Pages

BRAND NEW MUSIC

metty magese

metty magese

Listen & Download

http://mdundo.com/a/32626

Friday, September 30, 2011

JINAMIZI LA AJALI LAISAKAMA MKOA WA MBEYA

Hali ni tata kwa upande wa udhibiti ajali mkoani Mbeya.

AJALI sasa ni shetani aliyeukumbatia mkoa wa Mbeya, baada ya siku chache kupita tangu watu 14 wapoteza maisha kwa ajali ya Fuso la mnadani, watu wengine tisa wamekufa na wengine 12 kujeruhiwa katika ajali nyingine. Watu hao wamepoteza maisha katika ajali iliyohusisha basi dogo la abiria aina ya Toyota Hiace namba T 219 ASQ na gari aina ya Prado namba T 155 ACQ yaliyogongana uso kwa uso katika barabara ya Mbeya - Tunduma. Mkuu wa Wilaya ya Mbozi, Gabriel Kimolo amesema leo kuwa, ajali hiyo ilitokea jana saa 1.30 usiku katika Kijiji cha Chimbuya, Mbozi mkoani Mbeya. Kimolo amesema, dereva aliyekuwa akiendesha basi hilo, alishindwa kulimudu kutokana na mwendo wa kasi na kuyumba kutoka upande wake hadi upande wa pili na kugongana na gari hilo lililokuwa likienda Tunduma kutoka Mbeya.


KAPINGAZ DADAZ!! NDANI YA MSASANI BEACH CLUB

Wadada wa KAPINGAZ Blog ndani ya sherehe ya kumpongeza Dada Rehema kwa kufanya maamuzi mazuri ya kuolewa. Sherehe hiyo ilifanyika leo usiku katika ukumbi wa Msasani Beach Club.
Mmependezaa!!


MISS UTALII 2011/2010 KUPAMBWA NA VIONGOZI
Waheshimiwa wabunge wote wa Majimbo ya mkoa wa Dodoma, wakuu wa Wilaya zote na mkuu wa mkoa wa Dodoma, ni miongoni mwa wageni mashuhuri walio alikwa kuhudhuria shindano la kumpata mrembo wa utalii wa mkoa wa Dodoma 22-10-2011. Shindano hilo limepangwa kufanyika katika ukumbi wa hoteli ya kitalii ya New Dodoma hoteli, na kushirikisha jumla ya warembo kumi na tano toka wilaya zote za mkoa wa Dodoma, ambao hivi sasa wana endelea na kambi ya mazoezi katika Hoteli hiyo ya New Dodoma Hotel chini ya mkufunzi wao Neema Isdory (Miss Utalii Njombe 2010/2011) na Tabia Msuta (Miss Utalii Vyuo Vikuu Kanda ya Kati 2010/2011.

Mikoa na kanda karibu zote nchini wapo katika maandalizi ya fainali za mikoa na kanda zao, ikiwemo mikoa ya na tarehe za mashindano yao katika mabano Mara (7-10-2011),Shinyanga (29-10-2011), Njombe ( 26-11-2011), Iringa (28-10-2011),Kanda ya Kusini ( 2-12-2011),Kanda ya Kaskazini ( 3-12-2011),Dodoma ( 22-10-2011),Vyuo Vikuu Kanda ya Kati (8-12-2011),Kanda ya Magharibi (11-12-2011),,Kanda ya Mashariki (4-2-2012),Dar Es Salaam (28-1-2012), Kinondoni (9-12-2011),Temeke (31-12-2012),Ilala (24-12-2011),Pwani (25-12-2011), Kanda ya Ziwa (26-11-2011), Vyuo Vikuu Kanda ya Magharibi (21-1-2012),Morogoro (24-12-2011),Tabora (29-10-2011), aidha kalenda na tarehe kwa fainali za mikoa yote na kanda zote itatangazwa rasmi 5-10-2011 katika mkutano na waandishi wa habari wa vyombo mbalimbali vya kitaifa na kimataifa jijini Dar es Salaam.
Fainali za mwaka huu katika ngazi zote zinalenga, kuhamasisha na kutilia mkazo zaidi katika kuhamasisha Utamaduni, Utalii wa Ndani, Utalii wa Kitamaduni, Uzalendo kwa taifa na utumiaji wa Bidhaa za Tanzania, vita dhidi ya uharibifu wa Mazingira, Uvuvi haramu, Uwindaji Haramu ,.Mila Kongwe, Mila  Potofu, na vita dhidi ya Ujinga, Umasikini na Maradhi kupitia Utalii.
Wadhamini waliojitokeza ni pamoja na Asante Water, Kifimbo Radio, New Dodoma Hotel, Ngoto Funiture, Royal Vilage, Clouds Fm Radio, TANAPA, Ngorongoro Creater, VETA Hotel, Side Way Lodge, Shabibi Buss Service, Moronga By Makai Enterprises, Tanzania Daima & Sayari News Paper, Image Masters, Papaa Msofe, Zizzuu Fasheni, Dar City College, Kumekucha Action Mart, Viovena & Co LTD, pamoja na Waheshimiwa Wabunge wa Dodoma. 
Taarifa hii Imetolewa na Charles Gabriel Mkurugenzi wa Miss Utalii Mkoa wa Dodoma na Kuthibitishwa na Gideon Chipungahelo Rais Miss Utalii Tanzania



LAY IT ON ME YA KELLY ROWLAND SASA IKO KIDEONI
Although Kelly Rowland’s ‘Motivation’ video was almost too hot for TV, she’s definitely serving up more sexy in her latest video for her second single, ‘Lay It On Me’.   The video isn’t ready to premiere just yet, but in the meantime Kelly gives a quick behind the scenes peek at the visual that includes lots of boys with hot bodies and of course, Big Sean.

No comments: