Pages

BRAND NEW MUSIC

metty magese

metty magese

Listen & Download

http://mdundo.com/a/32626

Tuesday, May 27, 2014

POLISI YAPIGA MARUFUKU NGOMA ZA VIGODORO JIJINI DAR


Jeshi la polisi kanda maalumu ya Dar es salaam limepiga marufuku ngoma za kitamaduni ambazo zimekuwa zikifanyika  nyakati za usiku kwenye maeneo mbalimbali Dar es salaam ikiwa ni muendelezo wa kukabiliana makundi ya kihalifu ambayo yamekua tishio kwa usalama wa raia. 


Kufuatia kuibuka kwa makundi ya kihalifu kama Panya road na Mbwa mwitu ambayo wengi wao wanahusishwa na ngoma hiyo kwenye uporaji na upigaji wa watu, Kamanda wa polisi kanda maalumu ya Dar es salaam Suleiman Kova anasema "Ni marufuku kwa ngoma yeyote ya asili kuchezwa nyakati za usiku"
 
Kamanda Kova anasema kufuatia operesheni inayoendeshwa dhidi ya vikundi hivyo vya kihalifu, mpaka sasa tayari wanawashikilia wafuasi zaidi ya 100  ambapo pia watu wengi wamekuwa wakilalamikia vitendo viovu vinavyofanyika nyakati za usiku wakati wa ngoma hizo maarufu kama ‘vigodoro’ pamoja  na  ‘baikoko'.

No comments: