
Rapper Metty kutoka jijini Dar es salaam ametangaza kachia kibao kipya kinachoenda kwa jina la YOUR LOVE.
Wimbo
 huo wenye mahadhi ya muziki wa kizazi kipya " bongoflava" maudhui 
yalioambatana kuimba na kurap kiasi mtindo unaowavutia mashabiki wengi 
wa muziki huo.
Katika
 wimbo huo Metty amemshirikisha mwanadada Dayna Nyange anaefanya vizuri 
kwenye medani  ya muziki kwa sasa pamoja na muimbaji mwingine 
anaechipukia kwa kasi aitwae Nappy.
Wimbo
 wa YOUR LOVE umetengenezwa na mtayarishaji maarufu nchini Tanzania Mr T
 Touch katika studio za Touchez Sound zilizopo sinza jijini Dar es 
salaam.
Katika
 mahojjiano na mwandishi wa habari hizi Metty amesema wapenzi wa muziki 
wakae mkao wakupkea muziki mzuri wa level ya kimataifa,amejipanga 
vyakutosha na hivi punde ataachia kibao hiko ambacho kitapatikana katika
 vyanzo mbalimbali ikiwemo redio,lunimga na mitandao ya kijamii. 
 
