Pages

BRAND NEW MUSIC

metty magese

metty magese

Listen & Download

http://mdundo.com/a/32626

Wednesday, May 28, 2014

BOTI YAZAMA NA KUUA WATU ZIWA VICTORIA

Watu watano wamekufa maji baada ya boti waliyokuwa wakisafiria kuzama ndani ya Ziwa Victoria.
  Kamanda wa Polisi wa Mkoawa Kagera, George Mayungaalisema ajali hiyo ilitokea Mei 23 mwaka huu saa 8 usiku. Boti 
ya Mv Kitoko II waliyokuwa wakisafiria kutoka Bugombe kupitia Kasenye kwenda Mganza wilayani Chato, ilizimika ghafla ikiwa katikati ya ziwa.Alisema boti hiyo inayomilikiwa na Mama Chacha aishiye Muganza , 
ilikuwa na abiria hao watano,ambao wote walikufa maji. Maiti 
aliyepatikana ni mfanyabiashara raia wa Rwanda, Jane Mlekatete (36) 
ambaye mwili wake ulikutwa ukielea. Wengine waliozama ambao 
hawajapatikana ni Chikola Filbert (22) mkazi wa Muganza, Mapinduzi 
Daud ( 38 )mkazi wa Mwanza, Ashana Suzy waliotambuliwa kwa jina moja 
moja, wote wakazi wa Kasenyi na Mavombe (23) ambaye ni mkazi wa 
Muganza.Alisema chanzo cha ajali hiyo ni boti kubeba mzigo mkubwa. Kwa 
mujibu wa Kamanda, ilikuwa imebeba magunia 210.Chanzo kingine cha 
ajali hiyo ni kwamba licha ya kubeba mzigo mkubwa, ilisafiri usiku 
wakati kukiwa na upepo mkali na mawimbi yaliyosababisha injini ya 
botihiyo kuzimika kabla ya kuzama

No comments: