Pages

BRAND NEW MUSIC

metty magese

metty magese

Listen & Download

http://mdundo.com/a/32626

Wednesday, October 31, 2012

SHINDANO LA UNIQUE MODEL LAZINDULIWA KWA KISHINDO HOLIDAY INN JIJINI DAR ES SALAAM

Mkurugenzi wa shindano hayo, Methuselah Magese akizungumza mbele ya waandishi wa habari (hawapo pichani).

SHINDANO la kusaka wanamitindo wenye vegezo vya kipekee nchini, linaloratibiwa na kampuni ya Unique Entertainment, leo limezinduliwa rasmi katika hoteli ya Holiday Inn Posta jijini Dar es Salaam.

Magese (katikati) akiwa pamoja na bodi yake ya uandaaji…

 Shindano la kumsaka mwanamitindo mwenye vigezo vya kipekee nchini Tanzania(unique model) linaloandaliwa na Unique Entertainment limezinduliwa leo jumatano kwa kishindo katika hoteli ya Holiday Inn iliyopo katika ya jiji la Dar es salaam mbele ya waandishi wa habari.

Akizungumza na waandishi wa habari hao katika ufunguzi huo mkurugenzi wa shindano hilo Bw.Methuselah Magese amesema kuwa mchakato wa shindano umefunguliwa rasmi ili kutoa fursa ya wadhamini kujitokeza kwa wingi kudhamini shindano hilo ambalo litakuwa na mvuto wa aina yake kwa msimu huu wa pili.

Pia wanamitindo wenye sifa za kimataifa wameombwa kujitokeza kwa wingi katika usaili utakaofanyika tarehe 18 novemba katika hoteli ya Lamada Apartments.

 Tumeboresha shindano kwa kiwango cha hali ya juu tofauti na ilivyokuwa hapo awali,lengo ni kulifanya shndano hili liwe la heshima,hadhi na linalotimiza lengo lake la kuvumbua na kuinua vipaji vya wanamitindo wa kchipikizi.

“Tunaomba wabunifu wadogo kwa wakubwa wajitokeze kuja kuonyesha umahili wao katika shindano hili ambapo mwaka huu tutakutanisha wabunifu wengi wa mavazi nchini Tanzania katika shindano moja kwa lengo la kuwainua wabunifu wadogo na kuendelea kuwatangaza wabunifu wenye majina makubwa katika tasnia ya mitindo hasa katika kipindi hiki maridhawa cha mwisho wa mwaka” alisisitiza Magese.

Katika msimu huu wa pili wa unique model kutakuwa na nyongeza ya mataji mengine madogo matatu amabayo ni “model photogenic 2012”,”model talent 2012” na “model with good manner 2012” ambapo mataji hayo yatakuwa chini ya taji kuu la “Unique model of a year 2012”.

Fainali za shindano la Unique model 2012 zitafanyika mwishoni mwa mwezi Desemba ambapo kamati ya maandalizi imedhamilia kufanya onyesho lenye hadhi kuanzia ubora wa washiriki wenye vigezo vya uanamitindo ambao wataleta mabadiliko katika tasnia ya mitindo nchini.

Shindano la Unique model lilianzishwa mwaka 2010 ambapo kwa mwaka huu ni mara ya pili kufanyika,Asia Dachi ndiye mwanamitindo anaeshikilia taji hilo mpaka sasa.

Wito umetolewa kwa makampuni kujitokeza kuchukua mabalozi ambao ni wanamitindo washiriki kwa lengo la kufanya nao kazi za kutangaza bidhaa ama huduma inayotolewa na kampuni husika kwa lengo la kutoa ajira kwa wanamitindo hao wanaochipukia katika tasnia.

Unique model 2012 imedhaminiwa na Dtv,Gazeti la Tanzania Daima,Mashujaa investment ltd,Sophernner Investment co ltd,K.d.surelia,young don records,Kiu investment ltd,Oriental bureau de change,J’s professional ltd,Lamada apartments hotel, na Unique entertainment blog.

Monday, October 29, 2012

GIRAFFE OCEAN VIEW HOTEL PALIVYOWAKA MOTO LAST FRIDAY

 Siku ya ijumaa ilivyojili pale Giraffe ocean view hotel ambapo mamiss walichuana si mchezo..! 
Picha zote kwa hisani ya Magese unique.MWITA NA NAALI WANG;ARA MBIO ZA ROCK CITY MARATHON 2012

 Mwanariatha Mary Naaly kutoka Arusha akishangilia baada ya kumaliza mbio za kilometa 21 na kuibuka mshindi kwa upande wa wanawake katika mashindano yanayojulikana kama ‘Rock City Marathon 2012’ yaliyofanyika Jijini Mwanza jana Jumapili. Naaly alizawadiwa shilingi 1,200,000/= ya ushindi baada ya kutumia saa 1:16:33 kumaliza mbio hizo na kuwashinda wenzake zaidi ya 497 walijitokeza kushiriki mashindano hayo. 
 Mwanariatha Copro Mwita kutoka Mwanza akishangilia baada ya kumaliza mbio za kilometa 21 na kuibuka mshindi kwa upande wa wanawake katika mashindano yanayojulikana kama ‘Rock City Marathon 2012’ yaliyofanyika Jijini Mwanza jana Jumapili. Mwita alizawadiwa shilingi 1,200,000/= ya ushindi baada ya kutumia saa 1:04:02 kumaliza mbio hizo na kuwashinda wenzake zaidi ya 375 walijitokeza kushiriki mashindano hayo. 
 Wanariadha walioshiriki mbio za Rock City Marathon 2012 kilometa 21, wakichuana vikali kutafuta shilingi 1,200,000/= ambayo waandaaji wa mbiyo hizo, Capital Plus International Ltd (CIP), walitenga kwa mshindi wa mwaka huu. Mashindano hayo yalifanyika Mwanza.
 Wanariadha walioshiriki mbio za Rock City Marathon 2012 kilometa 21, wakichuana vikali kutafuta shilingi 1,200,000/= ambayo waandaaji wa mbiyo hizo, Capital Plus International Ltd (CIP), walitenga kwa mshindi wa mwaka huu. Mashindano hayo yalifanyika Mwanza.
 Wanariadha walioshiriki mbio za Rock City Marathon 2012 kilometa 21, wakichuana vikali kutafuta shilingi 1,200,000/= ambayo waandaaji wa mbiyo hizo, Capital Plus International Ltd (CIP), walitenga kwa mshindi wa mwaka huu. Mashindano hayo yalifanyika Mwanza
MWANARIADHA  mahiri Copiro Mwita wa Mwanza na Mary Naaly wa Arusha, jana waliibuka vinara upande wa wanaume na wanawake, katika mashindano ya riadha ya kilometa 21 ya ‘Rock City Marathon 2012’ yaliyofanyika leo Jijini Mwanza.
Mwita alishinda mbio hizo kwa upande wa wanaume akitumia saa 1:04:02, huku Mary akishinda kwa upande wa wanawake baada ya kutumia saa 1:16:33, katika mashindano hayo yaliyoshirikisha zaidi ya wanariadha 497 waliokimbia katika makundi matano.
Dotto Ikangaa kutoka Arusha aliibuka mshindi katika mbio za kilometa tano wanaume, akimpiku John Joseph kutoka Singida ambaye alishika nafasi ya pili, huku Paul Elias kutota Ukerewe, Mwanza akishika nafasi ya tatu.
Rock City Marathon ni mbio zinazondaliwa na kampuni ya Capital Plus International Ltd tangu mwaka 2009, ambapo kwa mwaka huu zilidhaminiwa na NSSF, Airtel Tanzania, Geita Gold Mine, ATCL, PPF, African Barrick Gold, New Africa Hotel, Nyanza Bottles, New Mwanza Hotel, TANAPA na Bodi ya Utalii Tanzania (TTB).
Katika mbio hizo, washiriki na mashabiki wake waliburudishwa na msanii maarufu wa Tanzania Juma Kassim ‘Sir Nature’ na kundi lake la TMK Wanaume, akishirikiana na Baby Madaha katika kuuzindua wimbo wao mpya ‘Narudi Nyumbani’ ambao waliimba kwa mara ya kwanza Mwanza.          

