Pages

BRAND NEW MUSIC

metty magese

metty magese

Listen & Download

http://mdundo.com/a/32626

Thursday, December 6, 2012

UNIQUE MODEL 2012 IMEIVA NI ZAIDI YA SHINDANO

Endelea kufatilia vyombo vya habari,ni hivi karibuni wanamitindo 12 kupanda jukwaa moja kumsaka Unique model of a year 2012,matangazo ya luninga kupitia Dtv,88.4 clouds fm,Gazeti la Tanzania Daima,Gazeti la kiu na blogs mbalimbali,matangazo yatakujia hivi karibuni stay tuned ujue ni lini na wapi fainali.

NJAA MBAYA,MWINYI AMLAMBA MIGUU JIDE

Katika kile kinachoonekana kama maisha kuanza kumpiga aliyekuwa muimbaji wa Machozi Band, Mwinyi Goha baada ya kuitosa, inadaiwa kuwa amempigia magoti Lady Jay Dee na kumuomba arudi kuendelea na kazi kwenye bendi hiyo.
Mwinyi alijiondoa Machozi Band katikati ya mwaka huu kwa madai ya kuchoshwa na uongozi wa kibabe, dharau na ubabaishaji wa wamiliki wa bendi hiyo.

 Pia alimshutumu Jaydee kwa kuwa na roho mbaya ikiwa pamoja na kumlipa ujira mdogo ambao nao alikuwa akipewa kwa masimango.

Na sasa Kupitia Facebook, Lady Jaydee amesema muimbaji huyo ameomba msamaha na anataka arejee kuendelea na kazi.

“Nadhani wote mnamkumbuka Mwinyigoha, aliekuwa MACHOZI BAND kitambo. Baada ya yote yaliotokea na mlioyasikia anataka kurudishwa kundini, Naomba mvae kiatu changu…, Je ingekuwa wewe ni JIDE ungemsamehe na kumrudisha tena kazini?? Jiweke kwenye nafasi yangu unipe jibu,” ameandika Jide.

Kutokana na maelezo hayo bado hatma ya Mwinyi Goha kurudishwa kwenye bendi hiyo ipo mikononi mwa mashabiki wa Lady Jaydee ambao wengi wamemshauri amsamehe.

Wednesday, December 5, 2012

MFANYABIASHARA WA MADINI AFIA HOTELI ARUSHA


MFANYABIASHARA wa madini aina ya Tanzanite mkoani Arusha,Ngerii Olerumwa anayekadiriwa kuwa na umri wa zaidi ya miaka 40 amekutwa amekufa katika mazingira ya kutatanisha ndani ya hoteli ya Premier Palace ambayo timu ya wabunge wa bunge la jamhuri ya muungano imeweka kambi hotelini hapo jijini Arusha.

Maiti ya mfanyabiashara huyo iligundulika majira ya saa 3 ;30 asubuhi jana mara baada ya mhudumu wa hoteli hiyo kugonga kwa muda mrefu mlango wa chumba alichokuwa amefikia marehemu huyo bila mafanikio na kisha kubaini alikuwa amefariki dunia.

Kwa mujibu wa mashuhuda wa tukio hilo akiwemo meneja wa hoteli hiyo ambaye alikataa kutaja jina lake hadharani alisema kwamba marehemu huyo aliwasili hotelini hapo mnamo desemba 3 mwaka huu majira ya saa 1 ;00 jioni na kukodi chumba kimojawapo hotelini hapo.

Meneja huyo akisimulia tukio hilo alisema kwamba marehemu aliwasili akiwa peke yake hotelini hapo na kubainisha kwamba yeye ndiye alikuwa mtu wa mwisho kukodi chumba hotelini hapo.
Hatahivyo,alidai kwamba ilipotimu jana majira ya saa 3 ;30 asubuhi wakati mhudumu wa hoteli hiyo akigonga mlango wa chumba alichofia marehemu kwa lengo la kufanya usafi mlango huo haukuweza kufunguliwa kwa wakati hali iliyowapelekea kufanya juhudi za kuufungua mlango huo kwa lazima.

