Pages

BRAND NEW MUSIC

metty magese

metty magese

Listen & Download

http://mdundo.com/a/32626

Thursday, May 31, 2012

WEMA SEPETU ACHUMBIWA NA MWINYI MACHOZIMsanii ambaye hajawahi kukaukiwa na matukio yenye kufaa kutengeneza vichwa vya habari katika vyombo vya habari nchini, Wema Abraham Sepetu, kwa mara nyingine ametawala vyombo vya habari baada ya tukio lake la usiku wa jana la kuvishwa pete ya uchumba na msanii wa bendi ya Machozi, anayekwenda kwa jina la Mwinyi.
Tukio hilo ambalo limevuta hisia za wapenzi wa masuala ya udaku na burudani nchini, lilijiri katika ukumbi wa Maisha Club, jijini dar es salaam, usiku wa kuamkia leo, ambapo lilishuhudiwa na mashabiki lukuki wa bendi ya Machozi waliokuwa wamejazana hapo kwa ajili ya burudani ya muziki uliokuwa ukiporomoshwa na bendi hiyo.
Hata hivyo, tofauti na ambavyo imechukuliwa na watu wengi kuwa Wema amepata mchumba mpya na ndio alikuwa akimvisha rasmi pete ya uchumba, ukweli ambao umewekwa wazi ni kuwa, mwanadada huyo alihusika katika tukio hilo kama sehemu ya maandalizi ya filamu yake mpya itakayokwenda kwa jina la Super Star.
Movie hiyo inatarajiwa kuelezea maisha halisi ya msanii huyo ambaye pia aliwika katika medani za ulimbwende, na Mwinyi atashiriki katika filamu hiyo akiigiza nafasi ya mwanamuziki Diamond, ambaye alikuwa mpenzi wa Wema na ambaye alimvisha pete ya uchumba lakini wakamwagana baadae kutokana na mikasa baina yao kuzidi kushamiri.
Kibwagizo: Hata hivyo, Wema anajulikana kuwa hajatulia, unadhani itashangaza kesho kusikia kuwa tukio hilo mbali ya kuwa sehemu ya filamu, lilikuwa pia tukio rasmi la kuwaunganisha wawili hao?

CLUB SILK ,SEAN NA LINDA LISA HAPATOSHILinda Lisa during her night
Elyt Magazine boss Sean Ndawula is has branded Club Silk publicist Linda Lisa brainless. Sean is accusing Lisa of stealing his idea and then using it to start her own theme night at Silk.
Sean two months back launched Bahamas night at the same club which was a huge success with several hot chics dressed in barely nothing showcasing what their mama’s gave them.
However, just last week Lisa launched Caribbean night which is no different from Sean’s Bahamas theme night. Some of the revelers who attended say the set up was the same apart from the theme names.
Sean’s close pals are now accusing Lisa for lack of brains and instead she is riding on other people’s ideas to make a living. Shockingly, they can’t believe that she is holding it at the same venue where he launched his.
Most revelers have vowed to snub both nights saying they can’t be served using the same menu.

MISS KIGAMBONI CITY NI BALAA

 Baadhi ya warembo wanaotarajiwa kushiriki shindano la Miss Kigamboni City 2012 wakipozi kwa picha katika mazoezi yao yanayoendelea kwenye ukumbi wa Break Point katikati ya jiji la Dar es Salaam.Shindano hilo limepangwa kufanyika Juni 15 katika ukumbi wa Navy Beach Kigamboni, jijini Dar es Salaam.