FLAVIAN MATATA KATIKA MERCEDES BENZ FASHION WEEK AFRICA NDANI YA J'BERG


Saturday, October 27, 2012

BABYLOVE KALALA AWA MISS TALENT 2012


Mshindi wa Redd's Miss Talent 2012,Babylove Kalala (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na warembo wengine walioingia hatua ya tano bora ya Redd's Talent iliyofanyika usiku huu katika hoteli ya Gireffe,jijini Dar es salaam.Kutoka kulia ni Mshiriki namba 13 kutoka kanda ya Mashariki,Joyce Baluhi,Mshiriki namba 15 kutoka Temeke,Catherine Masumbigana,Mshiriki kutoka Kanda ya Mashariki,Irene Verda na Mshiriki namba 26 kutoka Kinondoni,Brigit Alfred.
 Mgeni Rasmi katika Onyesho la Redd's Miss Talent,Mbunge wa Viti Maalum - Arusha,Mh. Catherine Magige (katikati) akizungumza machache wakati akifungua shoo hiyo iliyofanyika hivi sasa katika Hoteli ya Giraffe,Mbezi Beach jijini Dar es Salaam.Kushoto ni Mkurugenzi wa Rino International Agency ambao ni waandaaji wa Mashindano ya Miss Tanzania,Hashim Lundenga na Kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa Hoteli ya Giraffe,Dk. Charles Bekon.
 Mshiriki namba 30,Waridi Frank akionyesha umahiri wake wa kucheza ngoma za asili.
 Mshindi wa Redd's Miss Talent 2012,Babylove Kalala akionyesha umahiri wake wa kucheza ngoma za asili kwa kutimia Nyoka.
 Mshiriki namba 11 kutoka Kilimanjaro,Nandi Rafael akionyesha umahiri wake wa kusakata dansi.
 Mshiriki namba 29,kutoka Dodoma,Belinda Mbogo nae akisakata Dansi.
 Mshiriki namba 3 kutoka Chuo Kikuu Huria,Zuwena Naseeb akionyesha umahiri wake wa kuimba katika onyesho la kumpata mrembo mwenye kipaji lililofanyika katika Hoteli ya Giraffe,Mbezi Beach Jijini Dar es Salaam usiku huu.
 Mshiriki namba 13kutoka kanda ya Mashariki,Joyce Baluhi akionyesha uwezo wake wa kusakata dansi.
 Mshiriki namba 27 kutoka Ilala,Noela Michael akionyesha kipaji chake cha kuimba.
 Mshiriki namba 8 kutoka Kanda ya Ziwa,Happyness Rweyemamu akionyesha kipaji chake cha kuruka sarakasi katika onyesho la kumpata mrembo mwenye kipaji lililofanyika katika Hoteli ya Giraffe,Mbezi Beach Jijini Dar es Salaam usiku huu.
 Mshiriki namba 15 kutoka Temeke,Catherine Masumbigana akionyesha kipaji chake cha kupiga Zeze.
Mshiriki namba 7 kutoka Rukwa,Vency Edward akionyesha kipaji alichonacho cha kucheza.

Thursday, October 25, 2012

BATA BATANI NA VIPAJI VYA WALIMBWENDE@GIRAFFE OCEAN VIEW HOTEL 26 OCT 2012

WWW.UNIQUEENTERTZ.BLOGSPOT.COMPhoto: WWW.UNIQUEENTERTZ.BLOGSPOT.COMwww.uniqueentertz.blogspot.comwww.uniqueentertz.blogspot.com
Mdau Shah na mdau Mwita Mkama wakiwa na warembo walito wa Miss Tanzania, 2012,hili ni joto la vipaji vya warembo hao amabpo mtanange huo utafanyika palepale Giraffe ocean view hotel kuanzia saa moja usiku.

SHILOLE NAE AZIANIKA NGUO ZAKE ZA NDANI JUKWAANI


KATIKA kile kilichoonekana kama wasanii wa Bongo Movies wana ‘aleji’ na kujisitiri miili yao, baada ya Wema Sepetu na Aunt Ezekiel, safari hii Zuwena Mohamed ‘Shilole’ ameanika sehemu zake za siri kweupe.

Mpaka sasa tuna picha zinazomwonesha Shilole ambaye kwa sasa amegeukia muziki wa mduara, akiwa jukwaani huku akionekana hana habari kabisa na kitu kinachoitwa staha achilia mbali heshima.

Chanzo chetu cha habari kwa sharti la kutotajwa jina lake , kilinyetisha kwamba, Shilole amekuwa na kawaida ya kujiachia kihasarahasara hasa anapokuwa kwenye shoo na bendi yake.

Mdau wa filamu Jumanne Athuman, mkazi wa Magomeni jijini Dar es Salaam, alisema amekerwa sana na kitendo cha Shilole kukaa hovyo jukwaani kwani anajidhalilisha mbele ya jamii ambayo itajitizama kupitia kwake.

“Huyu Shilole hana heshima kabisa, juzi tu nilisoma katika mitandao akiwakashfu Wema na Aunt eti ndiyo tatizo Bongo Movies, mbona naye huwa anajiachia hovyo?

“Kwa nini hawa wasanii hawajiheshimu? Inaniuma sana, nahisi kama ndiyo kawaida yao. Ni sikio la kufa…hawasikii dawa. Wamezidi sana, wanajichafulia heshima zao kwenye jamii,” alisema Jumanne.

KUMEKUCHA MISS TANZANIA VIPAJI @GIRAFFE OCEAN VIEW HOTEL 26 OCT 2012


  Karibu ijumaa hii katika hotel yenye hadhi ya nyota nne Giraffe ocean view kutizama vipaji vya walimbwende wanaowania taji la mrembo mwenye kipaji ambapo kiingilio ni 15,000/= na getini itakuwa  20,000/=,kuanzia saa moja usiku na kuendelea ,tiketi za awali zinapatikana Shear Illusion (mlimani city)..USIKOSE..!Photo: WWW.UNIQUEENTERTZ.BLOGSPOT.COM!Photo: WWW.UNIQUEENTERTZ.BLOGSPOT.COM
Photo
PhotoPOA

WWW.UNIQUEENTERTZ.BLOGSPOT.COM