Spika wa bunge Anne Makinda
amesema taasisi ya bunge inalaani vurugu zilizojitokeza bungeni february
4 2013 na kusababisha kuahirishwa kwa kikao cha bunge wakati wa mjadala
wa mbunge wa Ubungo John Mnyika (Chadema) kuhusu upatikanaji maji
katika jiji la Dar es salaam.
Baada ya kipindi cha maswali na
majibu february 5 2013 Spika Makinda kasema katika kikao cha dharura
cha kamati ya uongozi kilichofanyika feb 4, kimelaani hizo vurugu na
kuamua kupeleka hiyo ishu kwenye kamati ya haki, kinga na madaraka ya
bunge ili kufanya uchunguzi na kuwasilisha bungeni matokeo ya uchunguzi
huo.
Jingine lililojadiliwa na
kufanyiwa maamuzi ni kamati kusitisha uwasilishwaji wa hoja zote binafsi
za wabunge zilizotakiwa kuwasilishwa katika mkutano huu wa bunge ili
kuepuka vurugu zinazoweza kutokea tena.
Baada ya hayo maelezo wabunge
kadhaa walisimama na kuomba muongozo wa spika akiwemo mbunge wa Arumeru
Mashariki Joshua Nassari aliyehoji kuenguliwa kwa hoja yake, pia mbunge
wa Singida Mashariki Tundu Lissu aliyetaka kujua hatua zilizofikiwa
katika rufaa za wabunge zilizokatwa kupinga maamuzi mbalimbali ya spika.
Namkariri mbunge wa Arumeru
Mashariki Joshua Nassari akisema “sasa kama fujo zinatokea bungeni na
kupelekea hoja yangu kuondolewa, kamati iliyopaswa kukaa kuzungumza ni
kamati ya maadili sio kamati ya uongozi, kamati ya uongozi kimsingi
haina mamlaka ya kuondoa hoja yangu kwenye ratiba ya shughuli za leo, mh
Spika naomba muongozo wako”
Mbunge Tundu Lissu alisema “kwa
taratibu za kanuni za bunge, mbunge ambae haridhiki na uamuzi wa spika
anatakiwa akate rufaa na naomba muongozo wako, rufaa zaidi ya 10 ambazo
zimekatwa dhidi ya maamuzi ya kwako spika na muheshimiwa naibu spika… za
tangu mwaka 1011, za mwaka jana,
No comments:
Post a Comment