Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) kupitia kinywaji chake cha Redd’s Original imeandaa maonesho makubwa ya mavazi yatakayowashirikisha warembo wa Miss Tanzania 2011 yenye kaulimbiu ya kusheherekea miaka 50 ya uhuru wa Tanzania.
Redd’s ambayo ni kinywaji rasmi cha shindano la Miss Tanzania 2011 wamedhamiria kutumia maonesho haya kama chachu ya kuwapatia washiriki nafasi ya kuonesha vipaji vyao katika sanaa ya mitindo.na kuwakutanisha na wadau wa fani ya mitindo ili waweze kujipatia njia mbadala ya kujiendeleza baada ya mashindano.
Akiwa anaongea kuhusiana na onesho hili meneja wa kinywaji cha Redds Bi. Victoria Kimaro alisema “Redds kama mdhamini aliyeshiriki kikamilifu kwenye mashindano haya ya urembo toka kwenye ngazi za chini za vitongoji imetambua kuwa kuna umuhimu wa kuwapatia washiriki nafasi za ziada za kuonesha vipaji vyao kwenye fani mbalimbali ikiwemo ya ulimbwende na mitindo ili kuwawezesha kuwa na njia mbalimbali za kujipatia mafanikio ya kimaisha. Maonesho haya ya mavazi yatawakutanisha warembo na wadau mbalimbali wa mitindo kama wabunifu wa mavazi, taasisi za walimbwende na makampuni ya matangazo ili waweze kugundua vipaji vipya na kuvipatia nafasi ya kuviendeleza.” Bi. Kimaro aliendelea kwa kusema kuwa “Tasnia ya urembo ina mchango mkubwa kwenye jamii yetu sio tu kwa upande wa burudani bali inawapatia nafasi warembo mbalimbali Tanzania kukuza vipaji vyao na kuwekea msingi ambao wakijipanga vizuri utawajenga na kuwaletea mafanikio mbalimbali kweye maisha yao. Maonesho haya ya mavazi ni mojawapo ya fursa ambayo Redds inayowapatia warembo wakuze vipaji vyao kama njia mbadala ya kujipatia maendeleo na mafanikio baada ya shindano la kitaifa.”
Maonesho hayo ambayo yatafanyika siku ya Ijumaa ya tarehe 2 Mwezi wa 8 katika viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam yatajumuisha wadau mbalimbali wa mitindo, burudani kutoka kwa Banana Zorro na B Band pamoja na mwanadada mkali wa mziki wa kizazi kipya Shaa. Warembo wa Miss Tanzania siku ya onyesho watavaa nguo zilizobuniwa na wanamitindo mbalimbali kama Binti Africa,, Kijo na Franco. Onyesho hili pia limemshirikisha mwanamitindo maarufu kutoka mji wa New York ambaye pia amefanya kazi na wabunifu mbalimbali wa kimataifa na nyota mbalimbali wa nchini Marekani Bi. Rosemary Kokuhilwa ajulikanaye kama Fashion Junkii.
Siku ya onesho warembo wataanza na safari ya kutembelea kiwanda cha Bia Tanzania (TBL) kilichopo Ilala Dar es Salaam ambapo watashuhudia mtiririko mzima wa upikaji wa bia na kujumuika na wafanyakazi wa kiwandani hapo kwenye chakula cha mchana.
Redd’s Original imeshiriki kikamilifu kwenye mashindano ya Miss Tanzania 2011 ambapo imefadhili zaidi ya vitongoji 35 na pia kama mdhamini mkuu wa Redds Miss Ilala, Redds Miss Temeke na Redds Miss Kinondoni.
SHABA YA WIZI YA MILIONI 400 YANASWA DAR
Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, limewataka wezi wa madini ya shaba na wasafirishaji wa bidhaa kinyume cha sheria wajisalimishe wao wenyewe. Akizungumza na waandishi wa habari jana jijini hapa Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Suleimani Kova alisema kuwa ameweka mtandao wenye vikosi maalum kwa ajili ya kuwashughulikia wezi hao. Kamanda Kova alisema mpaka sasa wanamshikilia mfanyabiashara mmoja (jina limehifadhiwa) kwa uchunguzi zaidi) baada ya kukamatwa na madini ya shaba yenye thamani ya Sh. milioni 400 ambayo yalikuwa yanasafirishwa kutoka Zambia kwenda katia bandari ya Dar es Salaam. Aidha, Kova alisema wizi huo unahatarisha uchumi wa nchi na kusababisha serikali kukosa mapato.
SWALA YA IDD EL FITRI BUKOBAWakazi wa mkoa wa Kagera wakiswali swala ya Idd El fitri leo asubuhi mjini bukoba.