Pages

BRAND NEW MUSIC

metty magese

metty magese

Listen & Download

http://mdundo.com/a/32626

Wednesday, December 29, 2010

ILIVYOJILI 24 DESEMBA KATIKA GIRAFFE UNIQUE MODEL 2010

     siku moja kabla ya show ndai ya kifaru hall

siku ya fainali katika jukwaa moja kumsaka huyo unique
  siku ya tarerhe 13 desemba siku ya ufunguzi wa kambi ya mazoezi tulifungua kwa kukata keki
 siku tuliotembelea Global publishers bamaga
 Tanga beach resort iliyopo Tanga ni mja ya hoteli ambazo zinamilikiwa na mdhamini mkuu mr. Bekon

TANGA BEACH RESORT

KARIBU KATIKA HOTELI YENYE SIFA ZA KILA NAMNA ILIOYOPO MJINI TANGA,MENGI ZAIDI NTAWAJUZA PUNDE....TANGA BEACH RESORT

Sunday, December 26, 2010

MSHINDI WA UNIQUE 2010 MODEL APATIKANA

   Mshindi wa Giraffe Unique Model, Asia Dachi (katikati) akiwa na furaha mara baada ya kutangazwa mshindi wa shindano hilo(unique model of the year 2010).Kulia ni mshindi wa pili, Diana Mainanson na mshindi wa tatu Mariam Rabii. shindani lilidhaminiwa giraffe ocean view hotel,channel ten,magic fm,Global pubishers,mohammed enterprises,Truworths,mtaakwamtaablog na uniqueentertz blog.

 Nawashukuru wate,vyombo vya habari,wadau na ushirikiano mzuri na sapoti kubwa aliyonipa Bwana CHARLES BEKON KWAKUNIDHAMINI NA  NIMEFANIKIWA KUFIKISHA JAHAZI UKINGONI na kufanikiwa kuwatangaza wanamitindo kumi katika soko a mitindo Tanzania.

NA MWANDISHI WETU

DANSA wa zamani Sammy Cool, ameanzisha mashindano ya kucheza muziki yanayotarajiwa kuanza mwezi ujao, jijini Dar es Salaam.
Akizungumza na Bingwa, Dar es Salaam jana, Sammy Cool alisema kuwa mashindano hayo anatarajia kuyapa jina la Black Moses Dancing Competition, lakini baada ya kupata ridhaa ya ndugu za marehemu wa mcheza dansi huyo wa zamani.
Sammy Cool alisema kuwa lengo la mashindano hayo, mbali na kuendeleza vipaji vya madansa, pia ni kumuenzi Black Moses aliyekuwa dansa maarufu nchini kutokana na umahiri wake katika fani yake hiyo.
Alisema kuwa anatarajia kuwashirikisha wadau mbalimbali katika mpango huo, lengo likiwa ni kuhakikisha mashindano hayo yanafanyika kwa ufanisi zaidi kama alivyokusudia.
“Kwa sasa kuna vipaji vingi vya madansa hapa nchini, lakini hakuna mpango wowote wa kuwasaidia…hivyo nimeona ni vyema nikaanzisha mashindano haya ili kila mwenye kipaji cha kucheza muziki,” alisema.
Alisema kuwa mashindano hayo yatakuwa yakifanyika zaidi ya mara moja kwa mwaka katika maeneo tofauti nchini, japo yataanzia jijini Dar es Salaam na baadaye kuhamia mikoani.
Aliwataka madansa wote wenye vipaji, zaidi wakiwa ni chipukizi kukaa mkao wa kula kwani shindano hilo linatarajiwa kuwa la aina yake na lenye mvuto wa kipekee.
Sammy Cool ni miongoni mwa madansa waliotamba nchini kutokana na uhodari wake wa kucheza muziki, akiwa ametwaa tuzo kadhaa nchini.                UKWELI KUHUSU SHUTUMA DHIDI YANGU,UNIQUE MODEL IMEANDAMWA NA MAMLUKI,PESA YATUMIKA KUMZALILISHA NA KUMCHAFUA MAGESE,MCHEZO MCHAFU WAGUNDULIKA DHIDIN YANGU.

