Pages

BRAND NEW MUSIC

metty magese

metty magese

Listen & Download

http://mdundo.com/a/32626

Wednesday, October 17, 2012

MISS TANZANIA MAPANGONI AMBONI


  
Hapa ni katika eneo ambalo linafananishwa na Mlima Kilimanjaro na hapa warembo wakipanda mlima huo ndani ya Mapango ya asya Amboni mkoani Tanga.
 Wakionesho eneo ambalo linafananishwa na daraja kwa jinsi lilivyo umbika.
 Hapa warembo wakipiga picha katika kiti cha enzi. Ni jiwe lililochongeka mithili ya sofa na ukiingia pangoni humo inapendeza kuchukua kumbukumbu.
 Eneo hili ni linafananishwa na Mlango wa kupandia ndege na hapa warembo wakipanda na kutoka nje ya pango.
 Bado pango hilo la Amboni linaendelea kukua. Na hapa warembo wakiangalia moja ya vitu vinavoota kila mwaka hasa wakati wa mvua.
 Hapa huna budi kuinama na huko ndani waweza kuinuka bila kugusa juu.Wanapotokea..
 Warembo wakiangalia moja ya vitu vya kuvutia na hapa waliangalia mchoro wa asili wa chui aliyelala baada ya kushiba.
 Hakika ukifanikiwa kupita hapa  utapita pango zimana kujionea vitu vingi. Hapa lazima utambae na wengi hushindwa kupenya hapa. Hata Father Kidevu nilipenya na  warembo walishangaa niliwezaje kupenya kirahisi.
 Ni full kushangaa kwa warembo hawa wa Redds Miss Tanzania 2012. Hakika ni utalii wa ndani uliofanywa na warembo hawa lakini je ni watanzania wangapi tunatalii katika maeneo ya utalii.

No comments: