(Tunaomba radhi kwa picha hii si nzuri,ila tunaiweka kukemea matendo ya kinyama dhidi ya watoto)
ZIKIWA zimepita siku takriban tano toka kukutwa kwa mwili wa mtoto
mchanga katika eneo la Semtema jirani na makazi ya wanafunzi wa chuo
kimoja cha dini mkoani Iringa, simanzi na majonzi zimeendelea kutanda
katika Manispaa hiyo baada ya mtoto mwingine wa jinsi ya kike kutupwa
katika dampo la taka eneo la Stendi ya M.R mjini Iringa.
Wakizungumzia
matukio hayo ya wanawake wasiofahamika kufanya vitendo hivyo vya
ukatili dhidi ya watoto wanaowazaa, baadhi ya akina mama wamelitaka
jeshi la polisi na jamii nzima kusaidiana kuendesha misako dhidi ya
wanawake wanaofanya vitendo hivyo vya kikatili.
Sarah Sanga, mkazi
wa Miyomboni mjini hapa alisema kuwa matukio ya wanawake kutoa mimba na
kutupa watoto yameendelea na kuwa ni tishio katika Manispaa ya Iringa.
Bwana
Said alishauri wanawake kuwafichua wenzao ambao siku za karibuni
walionekana na mimba na ghafla mimba hizo kutoweka kwani wanaweza kuwa
wahusika lakini akawalaumu wanaume kwamba wanaweza kuwa chanzo cha
tatizo hilo.
Mkuu wa Wilaya ya Iringa, Dk. Leticia Warioba
akizungumzia tukio hilo amewataka mabinti na vijana wilayani hapo
kuepuka kupeana mimba bila kuwa na uhakika wa ndoa.
“Serikali ya
wilaya itaendelea kutoa elimu zaidi kwa vijana ili kupunguza tatizo la
watoto kutupwa katika wilaya ya Iringa,” alisema
Jeshi la Polisi
Mkoa wa Iringa, limethibitisha kutokea kwa matukio hayo na kuahidi
kuendelea na msako mkali ili kuwakamata wahusika.
Mpekuzi.
No comments:
Post a Comment