Mrembo
atakaeiwakilisha Tanzania katika mashindano ya mwaka huu ya urembo ya
Miss East Africa atatangazwa rasmi tarehe 14/10/2012 katika hotel ya
Serena Jijini Dar es salaam.
Jumla ya warembo 148 wameomba kuiwakilisha Tanzania katika mashindano
ya Miss East Africa mwaka huu lakini ni Mrembo mmoja tu atakaechaguliwa
kuiwakilisha Nchi katika mashindano hayo makubwa ya urembo katika ukanda
huu wa Africa na yanayosubiliwa kwa hamu na wapenzi wa fani hiyo ndani
na Nje ya Africa Mashariki
Aidha maandalizi ya mashindano hayo yanaendelea vizuri ambapo
yatafanyika tarehe 07 December, 2012 katika ukumbi wa Mlimani City
Jijini Dar es salaam
Wakati huohuo Nchi ya Burundi imebadili mwakilishi wake ambapo sasa
itawakilishwa na mrembo Ariella Kaneza (23), Mwanafunzi wa mwaka wa pili
wa chuo kikuu cha Universte De Lumiere akichukua Degree ya marketing.
Taarifa kutoka Burundi iliyosainiwa na Mratibu wa Mashindano ya Miss
East Africa Nchini humo, Serge Nkurunziza, zimeeleza kwamba Burundi
imeamua kubadili mwakilishi wake ili kuhakikisha kwamba Nchi hiyo
inashinda Taji hilo kwa mara ya pili tangu mashindano hayo
yalipoanzishwa mwaka 1996 baada ya kugundua kwamba mwakilishi wake wa
awali anapungukiwa baadhi ya sifa chache za kuweza kunyakua taji hilo.
(Burundi imewahi kushinda Taji hilo mara moja mwaka 2008 kupitia kwa
mrembo wake Miss Claudia Niyonzima)
Mashindano ya Miss East Africa mwaka huu yanatarajiwa kuwa na mvuto wa
aina yake na yatashirikisha warembo kutoka Nchi 16 za ukanda wa Afrika
Mashariki.
Nchi
zilizothibitisha kushiriki mashindano hayo ni wenyeji Tanzania, Kenya,
Uganda, Rwanda na Burundi. Nchi zingine zilizoalikwa kushiriki ni pamoja
na Ethiopia, Eritrea, Somalia, Djibouti, Southern Sudan, Malawi, pamoja
na visiwa vya Seychelles, Madagascar, Reunion, Comoros, na Mauritius.
Mashindano
ya Miss East Africa yanalenga kukuza ushirikiano na kutangaza utamaduni
wa Afrika Mashariki, pamoja na kutangaza utalii wa Tanzania kama Nchi
wenyeji wa mashindano hayo makubwa katika ukanda huu wa Afrika.
Mashindano ya Miss East Africa yanamilikiwa na kuandaliwa na kampuni ya Rena Events Ltd ya jijini Dar es salaam,.
No comments:
Post a Comment