Pages

BRAND NEW MUSIC

metty magese

metty magese

Listen & Download

http://mdundo.com/a/32626

Wednesday, November 14, 2012

HAPATOSHI USAILI WA UNIQUE MODEL 2012@ LAMADA HOTEL JUMAPILI NOV 18

 
 Tunategemea kupokea wanamitindo wengi sana katika usaili wa kusaka wanamitindo kumi wa kike ambao watapata tiketi ya kushiriki shindano bora la wanamitindo nchini Tanzania liitwalo UNIQUE MODEL 2012.
 Wito umetolewa kwa binti yoyote ambae anahisi kuwa ana kipaji cha uanamitindo na alikuwa hana mahali pa kukuzia kipaji chake,hii ni fulsa pekee kwako kujitokeza kwani kupata tiketi ya kushiriki shindano hili utakuwa umetoka kinachofata ni bidii yako mwenyewe kukiendeleza kipaji chako ambapo utapewa sapoti yakutosha na kipaji chako kitaonekana kwa wadau wa tasnia ya mitindo.
 Huu utakuwa ni mwanzo wa wewe mwanamitindo kupasua anga katika tasnia hii ambapo kama utafanikiwa kuingia Top ten utakuwa umebahatika sana kwakua hakuna shindano bora la wanamitindo lenye hadhi na mtoko kama Unique model kwa sasa nchini Tanzania.
 Usaili utafanyika jumapili hii ya tarehe 18 mwezi huu katika hoteli ya Lamada iliyopo msimbazi center Ilala kuanzia saa nne asubuhi mwisho wa kufanya usaili ni saa saba mchana.

                        VIGEZO VYA KUSHIRIKI UNIQUE MODEL
·         Urefu usiopungua futi 5.8 na kuendelea.
·         Sura na  Umbo lenye mvuto wa kiuanamitindo.
·         Mvuto katika picha.
·         Uraia wa nchi yoyote.
·         Rangi ya ngozi na iwe asilia.
·         Umri wa miaka 18-25.
·         Tabia njema na muonekano wa heshima.
·         Uchangamfu,Uwezo wa kutambua mambo mbalimbali na kujieleza.

       VIGEZO VYA KUMPATA MSHINDI
              Jumla ya alama ni 100 na zimegawanyika kama ifuatavyo;-
·         sura na umbo lenye mvuto wa mwanamitindo. (Alama 30).
·         Uwezo wa ziada wa kutembea miondoko ya kimaonyesho ya nguo.(Alama 30).
·         Uwezo wa kutambua mambo mbalimbali na kujieleza (Alama 20).
·         Kujiamini na uchangamfu jukwaani.(Alama 10)
·         Nidhamu. (Alama 10).
 
....EWE MWANAMITINDO .JITOKEZE UKUZE KIPAJI..!
Shindano hili limedhaminiwa na :-
       Giraffe ocean view hotel,Dtv,Gazeti la Tanzania Daima,mashujaa Investment ltd,
Sophernner Investment co,Fabak fashions,ltd,K.d.surelia,young don records,Kiu investment ltd,Michuzi blog,Oriental bureau de change,,J’s professional ltd,Lamada apartments hotel,Jiachie blog,Mtaa kwa Mtaa blog na Unique entertainment blog.

No comments: