Mkurugenzi wa Tanzania One Thetre (TOT) ambaye pia ni Mbunge wa Mbinga Magharibi, John Komba akizunguma na waandishi wa habari nyumbani kwake, Mbezi Tangi Bovu, Kawe, Dar es Salaam, leo wakati
akizungumzia hali ya afya yake baada ya kurejea nchini akitoka nchini
India alikokwenda kufanyiwa upasuaji. Kushoto ni Mkewe, Salome Andrew
Komba.
**********************************
NA BASHIR NKOROMO
MKURUGENZI
wa Kundi la Tanzania One Theatre (TOT) ambaye pia ni Mbunge wa Mbinga
Magharibi, John Komba amerejea kutoka India ambako amefanyiwa upasuaji
kumtibu ugonjwa wa nyonga ulilokuwa ukimsumbua upande wa mguu wake wa
kulia.
Akizungumza
na waandishi wa habari, jana Julai 27, 2012, nyumbani kwake Mbezi kwa
Komba, mjini Dar es Salaam, Komba alisema amerejea nchini, Juzi, baada
ya kupatiwa matibabu hayo kwenye hospitali ya Appolo iliyopo Hydrabad
nchini India tangu mwanzoni mwa wezi huu.
Alisema,
aliondoka nchini, Julai 2, 2012, baada ya kupelekwa na serikali kwa
maelekezo ya Rais Jakaya Kikwete, Spika wa Bunge Anna Makinda na Katibu
wa Bunge John Kashilila na kwamba alikwenda baada ya kukosa matibabu
hapa nchini kwa sababu ya mgomo wa madaktari.
"Siku
napelekwa Muhimbili tu, tayari madaktari walikuwa wameanza siku ya
kwanza ya mgomo wao, nikawa sina namna ila kuujulisha uongozi wa Bunge
na kisha nikamuomba Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete, naye kwa
mamlaka yake akanisaidia haraka kama ambavyo huwasaidia wengine kwenda
kutibiwa nje", alisema Komba.
Alisema,
uzito ulichangia sana kusababisha mifupa kusagana kwenye nyonga upande
wa mguu wa kulia, ambapo hadi anakwenda India alikuwa na uzindo wa kilo
138 wakati wastani wa uzito aliotakuwa kuwa nao kulingana na ukumbwa wa
mwili wake ni kilo 90 au 100 tu.
"Amesema,
baada ya matibabu amerejea nchini akiwa na uzito wa kilo 128 ambao hata
hivyo ametakiwa kuudhibiti na kuupunguza katika siku hizi ambazo
atalazimika kupumzika nyumbani kabla ya kuanza kazi, Mwezi Septemba
mwaka huu kama alivyoelekezwa na madaktari.
Akizungumzia
upasuaji ulivyoendeshwa, Komba alisema, ulichukua saa tano na
kukamilika bila matatizo katika upasuaji huo ambao alisema sehemu
iliyopasuliwa ni ya ukumbwa wa futi moja.
Alisema,
hata hivyo baada ya upasuaji huo, hakuweza kurejea katika wodi ya
kawaida, kwa sababu majongwa kadhaa yaliibuka ikiwemo homa kali, presha,
hivyo akalazimika kulazwa katika wodi ya wagonjwa waliopo kwenye
uangalizi maalum (ICU) kwa siku tano.
"Sasa
nimerejea nikiwa mzima, kwa sasa natumia fimbo hii, ili kuwezesha uzito
uzilemee upande wa kulia nilikopanyiwa upasuaji, lakini sijambo
kabisa", alisema Komba.
Komba
alilaani baadhi ya vyombo vya habari ambavyo viliripoti kwamba katika
kuugua kwake alikuwa mahututi na kwamba alikuwa anaugua figo.
"Jamani
ninyi waandishi wa habari, jizoesheni kuandika habari zilizokamilika
siyo kurashia-rashia tu na kuzusha uongo, mfano gazeti moja liliandika
eti naugua figo nipo mahututi, wakati si kweli kabisa, ilikuwa jambo
rahisi tu, kuja hapa nyumbani na kuniuliza au kuuliza mke wangu
lingepata kwa uhakika ninachoumwa", alisema Komba.