  Nimesikitishwa na baadhi ya wanakamati wangu kuwa wasaliti kwa kupandikiza chuki kwa washiriki kuwahimiza waongee mambo ya uzushi na unafiki katika vyombo vya habari kwa lengo la kuniharibia shindano kwa kunivunjia uaminifu kwa jamii na wadhani.


TUMEKUWA NA MAMLUKI WENGI KATIKA MCHAKATO WA KUANDAA SHINDANI HILI KWANI TOKA AWALI TULIWAJULISHA WASHIRIKI NA VYOMBO VYA HABARI KUWA WAMEKUWA WAKITUMWA WATU MBALIMBALI KULETA MAMBO YA UZUSHI NA MAJUNGU HUKU WAKITUMIKIA NAFASI MBILI TOFAUTI


  Unique model ni shindano lililokuja kwa kasi lakini limeibua maadui wengi wanaolichukia shindano hili ikiwa hata wale wa ndani ya kamati kupeleka habari za uzushi katika vyoimbo vya habari mfano dhahili katika  Gazeti la MWANACHI  LILIANDIKA HABARI ZIMELETWA NA MMOA WA VIONGOZI WA SHINDANO LA UNIQUE MODEL.......jiulize sasa.. KIKULACHO KI NGUONI MWAKO,kama mtu anaweza kuandika habari ya kuchafua na kuituma kwenye vyoimbo vya habari je atashidwa kueneza maneno ya uzushi na kuwafatab chumbani washiriki waje kuongea maneno ambayo aliwasulutisha wayaseme kama alivyowanganga kuzungumza KATIKA TV YA TAIFA(...)

 MTU HUYU ALIDILIKI KUWASHAWISHI MAJAJI KUSUSIA MAAMUZI NA KUWASHAWISHI WASHIRIKI KUFANYA FUJO NA KUGOMEA KILE KILICHOTANGAZWA PALE JUKWAANI KWANI WAO HAWAKUWA NA WAZO HILO ALIONGEA MMOJA WA WASHIRIKI


WATNZANIA MIMI KAMA MWANDAAJI NAOMBA RADHI KWA YOTE YALIYOJITOKEZA ILA NAOMBA MTAMBUE KUWA KUNA MIKONO YA WATU WANAOTUMIA PESA,MAJUNGU,FITNA,UZUSHI NA KUWARUBUNI WASHIRIKI NA WATU WA KARIBU KUSAMBAZA MANENO YA UCHOCHEZI KUNIHARIBIA SHINDANO WABAKI PEKEAYO,ILA IPO SIKU UKWELI UTAJULIKANA TU KWA WATANZANIA WOTE....

INANIUMA SANA MTU KUMNUNUA MODEL WANGU AZUNGUMZE UONGO KATIKA MEDIA...HATA  YESU ALILETA UZIMA LAKINI ILIFIKA KIPINDI WATU WALIMTEMEA MATE,KUMDHIHAKI NA NA KUMDHALILISHA,KWANI BAADHI YA WATU HAO WALIONEKANA NI WENYE FURAHA SANA BAADA YA KUFANIKIWA MPANGO WAO AMBAO ULISUKWA KWA MUDA KADHAA NA KUWATUMIA WATU WA KARIBU YANGU KUFANIKISHA MKAKATI HUO


 MCHANGO WANGU KATIKA SANAA YA MITINDO NI MKUBWA LAKINI NDO UMEFIKA WAKATI AMBAO JIWE MOJA KUKATAA KUKAA KATIKA JIWE JENZAKE,PIA MEDIA ZOTE MNATAKIWA KUBALANCE STORY ZENU SIO KILA MNACHOAMBIWA TU MNAPELEKA HEWANI....INA MAANA LEO MTU AKISEMA AKISEMA MAGESE NI MCHAWI MNARUSHA TU....!?? TAFUTENI EVIDENCE KWANZA NDO MRUSHE SIO MNACHAFUA TU WATU NA BIASHARA ZAO.

