Pages

BRAND NEW MUSIC

metty magese

metty magese

Listen & Download

http://mdundo.com/a/32626

Tuesday, June 25, 2013

MISS KANDA YA MASHARIKI 2013 KURINDIMA JUNE 29

aaaaaaa

MASHINDANO ya Redds Miss Kanda ya Mashariki yatafanyika Juni 29 Nashera Hotel mkoani Morogoro kwa kushirikisha jumla ya warembo 14.
Mkurugenzi wa kampuni ya Nikalex Ltd, Alex Nikitas aliwataja warembo hao ambapo wapo kambini hotel ya Starwing Hotel chini ya mkufunzi, Kudra Lupatu kuwa ni Muzne Abduly (19), Ummy Mohamed (21), Sabra Islam (19) na Diana Laizer ambao wote wanatoka Morogoro.
Warembo ambao wanatoka Mtwara kwa mujibu wa Nikitas ni Ivony Stephen (22), Purkeriah Ndovi (21), Zulfa Semboja (19) na wa Lindi ni Janeth Awet (19), Zainab Shaaban (23) na  Sophia Mganga (21). Wanaotoka mkoa wa Pwani ni Elizabeth Perty (22), Suleiyah  Abdi (22)  na Easther Albert (20).
Nikitas alisema kuwa maandalizi ya mashindano hayo yaliyodhaminiwa na Redds Original, Dodoma Wine, CXC Africa, Nyumbani Park, Usambara Safari Lodge, Michuzi Blog, Clouds Media Group, Chilakale Resorts, Nashera Hotel, Starwing Lodge, Simple car Rental, Big Solution na Mikocheni Resort Centre yamekwisha kamilika na warembo watatembelea sehemu mbali mbali mkoa wa Morogoro na kufanya kazi za jamii.
“Tumejiandaa vziuri na warembo kwa sasa wapo kambini wakijifua kwa ajili ya shindano hilo, warembo watatu wataiwakilisha kanda hiyo katika mashindano ya Redds Miss Tanzania ambayo yatafanyika mwezi Septemba,” alisema Nikitas.
Alisema kuwa wamejipanga vilivyo kwa ajili ya mashindano hayo ambayo yanatarajiwa kuwa na ushindani mkali kutoka kwa warembo wote.

No comments: