Pages

BRAND NEW MUSIC

metty magese

metty magese

Listen & Download

http://mdundo.com/a/32626

Saturday, August 24, 2013

FILAMU YA LULU YAPIGWA STOP KUINGIA SOKONI





Msanii wa filamu Elizabeth Michael (Lulu) akiweka sahihi yake kuashiria amekubaliana na taratibu zote alizoelekezwa na Bodi ya Filamu wakati wa ukaguzi wa filamu yake ya “Foolish Age”.PIX 1 

Katibu Mtendaji Bodi ya Filamu Tanzania Bi. Joyce Fissoo akiwaonyesha wajumbe pamoja na wahusika wa Kampuni ya Proin Promotions baadhi ya maeneo muhimu ya kufanyiwa marekebisho wakati walipowasilisha filamu yao ya “Foolish Age” katika Bodi ya Filamu kwa ajili ya ukaguzi. PIX 2

Msanii wa filamu Elizabeth Michael (Lulu) akieleza jambo mbele ya Katibu Mtendaji Bodi ya Filamu Tanzania Bi. Joyce Fissoo wakati kampuni ya Proin Promotions ikiwasilisha filamu yake ya “Foolish Age” kwa ajili ya ukaguzi. Bodi ya ukaguzi wa filamu na michezo ya kuigiza nchini imeipiga stop filamu ya Foolish age ya msanii wa kike mwenye mvuto Bongo Elizabeth Michael ‘Lulu’ baada ya kukuta picha zilizo nje ya maadili ya Kitanzania katika filamu hiyo....

Filamu hiyo ambayo ilipanga kuzinduliwa mwezi huu tarehe 30 katika ukumbi wa Mlimani City inahitaji marekebisho.

Kikwazo kilichoikumba filamu hiyo ni nguo fupi zilizotumiwa na waigizaji walioshiriki katika filamu hiyo ambayo inatabiriwa kufanya vizuri katika soko la filamu Bongo kama itafanikiwa kuzinduliwa na kuingia sokoni, Kwa  mujibu  wa  Lulu  Michael,  juhudi zinafanyika kuhakikisha kuwa marekebisho yanafanyika ili kwenda na ratiba kama ilivyopangwa.

No comments: