Baada ya saa moja au zaidi ya kucheza ngoma, mwalimu akamshukuru mlevi na kuwaambia wanafunzi umuhimu wa burudani kama kitu cha kuunganisha watu, zana ya kutunza utamaduni na kutunza historia. Kuanzia wakati huo, niliamua kuwa kazi [katika sanaa] inaendana na maslahi yangu. Nikaanza kuifanyia mazoezi, na kujiunga na kwaya ya shule.
Sabahi: Nini kilifuatia baada ya masomo yako?
King Majuto: Mwaka 1966 nilimaliza darasa la nane. Mwaka mmoja baadaye, nilijiunga na Jeshi la Kujenga Taifa. Tulikuwa tunalipwa shilingi 20. Nilibakia kule kama askari hadi mwaka 1970, lakini mmoja wa viongozi wetu alikuwa ananikera sana. Kila nilipokuwa ninatunga nyimbo au kichekesho, alikuwa ananisumbua. Nikaliona jeshi la kujenga taifa [kuwa] sio bandari ya salama kwangu, kwa hivyo nikaacha kazi.
[Baada ya kufanya kazi kadhaa], mwaka 1976 niliamua kujishughulisha na kazi ya sanaa muda wote. Baada ya hapo, nikaanza kujiingizia hadi shilingi 6,000 kwa mwezi kutokana na kuimba na kuigiza, na nikamudu kujenga nyumba yangu ya mwanzo.
Mwaka 1983 nikajiunga na Bendi ya DDC Kibisa ya Dar es Salaam, na mwaka 1985 nikaenda katika Kikundi cha Utamaduni cha Muungano.
Sabahi: Tuelezee kuhusu Kikundi cha Utamaduni cha Muungano.
King Majuto: Tulikuwa tunatengeneza filamu, Kikundi kikaniteua kama mkuu wa idara ya sinema, ambayo ilikuwa inashughulika na filamu na vichekesho ambavyo vilikuwa vinakuza umoja wa Afrika.
Kile tulichokuwa tunatetea kikawa kweli. Tulikuwa tunaomba uwepo umoja wa Afrika, na sasa tunao Umoja wa Afrika. Hii ni moja ya michango mikubwa kabisa kwa Umoja wa Afrika kupitia sanaa yangu.
Sabahi: Ni katika kampeni gani nyingine ulishiriki?
King Majuto: Nimecheza sehemu ya filamu dhidi ya mauaji ya albino. Katika miaka mitatu iliyopita, nchi yetu imekumbwa na wimbi la mauaji ya kiasi cha albino 57 waliuliwa kutokana na imani za kishirikina kwamba kiungo chochote au mfupa wa albino unaweza kumfanya mtu awe tajiri.
Mwaka 2010 nilianzisha kampeni kubwa katika mikoa ya kanda ya ziwa (Mwanza, Kagera, Kigoma, Shinyanga na Mara) kuhusu suala hili na naamini ujumbe wetu ulifahamika. Mauaji ya albino yamesita. Ujumbe wangu kupitia filamu na vichekesho vifupi ulikua wazi. Ulisema, "huwezi kuwa tajiri kwa kuwaua albino". Ilikuwa kampeni ya miezi sita na ilifanikiwa.
Sabahi: Vipi sanaa inaweza kuleta mabadiliko Tanzania?
King Majuto: Bila ya kazi za sanaa katika nchi hii umoja ungekuwa umeharibiwa muda mrefu uliopita. Naendelea kuwakumbusha Watanzania kuwa umoja wetu, amani na utulivu lazima vibakie kuwa kipaumbele chetu cha kwanza. Naweza kusema kwa kujiamini kuwa filamu na vichekesho vyangu vimesaidia kuiunganisha Tanzania kila wakati nchi ilipoingia [katika mizozo].

Monday, March 11, 2013

TISHETI NDEMBENDEMBE NI HATARI KWA DUNGADUNGA


Hii inaitwa Wet T-shirt Competition msichana anamwagiwa maji akiwa amevaa t-shirt nyepesi mpaka chuchu zake zionekane vizuri...

Tamasha hili hufanyika nchini Kenya na hujumuisha michezo mbali mbali pamoja na mziki.

Tamasha hili ambalo hufanyika kila jumamosi ya kwanza ya kila mwezi,hugharimu  kiingilio  cha  sh. 10,000  za  kitanzania  sawa  na  sh.500  ya  Kenya.

