Zeinul  Mnzige (kulia) akikabidhi zawadi ya vitenge kwa Mratibu mkuu wa  Giraffe Unique Model,Methuselah Magese  ikiwa ni moja ya zawadi zitakazokabidhiwa kwa warembo hao.
UNIQUE  MODEL ni  shindano la kutafuta wanamitndo wenye sifa za kipekee. Kwa  mwaka huu  limepewa jina la Giraffe unique model kutokana na Hoteli ya  Giraffe  Ocean vew ambayo iko katika hadhi ya nyota nne kuwa mdamini mkuu  wa  shindano hili.
Lengo   la kuweka kambi ni kuwakusanya washiriki sehemu moja na kuwapa elimu   kuhusu masuala mbalimbali yahnayo husu mitindo, maadili na namna ya   kuishi na jamii yenye tabia tofautitofauti. Kwa upande wa unique   entertainment lengo lake ni kuinua na kuendeleza vipaji vya sanaa ya   uanamitindo hapa nchini.
Hiki  ni kitu kipya tumekuja nacho kutokana na  utafiti tuliofanya na kugundua  soko la mitindo hapa nchini na hata nje  ya nchi linahitaji wanamitindo  wa aina gani ili kila mtu avutiwe na  tasnia hii ndio maana unique  entertainment tumeamua kutengeneza  wanamitindo mabao watakidhi na  watakua bora katika soko la uanamitndo  kwa hapa nchini.
Shindano   hili litafanyika 24th desemba siku ya ijumaa kuanzia saa mbili usiku   ambapo tutakua pia na burudani kutoka kwa wasnii mbalimbali wa kizazi   kipya na kiingilio kitakua ni tsh. 20,000/= kwa viti vya kawaida na tsh.   30,000/= kwa viti maalum.
Kwa  upande wa udhamini tukimuacha Giraffe  ocean Vew Hotell kama mdhamini  mkuu pia tunao wadhamini kama Robbialack  paints, Mohamed enterprises,  Channel Ten, Global Publishers,  Truworths, Ally Rehemtullah, Galacha  wear mtata kwa mtaa blog na  uniqueentertz blog.
Kwa   kumalizia tu ni kwamba tiketi za tukio zitaanza kupatikana muda wowote   kuanzia leo na tunatarajia zitakua zikipatikana katika vituo mbalimbali   kama vile Truworths (mlimani city), Global publisher (bamaga), Giraffe   Ocean Vew hotel (Africana / kunduchi) na stears (posta).
Kuhusu UNIQUE  ENTERTAINMENT
UNIQUE ENTERTAINMENT ni kampuni iliyesajiliwa  kisheria nchini Tanzania chini ya BASATA kufanya kazi za mitindo na  burudani.
Kwa  mawasiliano zaidi:
e-Mail:  uniqueentertz@yahoo.com
web:  www.uniqueentertz.blogspot .com
Tel: +255 714 796 622, +255 769 378 747
Mratibu  wa shindani wa Giraffe Unique Models  2010
Methuselah Magese
 
 
No comments:
Post a Comment