MISS TABATA KUWAKA MOTO KESHO

Shindano la kusaka Miss Tabata 2012 linafanyika kesho katika ukumbi wa Da’ West Park, Tabata.
Mratibu wa shindano hilo Joseph Kapinga amesema leo  kuwa bendi za Mashauzi Classic na Mashujaa zitawasindikiza warembo 19 watakaopanda jukwaani kuwania taji hilo.
Mratibu wa shindano hilo lililoandaliwa na Bob Entertainment na Keen Arts  alisema kuwa mshindi wa kwanza atazawadiwa Sh 500,000/- na king’amuzi ambayo imelipia miezi sita yenye thamani ya sh 800,000 iliyotolewa na Multichoice.
Mshindi wa pili atapata sh 500,000, mshindi wa tatu sh 350,000 wakati washindi wa nne na watano kila moja atapata sh 200,000.
Kapinga alisema warembo watano watawakilisha Tabata kwenye shindano la Miss Ilala.
Warembo wengine watakaoingia 10 bora kila moja atapata sh 100,000 wakati waliyosalia watapata Sh 50,000 kila moja.
Kapinga alisema shindano hilo pia litatumika kwa ajili ya kusherehekea miaka 10 tangu kuasisiwa kwa shindano la Miss Tabata.
“Shindano la mwaka huu sio la kukosa kwani litakuwa ni la aina yake ukizingatia kuwa litatumika kusherekea miaka 10 tangua kuanza kuandaa Miss Tabata,” alisema Kapinga.
Alisema warembo waliyowahi kushinda mataji mbalimbali ya shindano hilo, pia wamealikwa kusherehekea miaka 10 ya Miss Tabata.
Shindano hili limedhaminiwa na Dodoma Wine, Redds, Integrated Communications, Fredito Entertainment, Multichoice Tanzania, Screen Masters, Kitwe General Traders, Step In Electronics, Brake Point, Atriums Hotel na Lady Pepeta.
Mrembo anayeshikilia taji la Tabata kwa sasa ni Faiza Ally.
Warembo wa Tabata wamekuwa wakifanya vizuri katika mashindano ya Miss Tanzania ambapo mwaka juzi Consolata Lukosi alishinda nafasi ya tatu kabla ya kutangazwa kuwa balozi wa kinywaji cha Redds.
Katika shindano la mwaka juzi Juliet William pia alishinda nafasi ya tatu katika ngazi hiyo ya taifa.

MISS UGANDA 2012 KUTIMUA VUMBI JUNE 1

               Anita Baruti

It is that time of the year again when gals from across the country come to vie for the position of most beautiful in the country. The search is on: a total of twenty four beauties turned up on Wednesday for the pre-selection of Miss Uganda 2011-2012 edition at Club Silk.
The show kicked off at approximately 10:45 am with the young beauties in bikinis trying their level best to meet the qualification and answer questions posed by the different judges.
On the panel of judges was no nonsense Brenda Nanyonjo,  Ayiekoh Lillian from Hot 100, Patricia Oluch from Atuki films.  They were shocked to find that most of the contestants were only interested in modeling rather than the big crown of `Miss Uganda`. Like it is for first timers, nervousness was quite evident but as the event went on, they picked up the courage. Twenty one gals went through to the next level which is slated for this Saturday where ten Miss Uganda finalists will be selected.
The pageant which is  sponsored by Redds, main sponsor; Red Pepper, the official Miss Uganda News paper, WBS TV, Capital FM, Silk Events, Club Silk among others is organized by Brenda Nanyonjo under the outfit Kezi International. Below are some of the hopefuls that went through to the second stage. Find all your Miss Uganda updates in the Red Pepper

Anita, Grace and Benita at Silk during the pre-selection event

Benita Namukwaya was among the gals that turned up for Miss Uganda pre-selection

Juicy Nabachwa Mariam wowed the people with her confidence; something that saw her in the finalists


Sylvia Namutebi was a contestant in last year's peagent, now she is back

LUCY STEPHANO NDIYE MISS MBULU 2012Hayawi hayawi hatimaye yakawa, hatimaye kitendawili cha nani kuibuka kidedea yaani atakayevikwa umalkia wa wilaya ya Mbulu kikateguliwa jana usiku katika ukumbu wa Kituo cha Jamii (Community Centre) kwa wawakilishi kutoka Haydom kuibuka kidedea kwa kushika nafasi za juu kabisa.