Alisema kwamba baada ya kufanikiwa kuufungua mlango huo walijaribu kumwamsha marehemu lakini hakuweza kuamka hali iliyowapelekea kuliarifu jeshi la polisi kuhusiana na tukio hilo.

Gazeti hili lilipofika maeneo ya hoteli hiyo liliwashuhudia askari wa upepelezi kutoka jeshi la polisi mkoani hapa wakichukua maelezo kwa baadhi ya watumishi wa hoteli hiyo wakiwemo walinzi wa hoteli hiyo huku baadhi ya wabunge wanaounda timu ya wabunge wa bunge la jamhuri wakitaharuki kutokana na tukio hilo.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti ndugu wa marehemu ambao walikusanyanya nje ya hoteli hiyo walisema kwamba wameshtushwa na kifo cha ndugu yao na wanahisi kwamba aliuwawa katika mazingira ya kutatanisha huku wakilitaka jeshi la polisi kubaini chanzo cha kifo cha marehemu.

Akihojiwa na waandishi wa habari kamanda mkuu wa jeshi la polisi mkoani Arusha,Liberatus Sabas alikiri kutokea kwa tukio hilo huku akisisitiza kwamba jeshi lake linachunguza kwa kina kifo hicho.

Sabas,alisema kwamba mwili wa marehemu umehifadhiwa katika chumba cha kuhifadhia maiti ndani ya hospitali ya mkoa ya Mt,Meru na atatoa taarifa kamili ya tukio hilo kuanzia leo mbele ya waandishi wa habari.

WASHIRIKI WA UNIQUE MODEL 2012 WALIVYOJIACHIA GIRAFFE OCEAN VIEW HOTEL HOTEL

Wabunifu wa mavazi kazi kwenu,jitokezeni kwa wingi kuwavalisha wanamitindo hawa wenye ndoto ya kuwa wanamitindo maarufu nchini Tanzania,kwa kufanya hivyo mbunifu utapata nafasi nyingine ya kutangaza kazi yako ya ubunifu kupitia shindano hili lenye mvuto wa aina yake nchini Tanzania.  wasiliana nasi :-0714796622,face book:- Unique modo na twiter:-  Unique model.

Tuesday, December 4, 2012

PEDESHEE WEMA SEPETU ALIFUNIKA WASANII WENZAKE MSIBA WA SHARO MILONEA

   Msanii nyota wa filamu nchini na aliyekuwa Miss Tanzania 2006/07 Wema Isack Sepetu katikati ya wiki iliyopita alilitia aibu kundi la bongo muvi kwa kufanya kitu cha kipekee kwenye msiba wa mwanamuziki na msanii wa komedi aliyefariki kwa ajali Mkoani Tanga Sharo Milionea.
Wema Sepetu ambae siku za hivi karibuni  amepumnzika skendo kwenye vyombo vya habari alipongezwa na watu kwa uungwana aliounonesha baada ya kutoa mchango mwingi kuliko msanii yeyote wa kundi hilo linalosifika kwa kashfa za ngono.
   Habari zilizothibitishwa na mmoja wa ndugu wa marehemu ambae aligoma kutaja jina lake kwa madai kuwa yeye si msemaji wa familia alisema kuwa” Ni kweli wasanii mbalimbali walijitolea kwa kuja huku Tanga lakini Wema ndiye aliyetoa mchango mkubwa sana kwa kutoa shilingi laki mbili peke yake 200000/= huku wasanii wengine wakiishia kutia aibu”Alisema mtu.
   Aidha ilidaiwa Wema ndiye aliyeonekana kuwa na uchungu wa dhati toka moyoni ambapo licha ya mchango huo pia alionekana kujishughulisha na kazi za kusaidia majukumu msibani hapo bila kujali ustaa wake aliokuwa nao.

MAJINA YA WABUNIFU WATAKAONG'ARA SWAHILI FASHION WEEK 2012

 The names of all designers are finally here...with official schedule of who will be showcasing when...am exciteeeed!

Monday, December 3, 2012

KAJALA KAFUTUKA FUTUUH GEREZANI..!!