MSHIRIKI WA GIRAFFE UNIQUE MODEL 2010 CHRISTINA PETER AWA BALOZI WA MeTL…!!!

Mshiriki namba 2 katika Shindano la Giraffe Unique Model 2010 Christina Peter ambaye amechaguliwa na Kampuni ya Mohammed Enterprises (MeTL) kuwa balozi wa kampuni hiyo katika kushiriki maswala ya kijamii pamoja na kutangaza bidhaa za Kampuni ya Mohemmed Enterprises kwa mwaka mmoja.

Kushoto ni Mwakilishi kutoka kampuni ya Mohammed Enterprises Zainul Mzige mara tu  baada ya kumkabidhi maua  kwa Balozi wa Kampuni ya MeTL  Christina Peter
Balozi wa MeTL Christina Peter katika picha ya pamoja na wazazi wake Mr & Mrs Kitine.
Picha za Shindano la Giraffe Unique Model 2010 zinafuata kaa tayari.

Wednesday, December 22, 2010

Tuesday, December 21, 2010

WASHIRIKI WA GIRAFFE UNIQUE MODEL WAENDELEA NA MAZOEZI KAMBINI.

Hapa wakifanya mazoezi ya kucheza mziki
Hapa wakipata mafunzo ya kutmbea (cat-walk) kutoka kwa mwalimu wao Victoria Martin.
Hapa wakipata maelezo toka wka victoria martin (matron) jinsi ya kuingia kwenye jukwaa

HAWA NDIO WASHIRIKI WA GIRAFFE UNIQUE MODEL 2010.

Shindano hili ltafanyika katika hotel ya Giraffe Ocean Vew hotel tarehe 24/12 2010 kwa kiingilio cha Tsh. 20,000/= viti vya kawaida na Tsh. 30,000/= kwa viti maalum. OFFER ya punguzo la bei ya vyakula na vinywaji siku ya tukio! Tiketi zitaanza kuuzwa jumatatu ya tarehe 20/12/2010 na zitpatikana  duka la nguo la Truworths (mlimani city), Global publisher (bamaga), Giraffe Ocean Vew hotel (Africana / kunduchi) na stears (posta).
Zeinul Mnzige (kulia) akikabidhi zawadi ya vitenge kwa Mratibu mkuu wa Giraffe Unique Model,Methuselah Magese ikiwa ni moja ya zawadi zitakazokabidhiwa kwa warembo hao.


UNIQUE MODEL ni shindano la kutafuta wanamitndo wenye sifa za kipekee. Kwa mwaka huu limepewa jina la Giraffe unique model kutokana na Hoteli ya Giraffe Ocean vew ambayo iko katika hadhi ya nyota nne kuwa mdamini mkuu wa shindano hili.
Lengo la kuweka kambi ni kuwakusanya washiriki sehemu moja na kuwapa elimu kuhusu masuala mbalimbali yahnayo husu mitindo, maadili na namna ya kuishi na jamii yenye tabia tofautitofauti. Kwa upande wa unique entertainment lengo lake ni kuinua na kuendeleza vipaji vya sanaa ya uanamitindo hapa nchini.
Hiki ni kitu kipya tumekuja nacho kutokana na utafiti tuliofanya na kugundua soko la mitindo hapa nchini na hata nje ya nchi linahitaji wanamitindo wa aina gani ili kila mtu avutiwe na tasnia hii ndio maana unique entertainment tumeamua kutengeneza wanamitindo mabao watakidhi na watakua bora katika soko la uanamitndo kwa hapa nchini.
Shindano hili litafanyika 24th desemba siku ya ijumaa kuanzia saa mbili usiku ambapo tutakua pia na burudani kutoka kwa wasnii mbalimbali wa kizazi kipya na kiingilio kitakua ni tsh. 20,000/= kwa viti vya kawaida na tsh. 30,000/= kwa viti maalum.
Kwa upande wa udhamini tukimuacha Giraffe ocean Vew Hotell kama mdhamini mkuu pia tunao wadhamini kama Robbialack paints, Mohamed enterprises, Channel Ten, Global Publishers, Truworths, Ally Rehemtullah, Galacha wear mtata kwa mtaa blog na uniqueentertz blog.
Kwa kumalizia tu ni kwamba tiketi za tukio zitaanza kupatikana muda wowote kuanzia leo na tunatarajia zitakua zikipatikana katika vituo mbalimbali kama vile Truworths (mlimani city), Global publisher (bamaga), Giraffe Ocean Vew hotel (Africana / kunduchi) na stears (posta).