Lucy Stephano ambaye ni Miss Haydom No.2 kiunoni,hakuamini masikio yake pale alipotangazwa mshindi na kujinyakulia kitita cha shilingi laki tatu (300,000/=) huku Linah Emmanuel ambaye alikuwa Miss Haydom No. 3 akiibuka mshindi wa pili na kuweka kibindoni kitita cha shilingi laki mbili (200,000/=).

Tuesday, May 29, 2012

STELLA AGUSTINO NDIYE MISS ILEMELA 2012

Mshindi wa taji la miss Ilemela 2012 Stella Agustino (katikati) akiwa na mshindi wa pili Hapiness (kushoto) na mshindi wa tatu
Warembo walioingia kumi bora miss Ilemela 2012.
Sharowbarow President Bob junior akimalizaaaaa...
Flash na sehemu ya Gold Crest Hotel.
Mshiriki namba 3.
Mshiriki namba 9.
Mshiriki namba 4.
Pichani huyu si mshiriki miss Ilemela 2012 bali ni sehemu ya Onyesho la mavazi ya Harusi toka Munira Classic.
Mc wa tukio Mr. G. Sengo(gsengo blog) toka Clouds Fm Mwanza.
Meza ya majaji chini ikitafakari muonekano wa kwanza kupitia open show ya Miss Ilemela 2012.
Ze pipooo.
Wadadaz wakipata flash kwa blog....
Hapa Chief Judge Muhksin Mambo toka Star Tv (nyuma ya mshiriki no 7) alipokuwa akitaja kumi bora.
Ze flawaz..
Kipaji toka moyoni mshiriki wa kinyang'anyiro miss Ilemela Stela akionyesha kipaji cha kucheza wimbo wa Fally Ipupa - Bakanja.
Mshiriki wa kinyang'anyiro cha Miss Ilemela  Hapiness akichora ndani ya kuonyesha vipaji.
Kipaji toka moyoni mshiriki Zaifath kipaji cha kuimba.
Afisa Promosheni wa Nyanza Bottling Co. LTD watengenezaji wa soda jamii ya Coca cola Mr.Rutta, akimkabidhi mshindi nafsi ya 3 cheki ya shilingi laki mbili.
Afisa Promosheni wa Nyanza Bottling Co. LTD watengenezaji wa soda jamii ya Coca cola Mr.Rutta, akimkabidhi mshindi wa nafsi ya pili Hapiness, cheki ya shilingi laki tatu.
Afisa Promosheni wa Nyanza Bottling Co. LTD watengenezaji wa soda jamii ya Coca cola Mr.Rutta, akimkabidhi Miss Ilemela 2012 Stella Agustino, cheki ya shilingi laki tano.

Monday, May 28, 2012

SARAH PAUL NDIYE MISS TABORA 2012

 Mshindi wa redd's miss Tabora 'Sarah Paul '
mshindi wa taji la Redds Miss Tabora 2012 Sarah Paul katikakati akiwa na washindi wengine wawili Glory Mongi kulia na Alice Amour kushoto mara baada ya kufanikiwa kutawaza washindi wa taji hilo na kufanikiwa kuingia katika kinyanganyiro cha kanda kuelekea kwenye fainali ya Redds Miss Tanzania 2012

FLAVIANA MAEDA NDIYE MISS KURASINI 2012

 Miss Kurasini 2012,Neemadoreen sivery akiwa ameketi katika kiti baada ya kuvikwa taji hilo.

Tano bora ya Miss Kurasini ikiwa katika picha ya Pamoja kabla ya kutangaza mshindi.(kutoka kushoto)
1. FLAVIANA MAEDA ,2. NEEMADOREEN SYLVERY,3. LILIAN JOSEPH,4. BETTY PETER 5. ANGEL GASPER.

 Warembo waliokuwa wakiwania taji la Redds Miss Kurasini 2012 wakicheza show ya ufunguzi wakati wa shindano hilo Mwishoni mwa wiki iliyopita.

EAST AFRICA FASHION EXTRAVAGANZA

 A model showcasing Afrikalos collection by Pan African Designer Mustafa Hassanali during the East African Fashion Extravaganza held in Kampala on May 26 2012
 A model showcasing Afrikalos collection by Pan African Designer Mustafa Hassanali during the East African Fashion Extravaganza held in Kampala on May 26 2012
 A model showcasing Afrikalos collection by Pan African Designer Mustafa Hassanali during the East African Fashion Extravaganza held in Kampala on May 26 2012
 A model showcasing Afrikalos collection by Pan African Designer Mustafa Hassanali during the East African Fashion Extravaganza held in Kampala on May 26 2012
 A model showcasing Afrikalos collection by Pan African Designer Mustafa Hassanali during the East African Fashion Extravaganza held in Kampala on May 26 2012
 A model showcasing Afrikalos collection by Pan African Designer Mustafa Hassanali during the East African Fashion Extravaganza held in Kampala on May 26 2012
 A model showcasing Afrikalos collection by Pan African Designer Mustafa Hassanali during the East African Fashion Extravaganza held in Kampala on May 26 2012
 Pan African Designer Mustafa Hassanali during the finale of his collection at the East African Fashion Extravaganza held in Kampala on May 26 2012

FINA REVOCATUS NDIYE MISS IFM 2012

Mshindi wa Redd’s Miss IFM 2012, Fina Revocatus (katikati) akiwa na Mshindi wa Pili, Jane Augustino (kushoto) na wa Tatu Theresia Issaya muda mfupi baada ya kumalizika kwa shindano lao hilo lililofanyika usiku wa kuamkia leo kwenye ukumbi wa Hoteli ya Blue Peal, Ubungo Jijini Dar..

Top five ya Miss Ifm 2012.

DIAMOND APOFUNIKA BIG BROTHER STARGAME

  MWANAMUZIKI nyota wa Tanzania wa Bongo flava, Naseeb Abdul ‘Diamond Platnumz” juzi usiku aliweza kuuteka umati wa wageni maalum uliofurika kwenye ukumbi wa  jumba la shindano la Big Brothe stargame, na afrika kwa ujumla kwa kupiga shoo kali na ya aina yake ,nchini Afrika Kusini.
Katika shoo hiyo ambayo pia ilishuhudiwa na mamilioni ya watazamaji, ulimwenguni kote kupitia ving’amuzi vya Dstv,  Diamond aliweza kudhihirisha uwezo wake huo kwa kuangusha bonge la shoo  ikiwemo kwa wimbo wake wa ‘Mawazo’ ambao  uliwachanganya watu mbalimbali na kuamka vitini mwao na kupanda  jukwaani na kucheza nae.
Diamond kama kawaida yake, aliweza kuvalia vilivyo, alikonga nyoyo za mashabiki hao kwa staili yake ya uchezaji ikiwemo ya kuigiza kama anaanguka pamoja na ile ya miondoko ya msanii wa Orijino komed, Joti, hadi anamaliza shoo hiyo mashabiki hao walikua na hamu ya kumuona na kusikia nyimbo zake.
Awamu ya pili, Mshereheshaji mkuu wa shindano hilo, Osakioduwa maalufu, IK, aliweza kumwita tena jukwaani Diamond ilikuzungumza machache, Diamond bila hiyana aliwashukuru mashabiki kwa sapoti waliompa na kuwapongeza wote.

“Nimefarijika sana,nawapendeni wote Big brother, funs, na wote” alisema Diamond na baadae IK, alimuomba apige wimbo wa mwisho wa kufungia shoo hiyo na kuporomosha kibao cha ‘Moyo wangu’ ambacho nacho kiliwachanganya zaidi mashabiki huku kivutio lkikubwa kikiwa juu ya uchezaji wake huo wa Kijoti.
Katika shoo, hiyo, mshiriki wa Zambia, Mampi aliweza kutolewa kufuatia kupata kura chache zilizopigwa baada ya kuingia kwenye hatari yeye na wenzake wawili,Maneta na Lady May.