JACKLINE WOLPER..... MMMH ...!!

Hatimaye staa wa fi lamu za Kibongo mwenye heshima tele, Jacqueline Massawe Wolper amenaswa ‘laivu’ akiwa amepiga picha chafu inayoonesha sehemu kubwa ya nyeti zake.
 

Kunaswa kwa picha hiyo, kumevunja heshima ya staa huyo aliyekuwa pekee hajapiga picha ya namna hiyo kati ya mastaa wa kike wanaotamba katika tasnia ya fi lamu hapa Bongo.
Wolper alinaswa na mwandishi  wetu katika sherehe ya ‘bethidei’ ya msanii mwenzake iliyofanyika hivi karibuni Ubungo jijini Dar.

Siku za nyuma, staa huyo aliwahi kukataa kupiga picha kama hiyo alipotakiwa kufanya hivyo na mwandishi wetu katika ufukwe mmoja jijini Dar.
Wolper aliapa kamwe hataweza kupiga picha ya namna hiyo katika maisha yake yote

Friday, March 8, 2013

DIAMOND ATINGA KUSWALI NA HERENI MASKIONI

MWANAMUZIKI Nasibu Abdul ‘Diamond’ hivi karibuni aliwachefua waumini wenzake wa dini ya Kiislam baada ya kutinga kwenye Maulidi akiwa amevaa hereni na cheni.

Tukio hilo lilijiri maeneo ya Tandale, Dar ambapo mama yake
aliyemtambulisha kwa jina la Aunt Shani aliandaa maulidi kwa ajili ya kumshukuru Mwenyezi Mungu.
Akiwa mmoja wa waalikwa, Diamond alinaswa akiomba dua sambamba na rafiki yake aitwaye Remeo Jones ‘RJ’ huku akiwa amevaa kanzu safi na balaghashia lakini akaharibu kwa kuvaa hereni na cheni.

Kitendo hicho kiliwachefua Waislam ambapo baadhi walifikia hatua ya kumchana laivu kuwa, alichokifanya kilikuwa kinyume na Uislam.

Tuesday, March 5, 2013

KIJANA ACHARANGWA MAPANGA AKITOKA KUJIRUSHA USIKU

Kijana  Godfrey Masharo  mkazi  wa mjini Iringa  akivuja damu  baada ya  kuchomwa na kitu chenye ncha kali kifuani na watu  wasiofahamika  usiku  wa jana  wakati akitoka  kujirusha disco 

WATU  wasiofahamika   wamemvamia na  kumchoma  na kitu  chenye  ncha kali  kifuani mkazi  wa mjini Iringa Godfrey Masharo (pichani) .

Tukio hilo  limetokea jana usiku majira ya saa 11 alfajiri  wakati  kijana  huyo akitoka  kujirusha katika  kumbi  za starehe mjini  hapo.

Akizungumza kwa  tabu na mtandao huu  kijana  huyo anadai kuwa watu hao  watatu ambao hawafahamiki  kwa majina  walimvamia na kumchoma na kitu hicho chenye ncha kali kifuani na kukimbia .


Alisema  kuwa  tukio  hilo  limetokea eneo la Miyomboni barabara  kuu ya Iringa -Dodoma jirani na jengo la Hazina Ndogo ya  mkoa  wa Iringa .
Hata  hivyo  alisema  kuwa  msaada  wake  ulitoka kwa  wasamaria  wema ambao  walimkuta  eneo hilo akiwa ameanguka kwa  kupoteza fahamu na kukimbizwa  katika  kituo cha polisi kabla ya  kupelekwa Hospitali ya  rufaa ya mkoa  wa Iringa kwa matibabu  zaidi .
Umeona kifuani.....ni hatari sana

Friday, March 1, 2013

OMOTOLA ANG'ARA KWENYE KIPINDI CHA BOUNCE -USA


Muigizaji wa Nollywood, Omotola, Jalade- Ekeinde, ameanza kuonekan kwenye televisheni za Marekani, kwenye kipindi kiitwacho Bounce

Nyota huyo ambaye amekuwa Marekani kwa muda sasa ameanza kuonyesha uwezo wake mbele ya wakali wa Hollwood nchini Marekani

Baadhi ya wasanii mbalimbali kutoka Nigeria walishindwa kung'aa lakini msanii huyo amefanikiwa kushiriki kwenye tamthilia nchini Marekani

Katika tamthilia hiyo Omotola amecheza na Kimberly Elise