Pages

BRAND NEW MUSIC

metty magese

metty magese

Listen & Download

http://mdundo.com/a/32626

Wednesday, June 12, 2013

MTOTO WA MANGWEA AKATALIWA NA FAMILIA YA MANGWEA

Mtoto wa Ngwea akiwa na baadhi ya wanafamilia wakati wa mazishi ya baba yake.
Siku chache baada ya aliyekuwa mkali wa Hip Hop Bongo, Albert Kenneth Mangweha ‘Ngwea’ kupumzishwa kaburini kufuatia kifo cha usingizini nchini Afrika Kusini kilichotokea Mei 28, mwaka huu, mambo kibao yanazidi kuibuka
Habari zinadai kuwa familia ya marehemu Ngwea imemkataa mtoto aliyeletwa na mama yake makaburini akidaiwa kuwa ni mtoto wa Ngwea.

Juni 6, mwaka huu wakati wa mazishi, mwanamke aliyejitambulisha kwa jina la Paulina Jeremiah, mkazi wa Kigamboni, Dodoma alitimba akiwa na mtoto huyo wa kike aitwaye Neema Albert na kudai kuwa alimzaa na Ngwea mwaka 2001, wakati msanii huyo akisoma Sekondari ya Mazengo.


Wakati akijieleza, ndugu wa Ngwea, Anthony Mangweha alikuwa akimsikiliza ambapo aliwataja wanandugu wa marehemu waliokuwa wakijua suala hilo.


Waliotajwa kujua kuwa mtoto huyo alikuwa wa Ngwea ni Frank, Jotam na Amani ambao waliwahi kutumwa na marehemu kwenda kumwangalia mkoani Dodoma.

Hata hivyo, ndugu huyo aliyekuwa akimsikiliza alimtaka mama Neema kupoa, hadi familia ikae kikao.


Mama Mangwea.
“Kweli wikiendi iliyopita familia ilikaa kikao kwa zaidi ya saa 7, pamoja na mambo mengine lakini wanadaiwa kufikia uamuzi mzito wa kumkataa mtoto huyo hadi mama Neema apeleke vigezo vya uthibitisho,” kilisema chanzo chetu ndani ya kikao hicho.
Akizungumzia suala hilo kwa sharti la kutotajwa , mmoja wa dada zake Ngwea alisema: “Ni kweli yule mtoto aliondoka na mama yake lakini kama akileta uthibitisho tutampokea.”

No comments: