Pages

BRAND NEW MUSIC

metty magese

metty magese

Listen & Download

http://mdundo.com/a/32626

Sunday, June 30, 2013

LUCY CHARLES NDIYE MISS LAKE ZONE 2013


Mrembo Lucy Charles akitabasamu baada ya kuvikwa taji la Redd's miss Kanda ya Ziwa usiku wa jana.
Kinyanganyiro cha kumtafuta mnyange wa Kanda ya Ziwa kwa mwaka 2013, kimeteguliwa usiku huu kwenye Ukumbi wa Hoteli ya Gold Crest baada ya Mrembo Lucy Charles msomi wa chuo kikuu cha mtakatifu Augustino, kuwabwaga warembo wengine 17 waliojitokeza.
Vinara watatu .katikati ni Lucy Charles mshindi wa Redd's miss Lake zone 2013, kulia ni Eshe Rashid kutoka Mara na kushoto ni Salsha Isdore kutoka Geita na wote watatu wanaenda ngazi ya taifa.
Mkurugenzi wa kamati ya Miss Tanzania, Hashim Lundenga
Show ya ufunguzi kwa warembo ikaanza
Warembo wakionesha vipaji vyao
Furaha ikitanda kwa kila mmoja
eee..na yule yumo...!!!
Kila mrembo akiesha uchezi wake hapa na makeke zaidi ..kiufundi kujitengenezea nafasi ya kushinda taji
Furaha zikapenya kwa Viongozi hawa ambao ndiyo walikuwa majaji
Mashidonge- akicheza na Moto kwenye ukumbi huu wa Gold Grest Hotel
...
Miss Talent naye akuwa Nyuma Babylove Kalalaa akaanza kuonesha vitu vyake ...kipanji toka moyoni.Babylove Kalalaa akiwa na nyoka wake jukwaani kuwapagawisha mashabiki wake.
Naibu Waziri wa Sayansi na Teknolojia, Januari Yussuf Makamba ilibidi asimame maana ilikuwa kazi kweli kweli na kwa mara ya kwanza namuona na yeye anachukua kumbukumbu kwenye simu yake.!!
matukio ..tunachukua na sisi...
Babylove Kalalaa akijikusanyia makato!!
warembo wote wakaitwa !!
Kiongozi wa BHATT ELECTONICS LTD Akiteta baada ya kuchagua warembo na kuwapatia kazi kwenye ofisi zao. Kumbuka BHATT ni wakala wa Samsung.
Mkurugenzi wa kamati ya Miss Tanzania, Hashim Lundenga akijiandaa kuanza kuita 10 Bora hapa
Top Ten hii hapa.
Ommy Dimpoz akishambulia jukwaa
Dadaz wakidata na nyimbo za mkali Ommy Dimpoz
P...Omama yoyo!!
wewe tu ...nipe tano kwanza!!
kamata kitita chako Mrembo!!!
ushindi  mtamu jamaniiii!
Wanyange !!

MISS INTER UNIVERSITY KURINDIMA JIJINI DAR


Washiriki wa Mashindano ya Miss Inter University Dar es Salaam, wakiwa katika mazoezi ya katika Ukumbi wa Sansiro Dar es Salaam jana kujiwinda na Onyesho litakalofanyika kesho (Leo) katika Ukumbi huo wa Sansiro, washindi wataungana na washindi wa kanda zingine kuunda kikosi cha Tanzania katika mashindano ya Vyuo Vikuu Tanzania
(Tanzania ambassador of Democracy 2013).
 
Washiriki wa Mashindano ya Miss Inter University Dar es Salaam, wakiwa katika Pozi  wakati wa mazoezi katika Ukumbi wa Sansiro Dar es Salaam leo kujiwinda na Onyesho litakalofanyika june 29 katika Ukumbi huo wa Sansiro, washindi wataungana na washindi wa kanda zingine kuunda kikosi cha Tanzania katika mashindano ya Vyuo Vikuu Tanzania (Tanzania ambassador of Democracy 2013).