Kuhusu UNIQUE ENTERTAINMENT

UNIQUE ENTERTAINMENT ni kampuni iliyesajiliwa kisheria nchini Tanzania chini ya BASATA kufanya kazi za mitindo na burudani.
Kwa mawasiliano zaidi:
e-Mail: uniqueentertz@yahoo.com
web: www.uniqueentertz.blogspot .com
Tel: +255 714 796 622, +255 769 378 747

Mratibu wa shindani wa Giraffe Unique Models 2010

Methuselah Magese

Sunday, December 12, 2010

KAMBI YA WASHIRIKI WA GIRAFFE UNIQUE MODEL 2010 KUFUNGULIWA RASMI 13 DESEMBA

  Kambi ya washiriki wa shindano la  kumtafuta mwanamitindo bora wa mwaka 2010 katika Shindano jipya la mitindo liitwalo Giraffe unique model 2010 ambapo itakuwa ndani ya hoteli yenye hadhi nne Giraffe Ocean view  iliyopo jijini Dar es salaam.Event ni tarehe 24 desemba saa mbili usiku.
  Kambi hiyo itakuwa ni ya wiki mbili ambapo washiriki  wanaingia ktarehe 13 desemba na kutoka siku ya krismas asubuhi 25 desemba baada ya kumalizika kwa shindano hilo usiku wa tarehe 24 siku ya mkesha wa krismas.
  Nia na madhumuni ya kuweka kambi ni kuwakusanya washiriki wakae sehemu moja kwaajili ya kuchuliwa kimitindo,kuondo usumbufu wa kuwakusakusanya kila siku,kupewa kanuni za kutunza urembo wao wakiwa wanamitindo na pamoja kuwafunza namna ya kuishi na jamii,catwalk,dance,michezo,maadili na kutembelea sehemu mbalimbali ya jiji la Dar es salaam kujifunza na kujionea mambo kadhaa ambayo hawakuwai kuyaona wakiwa nyumbani.

Friday, December 10, 2010

WASHIRIKI WA SHINDANO LA GIRAFFE UNIQUE MODEL WATEMBELEA MLIMAN TV NA KUFANYA KIPINDI CHA MITINDO NA UREMBO NA MWANADADA SHIKiNA OTHMAN.

Hili ndio gari kutoka Gioraffe ocean vew hotel ambalo washirki hulitumia katika safari za hapa na pale mjini katika msimu wa Giraffe unique model 2010 (seasone one) ambapo fainali zake zitakuwa 24 desemba katika hoteli ya Giraffe ocean view
Hapa washiriki wakiwa mlimani city ambapo walitembelea na kupata chakula cha mchana samakisamaki kabla ya kwenda mlimani tv.
Sarari ya kwenda mlimani tv ilianza......
Hatimae wakafika eneo la  mlimani tv na make-up zikaanza...daaah!!
Kabla ya kuanza kipindi washiriki walijipiga ma make up ya kutosha na kipindi kikaanza kama ifuatavyo na mwanadada Shikinah.
Kipindi kilirikodiwa dizaini hiyo na baadhi ya washiriki ambao walijitoa muhanga kujinadi kwaajili ya fainali 24 desemba hii.
Baada ya kumaliza kurikodi kipindi watu walijiachia na kamera mapicha kadri watavo ndani ya eneo la mlimani tv.
SHUKRANI KWA MLIMANI TV KWA KUTUPA SAPOTI YA NGUVU TUNAHESHIMU SANA UEPO WENU KATIKA SHINDANO HILI LENYE MVUTO WA AINA YAKE