Pages

BRAND NEW MUSIC

metty magese

metty magese

Listen & Download

http://mdundo.com/a/32626

Friday, November 30, 2012

VIJANA WALA BATA JIJINI DAR HAWA HAPAMartin Kadinda akiwa ameweka mapozi na Jaqueline patric (mke wa mtu),wakila bata moja ya siku za ujana wao,kinachoendelea mi sijui. http://3.bp.blogspot.com/-ysjTduiDWZ4/UJd-S_GeJsI/AAAAAAAAMyY/Dl2HJwlFy7s/s640/zungo7.jpg

Thursday, November 29, 2012

MPANGO MZIMA WA SWAHILI FASHION WEEK HUU HAPA

WANACHUO MACHANGUDOA WASAKWA UDOM

RAIS wa Serikali ya Wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOSO), Paul Yunge, amesema kuwa wanafanya uchunguzi wa kina ili kuwanasa wanafunzi wa chuo hicho wanaojihusisha na biashara ya kujiuza kimwili ili wawachukulie hatua.

Yunge alifafanua kuwa, wanafunzi watakaobainika kujihusisha na vitendo hivyo watachukuliwa hatua kali za kinidhamu ili iwe fundisho kwa wengine.

Akizungumza na waandishi wa habari mjini Dodoma, Yunge alisema kazi ya kufanya uchunguzi tayari imeanza na wanategemea wakati wowote watabaini ukweli kuhusiana na jambo hilo.

Alifafanua kuwa, wanafunzi wanaojihusisha na vitendo hivyo wanakidhalilisha na kukishushia heshima chuo hicho ambacho kimsingi kinapaswa kuwa kioo.

“Ni aibu sana kama watu wamekuja UDOM kusoma na badala yake wanageuka na kufanya biashara ya kujiuza ambayo ni ya kudhalilisha utu wao pamoja na chuo kwa ujumla. Jambo hili lazima tulifanyie kazi,” alisema.

Yunge alidai kuwa wamefikia uamuzi huo baada ya taarifa hiyo kuripotiwa na vyombo vya habari, kitendo ambacho kimeisononesha nchi nzima ukiwemo uongozi wa chuo pamoja na wazazi wa wanafunzi hao.

Hatua ya serikali ya chuo kuanza uchunguzi imekuja baada ya baadhi ya vyombo vya habari wiki iliyopita kuripoti kuwa baadhi ya wanafunzi wa chuo hicho wanajiuza katika sehemu mbalimbali za mji wa Dodoma.

VIBAKA WALIIBA VITU VYA SHARO MILIONEA BAADA YA AJALI KUTOKEA


 Kitendo cha baadhi ya wananchi wa kijiji ilipotokea ajali ya sharo milionea kumwibia 
 kila kilichowezekana kubebeka kimelaaniwa na watanzania waungwana.
 Kumbukeni Sharo ni mtanzania mwezetu,ndugu yetu na msanii wetu mlitakiwa kuwa na utu na sio kukimbilia kuiba vitu vya thamani bila kujali thamani ya mtu.
 Marehemu sharo milionea alikutwa na singilendi na boxa tu vitu vingine kama siumu,cheni,nguo,wallet, redio ya gari ,n.k havikupatikana kutokana na watu kugeuza ajali ya msanii huyo kuwa mtaji kwa watu hao wenye tamaa kuliko utu.
 Blog hii ya jamii inakemea vitendo hivyo vya kupora mali za ndugu zetu pindi wanapopata ajali,wanapaswa kutoa msaada na sio kuona ndiyo muda wa neema kuchukua vitu vya wajeruhiwa au marehemu.

PICHA ZA MAZIKO YA SHARO MILIONEA


Swaiba King Majuto akimwaga mchanga ishara kumuaga rafiki kipenzi chake sharo milionea.

Wednesday, November 28, 2012

PICHA ZAIDI MSIBA WA SHARO MILIONEA HIZI HAPA

Wasanii wa bongo flava pia walifunga safari kwenda kumzika Sharo milionea ambapo amezikwa leo mchana karibu na nyumbani kwao.

WANYANGE WA MISS EAST AFRIKA HAWA HAPA

.


Burundi


Eritrea


Ethiopia


Kenya


Rwanda


Tanzania


Uganda


Somalia

SHARO MILIONEA AZIKWA LEO KWA MAJONZI MAZITO

 
 
 Mwili wa Marehemu Sharo Milionea ukiswaliwa mapema mchana huu kabla ya kupelekwa kwenye nyumba yake ya milele 
 
 
 Rafiki mkubwa wa marehemu Sharo Milionea,Mzee Majuto akiwa ameshikwa mkono na Msanii wa filamu JB wakielekea kwenye mazishi mapema mchana huu,Muheza mkoani Tanga.

PICHA ZA AJALI YA SHARO MILIONEA

 
 
 

Gari aina ya Harrier lenye namba za Usajili T478BVR lililokuwa likiendeshwa na Marehemu  Hussein Ramadhani Mkieti (27) maarufu SHARO MILIONEA alifariki duni juzi katika ajali ya gari kijii cha Maguzoni Soga Wilaya ya Muheza jijini Tanga likionekamna katika taswira tofauti baada ya kupata ajali hiyo na kuondoa uhai wa Msanii hiyo.

Tuesday, November 27, 2012

CHANZO CHA AJALI NA KIFO CHA SHARO MILIONEA HIKI HAPA

 Habari za uhakika kuhusiana na chanzo cha kifo cha msanii Hussein Ramadhan a.k.an Sharo milionea ni kwamba gari yake aina ya Toyota harrier ilipata pancha tairi la upande wa kulia na kukosa mwelekeo kisha ikaacha njia na kuelekea mtaroni lakini ule mtalo haukuizuru sana gari hiyo ikaruka na kuingia katika shamba la maindi.
 Kitu kilichoshangaza wengi ni sehemu ambayo si hatarishi sana kiudereva sababu iko tambarare na kona si kali eneo hilo.
 Chanzo cha habari kinaendelea kufafanua kuwa baada ya gari kuacha njia ilienda kugonga mti mkubwa na kuung'oa baada ya kuuchana katikati kutokana na gari ilivyokuwa mwendo kasi.
Mwili wa marehemu ulitupwa nje ya gari baada ya kugonga mti huo ambapo gari hiyo iliharibika vibaya kuanzia kwenye roof hadi vioo vyote kupasuka japo vizuizi vilifunguka lakinini havikusaidia.
 Baada ya kishindo kikubwa cha mlio wa pancha kilisikika kwa wakazi wa kijiji hiko na kuamua kujitokeza kujua nini kimejili pale na wakati wanafika hapakuwa na mwili wa marehemu katika  eneo la tukio,ndipo mama mmoja aligundua mwili wa msanii huyo mita chache kutoka gari ilipogonga mti na kuharibika vibaya.
 Mganga mkuu wa hospitali teule ya Muheza amesema kuwa chanzo cha kifo cha Sharo ni kubonyea kwa kichwa ikiambatana na majeraha yaliopo kichwani na sehemu ya mabega ndiyo yalipelekea msanii huyo kupoteza maisha papo hapo.
 Hata hivyo jeshi la polisi lilikuja masaa mawili baada ya kutokea ajali hiyo,ambapo gari la Tanesco ndilo lililotumika kuvuta gari hiyo hadi kituo cha polisi wilayani humo.
habari zaidi endelea kuchungulia hapahapa .
Mwili wa Sharo utazikwa kesho saa saba mchana .

MSANII JOHN MAGANGA AZIKWA LEO JIJINI DAR

  Wasanii wa Bongo Movie wakibeba jeneza lenye mwili wa msanii mwenzao, John Maganga, wakati wa kuaga mwili huo, Mwananyamala, Dar es Salaam
 Katibu wa  Itikadi na Uenezi CCM na Mjumbe wa NEC, Nape Nnauye akitoa salam za Chama, kwenye msiba wa msanii, Joseph Maganga, Mwananyamala, Dar es salaam.

UJUMBE MZITO WA SHARO MILIONEA WANASWA AKICHATI NA LINEX NI KAMA AMEROGWA HIVI

Huu ni ujumbe kutoka kwa marehemu baada ya ku chart na msanii wa Bongo Fleva hapa Tz almaarufu kama Linex Sunday
Ujumbee ulikuwa kama antabiri kuwepo kwa zengwe katika safari yake ni kama kifo kilikuwa kinamuita vile...ohh mamamaah R.I.P Shaloo.

GARI NA MAHALI ALIPOKATIA ROHO SHARO MILIONEA

Hii ndiyo gari aina Toyota Harrier yenye namba T278 BVR ilipinduka na kusababisha ajali iliyopelekea kifo cha msanii Sharo milionea jana usiku mishale ya saa mbili.
Taarifa zaidi endelea kuchungulia blogu hii.

MWILI WA MAREHEMU SHARO MILIONEA ULIVYOHARIBIKA

 Mwili wa marehemu Sharo Milionea umeharibika vibaya kama unavyoonekana pichani hapao juu pichani ni wazi ilikuwa ajali mbaya.
 Blog ya burudani Unique Entertainment inatoa salamu za maombolezo ya msanii nguli wa vichekesho Sharo milionea kwa kupoteza maisha kutokana na ajali ya gari iliyokea mkoani Tanga.

TAARIFA KAMILI KUHUSU KIFO CHA SHARO MILLIONEA .
 Taarifa kuhusu kifo cha Msanii wa maigizo na Mziki wa Bongo fleva kufariki zimasamba nchi nzima masaa machache yaliopita.
 Kwa mujibu wa chanzo cha habari ni kwamba amepata uthibitisho kutoka kwa diwani Makame Seif ambaye ni rafiki yake wa karibu sana wa Marehemu Hussen Ramadhani Mkiete maarufu kama Sharo Millionea amepata ajali mida ya saa mbili eneo la maguzoni Tanga na amefariki dunia papo hapo. 


Polisi wametambua ni Sharo Millionea kwa vitambulisho vyake na picha moja ya passport aliokuwa nayo mfukoni ambavyo kwa sasa viko na polisi.
 Diwani huyu amemfahamisha mwandishi kuwa Sharo Millionea ameumia vibaya sana kichwani, kifuani na kwenye mikono.

 Pia Mjomba wa marehemu amethibitisha kuwa Sharo Millionea atazikwa Tanga na asubuhi ya leo ratiba ya msiba itatolewa. 
 Ndugu na marafiki wa Sharo wameanza kwenda hospitalini baada tu ya taarifa hizi kuwafikia. Familia ya Sharo imeshafika Hospitali ya Teule ya Tanga.

Monday, November 26, 2012

UNIQUE MODEL 2012 NDO HABARI YA MJINI


WASHIRIKI WA UNIQUE MODEL 2012 KATIKA RED CARPET YA KHANGA ZA KALE

Ze heavy weight models in town "unique models" wakiwa katika pozi red carpet ambapo unique model ilidhamini onyesho hilo@serena hotel.
Jane unique.
 Uniquez.
 Liz unique.
Caty unique.
 Amina unique.
 Zeanath unique.
 Bether unique.
 Secy unique.
 Namshukuru sana mwenyezi mungu kunipa timu kama hii najiskia furaha sana kutoa vipaji vya ukweli,tumaini lamgu ni kukuza vipaji vya mabinti hawa katika tasnia ya mitindo nchini Tanzania ila bado naitaji sapoti kubwa toka kwenu watanzania.
 My dream team 2012.