LINA ALLAN ANYAKUWA MISS KANDA YA NYANDA ZA JUU KUSINI 
  MSHINDI WA MISS REDD'S TANZANIA KANDA ZA NYANDA ZA JUU KUSINI LINA ALLAN AKIWA NA WASHINDI WENGINE AMBAO WALISHINDA TANO BORA
 MSHINDI WA MISS REDD'S TANZANIA KANDA ZA NYANDA ZA JUU KUSINI LINA ALLAN AKIVISHWA TAJI LA USHINDI NA MSHINDI AMBAYE ALIKUWA ANASHIKILIA TAJI HILO NAOMI JONES

 
 WASHIRIKI WA MISS REDD'S TANZANIA KANDA ZA NYANDA ZA JUU KUSINI WAKIWA WANAONESHA VIPAJI
 BWANA HIDAN ERICCO AKITANGAZA WASHINDI WALIOINGIA KATIKA TANO BORA
 WASHINDI WALIOFANIKIWA KUINGIA KATIKA TANO BORA

WAFARIKI BAADA YA KUANGUKA WAKIFANYA MAPENZI

Wapenzi wameanguka na kufa baada ya dirisha walipokuwa wakifanyia mapenzi kufunguka ghafla nchini China.

Wawili hao wanasemekana kudondoka kutoka kwenye dirisha la jengo moja la makazi kwenye jiji la Wuhan nchini humo pale dirisha hilo walilokuwa wameegemea kufunguka.


Mashuhuda walivieleza vyombo vya habari vya China kwamba wapenzi hao walikumbatiana wakati wakianguka kwenye njia ya waenda kwa miguu nje.


Kwa mujibu wa The Sun, chanzo kimoja cha habari kilisema: "Huku wawili hao wakiwa wameshikamana vilivyo, walianguka nje ya jengo hilo."


Picha za kuogofya zimefichuliwa kwenye tovuti za nchini humo zikionesha wapenzi hao wakiwa wamefunikwa kwa mashuka na polisi.


Damu ilitapakaa kwenye njia ya waenda kwa miguu karibu na wapelelezi wanaonekana wakichunguza eneo la tukio.Miili ya wapenzi hao ilipigwa picha karibu na baiskeli ambayo ilikuwa imelazwa chini, lakini hakukuwa na ripoti zozote kwamba yeyote chini alikuwa amejeruhiwa katika ajali hiyo.


Ripoti zinasema kwamba madirisha hayo kwenye jengo hilo la makazi yalikuwa hayana ubora unaotakiwa.


Inafikiriwa kwamba mwanaume huyo na mwanamke wanawezekana walikuwa wakijaribu kujipooza kando ya dirisha hilo ndipo tukio hilo likatokea.


Haikufahamika ni umbali gani kutoka juu wawili hao walikuwa wakati wakianguka.
 

Wuhan ni jiji maarufu zaidi lililopo katikati ya China.
Ukiwa na historia ya miaka 3,500 ni moja kati ya miji mikongwe na iliyostaarabika katika China.

Saturday, June 29, 2013

WASAUZI WALIVYOANDAMANA KUPINGA UJIO WA RAIS OBAMA AFRIKA KUSINI

  Waandamanaji Nchini Afrika Kusini wakiwa wamebeba mabango yanayopinga kuja Kwa Raisi Obama nchini Humo wakati wa maandamano ya Amani ya Kupinga Kuja Kwa Obama Katika Jiji la Pretoria Nchini Afrika  jana Jioni - Juni 28

 Waandamanaji Nchini Afrika Kusini Wakisali mbele ya Bango linalopinga Kuja kwa Raisi Obama Nchini Humo wakati Raisi Obama alipotua Nchini Afrika Kusini Jioni ya jana  Juni 28

 Waandamaji wa Nchini Afrika Kusini wakiwa wanasali mbele ya Ubalozi wa Marekani wakati wa maandamano ya kupinga kuja kwa Raisi Obama Nchini Humo jana  wakati Raisi Obama alipotua Nchini Humo Kwa Ziara ya Siku 2 ..

Mmoja wa waandamaji nchini Afrika Kusini ambaye jina lake halikuweza kupatikana mara moja akiwa amebeba moja ya Bango ambalo Linamwita Raisi OBAMA kuwa ni Mpishi wa Ikulu ya Marekani kama linavyosomekana na kuendelea kuelezea kuwa sera za Marekani ni tatizo.Mwandamaji huyu alibeba bango hilo jana  Juni 28 wakati wa maandamo ya amani kuelekea mbele ya Ubalozi wa Marekani NChini humo kwa kupinga Kuja Kwa OBAMA Nchini Mwao

USIKU WA UJANA NA LEO JULAI 6

MISS LAKE ZONE 3013 KUPAMBA MOTO USIKU WA JUNE 29

http://1.bp.blogspot.com/-giLjbWAmTeg/Uc7KJYhuO1I/AAAAAAAAqNU/L_OfrA1x_AE/s1600/Miss+Lake+Zone+2013+Poster.jpg

Friday, June 28, 2013

BLING BLING KUMFIKISHA KORTINI RICK ROSS


Rick Ross has just been sued for being so sophisticated ... he forgot to pay a nearly $90,000 bill for three Rolexes he bought last year -- this according to a new lawsuit.

Johnny's Custom Jewelry in Texas filed the suit against Ross and his company Maybach Music, claiming the rapper agreed to purchase 3 diamond Rolexes last August for a total of $89,847.50.

According to Johnny's, the Rolexes include one 18K gold watch with 30CT of diamonds ($55,000), one 18K gold watch with 7CT of diamonds ($14,000), and one two-tone watch with 5CT of diamonds ($14,000).

0627-rick-ross-reciept-wm-2

Johnny's says it held up its end of the bargain -- delivering the watches as ordered -- but Rick still hasn't paid for the bling. Johnny's wants the rapper to cough up the owed money stat, plus interest.


MISS TEMEKE KUMEKUJA NI JUNE 5 TTC CLUB

Warembo wanao wania Taji la Redd's Miss Temeke 2013, kutoka kushoto walio simama Margreth Olotu, Narietha Boniface, Latifa Mohamed, Mutesa George, Naima Ramadhan, Margreth Gerald, Mey Karume, Esther Muswa, Aksaritha Vedustus na Svtlona Nyameyo CHINI, Irenej Rajab, Darlin Mmary, Stella Mngazija na Hyness Oscar. Wakipiga picha ya pamoja baada ya mazoezi yao jijini Dar es Salaam jana.
Na Mroki

WEMA SEPETU ASHITAKIWA KWA KUCHAFUA MAZINGIRA KIJJITINYAMA


MKURUGENZI wa Kampuni ya Filamu ya Endless Fame, Wema Sepetu hivi karibuni amejikuta kwenye wakati mgumu baada ya majirani zake kumshitaki kwenye serikali ya mtaa kufuatia tabia ya wafanyakazi wake kutiririsha maji machafu mtaani.  Taarifa iliyomfikia mwandishi wa habari hii inadai kuwa, majirani wa Wema katika eneo analoishi, Kijitonyama jijini Dar wamekuwa wakimlalamikia msanii huyo kwa kitendo hicho lakini imeonekana uvumilivu umewashinda.
“Mara kwa mara wafanyakazi wake wamekuwa wakitiririsha maji hapa mtaani sasa leo tumeona tukamshitaki serikali za mitaa ili sheria ichukue mkondo wake,” alisema mmoja wa majirani wa staa huyo aliyeomba jina lake lisiandikwe gazetini.
Juni 26, mwaka huu Ijumaa lilifika kwenye nyumbani kwa Wema na kushuhudia maji yakitoka kisha kuzagaa mtaani na muda mfupi baadaye alifika Afisa Mtendaji wa Kata ya Makumbusho (jina halikufahamika mara moja) ambaye aligonga kwenye nyumba ya Wema, baada ya muda alitoka binti wa kazi aitwaye Bite.
Katika mazungumzo yao, Bite alionekana kujitetea lakini baadaye ilibainika wana makosa na akatakiwa kwenda ofisi za kata kwa maelezo zaidi.
Amri hiyo ilionekana kuwa ngumu kwa Bite na wafanyakazi wenzake ambapo busara zilitumika na kiongozi huyo wa serikali akataka walipe faini na kuwaonya waache tabia hiyo.
Kufuatia hatua hiyo, Bite aliingia ndani (inadaiwa alikwenda kumtonya Wema) ndipo alipotoka akiwa na fedha ambazo Ijumaa halikujua ni kiasi gani, wakasainishana (angalia picha ukurasa wa pili)kisha mchezo ukaishia hapo.
Jitihada za kumpata Wema kuzungumzia sakata hilo ziligonga  mwamba kutokana na msanii huyo kutopokea simu na hata mwandishi alipofika nyumbani kwake aliambiwa hayupo.

BINTI AJIFUNGULIA NJIANI UCHUNGU WAMPATA AKIWA AMEPANDA BODABODA

Josephine Michael akiwa barabarani baada ya kujifungua.
Tukio hilo lililowashtua watu wengi lilitokea asubuhi kwenye Kituo cha Daladala Cha Nanenane kandokando ya Barabara Kuu iendayo Dar es Salaam.
Mwandishi wetu alifika eneo la tukio na kumshuhudia askari wa kike wa kikosi cha usalama barabarani ‘trafiki’ (jina lake halikupatikana) akiacha kazi ya kuongoza magari na kugeuka mkunga kwa muda ili kumsaidia binti huyo akiwa sambamba na wanawake wengine na kufanikisha kupatikana kwa mtoto wa kiume ‘dume la nguvu’.
Mmoja wa akina mama waliofika eneo hilo akiwa amembeba mtoto wakati mama yake akihojiwa na mwanahabari.
Awali, wanawake hao walizungusha kanga ili kuweza kuweka usiri wakati wa kumsaidia mwanamke mwenzao alipokuwa akijifungua.
Mara baada ya zoezi hilo kwenda salama, Josephine alisema alipatwa na uchungu alfajiri ya siku hiyo na mume wake aliwapigia simu madereva wa teksi zaidi ya wawili ambao waligoma kufika kijijini kwao kutokana na ubovu wa barabara.

Kulia ni trafiki aliyemsaidi Josephine kujifungua na kushoto mtoto aliyezaliwa akiwa amebebwa.
“Hali ilipozidi kuwa mbaya tuliwasiliana na dereva wa bodaboda ambaye alifika na kunibeba huku mume wangu akitufuatilia nyuma kwa baiskeli yake,” alisema Josephine kwa uchangamfu.
Binti huyo alisema kwamba walipofika eneo la Nanenane hali ilizidi kuwa mbaya akashindwa kujizuia baada ya mtoto kushuka chini, hivyo akamuomba dereva wa bodaboda asimame ndipo alipoanguka chini na hali kuzidi kuwa mbaya.

Wananchi waliofika eneo hilo wakiwa na Josephine (aliyekaa chini).
Baada ya kuliona tukio hilo, trafiki na wanawake wengine waliokuwa jirani wakajitolea kumsaidia hadi alipojifungua salama.
Dereva wa bodaboda aliyembeba Josephine anayejulikana kwa jina la Gitogo Shilagi alikiri barabara iendayo Kijiji cha Kiegea kuwa mbovu.
Hivi ndivyo hali ilivyokuwa baada ya Josephine kujifungua salama mtoto wa kiume.