MSANII wa filamu Bongo ambaye yuko nyuma ya nondo Gereza la Segerea, Dar es Salaam kwa mashitaka ya kuuza nyumba iliyowekewa kizuizi na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), Kajala Masanja anaweza kupata gonjwa la moyo kufuatia kunenepa sana akiwa gerezani humo.
Kajala Masanja wakati akipandishwa katika Mahakama ya Kisutu, Dar es Salaam Jumatatu wiki hii. Kajala aliyepandishwa katika Mahakama ya Kisutu, Dar es Salaam Jumatatu iliyopita, muonekano wake kwa sasa uliwashangaza watu katika mahakama hiyo baada ya kuonekana amenenepa sana kuliko alivyokuwa uraiani.
Baadhi ya watu walisikika wakihojiana wenyewe kwa wenyewe kama kuishi gerezani kwa muda mrefu kunasababisha mtu kunenepeana kama yeye.
“Hivi kumbe gerezani kunaweza kumnenepesha mtu jamani? Kajala shavu dodo,” alisema mwanamke mmoja ambaye mwenzake alikuwa kinyume naye.
Mwenzake: “Ila kunenepa kwa aina hii halafu unakaa kwa muda mrefu kuna hatari ya kupata magonjwa ya moyo. Unajua uraiani chakula kinachukuliwa na kazi za siku nzima, gerezani muda mwingi ni kukaa tu, inabidi afanye mazoezi ya kupungua.”

Kajala akionekana kanenepa kuliko alivyokuwa uraiani. Mwingine: “Dah! Hebu mcheki kwanza, yaani anazidi kuwa bomba kila kukicha, sasa hivi amekuwa shavu dodo kuliko hata alivyokuwa uraiani! Tusidanganyane jamani, piga ua kutakuwa na mtu anamtunza huyu hukohuko aliko si bure. ”
Hata hivyo, miongoni mwa waliodatishwa na muonekano wa Kajala ni msanii mwenzake, Mahsein Awadh ‘Dokta Cheni’ ambaye alimsogelea na kutaka kumkumbatia lakini alizuiliwa na askari waliokuwa wakimlinda.

...akiwa na sura ya tabasamu.

BERENIKI KIMARO NDIYE MSHINDI WA MAISHA PLUS 2012

Na Mshindi wa Maisha Plus 2012 ni BERENIKI KIMIRO, amejishidia Tshs. Millioni 20, -- Mshindi wa Pili ni Venance Mushi amejishindia Tshs. Million 6…. Mshindi wa Tatu ni Justine Bayo, amejishindia Tshs. Million 4.
Mshindi wa Maisha Plus 2012, BERENIKI KIMIRO ameanza kwa Kumshukuru Mungu kwa ushindi, asema ye si kitu kwa wenzake, hilo ni zali tu.. Amemshukuru baba yake mzazi kwa kumshauri kusali.. Amewashukuru pia wapenzi watazamaji kwa kumpiga kura, ameahidi kuendeleza kile alichokianza kijijini na kuitendea haki nchi yake.. Amemshukuru babu, Brother Masoud na Crew nzima ya Maisha Plus.. Amemshukuru pia mwanae Kelvin (6yrs) kwa kuvumilia kipindi chote bila kuongea na mama.. Amesema Mungu amejibu maombi yake kwani ukipiga goti, maombi yako yatajibiwa..

RAIS KIKWETE AAHIDI KUMPA BAJAJI MLEMAVU LINDI

Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiongea na mlemavu Bwana Mwendo Saidi katika kijiji cha Mandawa wilaya ya Lindi vijijini leo wakati Rais aliposimama kwa muda kuzungumza na wananchi wa kijiji hicho ili kujua changamoto za kimaendeleo zinazowakabili.Mlemavu huyo alimweleza Mheshimiwa Rais Kuwa yeye na wenzake wawili wanaomba wapatiwe Bajaji ili kuanzisha mradi utakaowawezesha kujikimu kimaisha.Mheshimiwa Rais Kikwete aliridhia ombi hilo na kuahidi kutoa msaada huo mara moja.Rais Kikwete yupo mkoani Lindi kwa ziara ya kikazi ya kukagua miradi ya maendeleo.

Sunday, December 2, 2012

THE MAKING OF NATAKA KULEWA YA DIAMOND

Director Raqey toka I-VIEW akifanya yake pia...
 
Mose Iyobo,Emma Platnumz & Rama (Wasafii)

Mose Iyobo


Nisha kageuka kuwa Pedeshee wa Kike nikumwaga minoti 

WEMA SEPETU NA DIAMOND PENZI LAO LAFUKUTA UPYAA..!!

 Penzi la Wema sepetu na Diamond platnum inaonekana kushika kasi upya baada ya kuendelea kuwepo kwa ukaribu ambao umezua minong'ono mingi jiji hapa.
 Wema amekuwa msaada mkubwa kwa Diamond kwa vitu mbalimbali na hii imethibishwa na Diamond mwenyewe kuwa kati ya wanawake waliomsaidia kufika hapo alipo ni Wema sepetu.
 Kuthibitisha hayo ni kutokana na muoendelezo wa nyimbo anazozitoa Diamond ambazo zina baadhi ya mistari katika mashairi yaliotungwa na Wema ikiwepo nyimbo ya 'nataka kulewa' ambayo inamtambisha msanii huyo kwa sasa.
 Katika hali ya uperuzi na kudadisikuhusiana na kuwepo kwa mahusiano yanayoendelea kati ya wawili hao kuna asilimia nyingi zaidi zinazoshabikiana na ukweli wa jambo hili ingawa Diamond amekuwa katika mahusiano ya wasichana wengi tofauti lakini ni wazi anamzimia sana Wema kuliko wanawake wote aliowahi kuwa nao katika maisha ya ujana wake.

RIHANNA NA CHRISS BROWN WARUDIANA KIMAPENZI

Rihanna told Oprah Winfrey that although she loved criss Brown, that they were nothing more than friends. Well, she lied.
Chrianna is alive and well as evidenced by the intimate photo Rihanna posted on her Instagram of her hugging her boo in some revealing short-shorts after he performed at Adagio club in Berlin.
Reports say that she huged ana kissed him, so no, this is NOT a platonic hug between friends.
If nothing else, this photo and the whole “fuck the world, we love each other” campaign these two have been on prove that Chrianna is the new Bobby and Whitney.
It won’t be long before they remake Bobby & Whitney’s “Something In Common” video. Watch.

UZINDUZI WA ALBAM YA MASHUJAA LEADERS CLUB ILIVYOJILI


 Wanenguaji wa Mashujaa Band, wakikamua jukwaani wakati wa shoo ya ufunguzi wa uzinduzi wa albam yao, ambao shoo hii waliicheza jukwaani bila kumalizika kutokana na matatizo ya umeme.
 'Mkaanga Chips' wa Mashujaa, akizicharaza Drams.
 Wanamuziki wa Bendi ya Mashujaa wakiingia kwa staili yao ya kucheza muziki wa Kihindi, wakati wa shoo yao ya pamoja, ambayo hata hivyo haikuweza kumalizika.
 Wanenguaji wa Mashujaa, wakikamua jukwaani..
 Makamuzi yakiendelea..
 Shoo ilikuwa ni tamu kwa kweli, lakini haikuwa na raha kutokana na karaha ya umeme.
 Mpiga Tumba wa bendi hiyo, MCD, akizicharaza tumba....
 Sehemu ya mashabiki wa VIP waliolipa kiingilio cha Sh. 100, 000 kila mmoja, wakiwa katika eneo lao la VIP.
 Gari, alilotumia JB Mpiana kuingia uwanjani hapo......
 Mafundi mitambo, wakishangaa wasijue la kufanya baada ya kukatika kwa umeme huo kila muda.
 Mtangazaji Ben Kinyaiya, akifanya mahojiano na Jado Fidifosi wakati wakiendelea kulazimisha shoo hiyo.
 Ben Kinyaiya naye akisebeneka..
 Mnenguaji wa Mashujaa, akikamua.
 Rapa wa Bendi ya Mashujaa, Ferguson, akiwachezesha wanenguaji wake.....kwa rap ya 'Kibega'

Saturday, December 1, 2012

VITU VYA SHARO MILIONEA VILIVYOIBIWA VYAANZA KUPATIKANA


Baadhi ya vitu vya marehemu Sharo milionea vilivyokamatwa baada ya msako mkali baina ya Polisi na wananchi wa Kijiji Songa Kibaoni.

WATU wanaosadikiwa kuiba vitu vya marehemu Hussein Mkiety maarufu kwa jina la 'Sharo Milionea' aliyefariki kwa ajali ya gari katika kijiji cha Songa Kibaoni wilayani Muheza Novemba 26 mwaka huu, wamesalimisha baadhi ya vitu hivyo kwa mwenyekiti wa Kijiji hicho huku wakiendelea kuishi mafichoni kuogopa kutiwa mbaroni.

Watu hao wamesalimisha vitu hivyo baada ya Mkuu wa wilaya ya Muheza Subira Mgalu ambaye ni mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama kuwatangazia kwamba wale wote waliomwibia marehemu watasakwa na kuchukuliwa hatua za kisheria kufutia kitendo walichokifanya kutokuwa cha kiungwana.

Mkuu huyo pamoja na jeshi la polisi wilayani humo waliendesha msako juzi usiku lakini hawakuweza kuwakuta watu baada ya kuzihama nyumba zao kuogopa kutiwa mbaroni na mkuu huyo kuwalazimsha baadhi ya familia walizozikuta kuendesha zoezi la kuwataja watu wanaohofiwa kwamba huenda watakuwa wamchukua vitu hivyo.

Kamanda wa polisi mkoani Tanga ACP Constatine Masawe, aliwaeleza waandishi wa habari ofisini kwake kuwa, usiku wa kuamkia juzi mwenyekiti wa kijiji hicho Abdi Zawadi alipelekewa vifaa mbalimbali ikiwemo nguo ambazo marehemu alikuwa amezivaa pamoja na spea tairi ambalo waliling'oa na kutokomea porini.



Kamanda huyo alitaja vitu vilivyokabidhiwa kwa mwenyekiti huyo kuwa ni pamoja na begi lake lililokuwa na 'viwaro' nguo zake, betri ya gari hilo lililokuwa na namba T 478 BVR aina ya Toyota Harrier, saa yake ya mkononi, simu yake aina ya Blackberry na redio ya gari iliyokuwa pia imeng'olewa na wezi hao.



Kamanda huyo alisema vitu hivyo vilipelekwa na mtu mmoja ambaye kwasasa jeshi hilo linashindwa kumtaja jina lake kwa vile alijitambulisha kwamba ana undugu na wezi hao ambao walimpa vitu hivyo avipeleke kwa uongozi wa kijiji hicho hatua ambayo alidai kwamba wanafanya uchunguzi ili kuwatia nguvuni wale wote waliohusika na tukio hilo. 
Alisema waliweka mtego baada ya kusikia kwamba kuna mwizi mmoja wapo anaitafutia mteja simu ya mkononi ya marehemu lakini wakati wameweka mtego huo kijana huyo alipokuwa akijadiliana bei na mtu waliyemweka, alibaini na alipompa mkononi alikimbia vichakani kuogopa kukamatwa.
 

Kamanda huyo aliwashukuru baadhi ya wananchi wa kijiji hicho pamoja na Mkuu wa wilaya kuhakikisha wanashirikiana na jeshi hilo ili kuwabaini na kuwakamata wote waliohusika katika tukio hilo ambalo limetokea huku wananchi kadhaa wakiomboleza kifo cha msanii huyo ambaye alizikwa kijijini kwao Lusanga wilayani Muheza juzi.

Katika hatua nyingine kamanda huyo alisema katika matukio ya ajali yaliyotokea mwezi huu wa Novemba jumla ya ajali 10 zilitokea ambazo zimesababisha vifo ni 7 na zilizosababisha watu kujeruhiwa ni tatu, kati ya hizo watu 12 walipoteza maisha na wengine wanane walijeruhiwa.

Kamanda Masawe alisema jumla ya makosa 2,365 yalitendeka na kupigwa faini iliyosababisha serikali kujiingiza kiasi cha sh. 70,950,000 hatua ambayo kamnada huyo alisema haioneshi kwamba watumiaji barabara wamekuwa wakifuata wakitii sheria za usalama barabarani.