Habari za uhakika kuhusiana na chanzo cha kifo cha msanii Hussein Ramadhan a.k.an Sharo milionea ni kwamba gari yake aina ya Toyota harrier ilipata pancha tairi la upande wa kulia na kukosa
mwelekeo kisha ikaacha njia na kuelekea mtaroni lakini ule mtalo
haukuizuru sana gari hiyo ikaruka na kuingia katika shamba la maindi.
Kitu kilichoshangaza wengi ni sehemu ambayo si hatarishi sana kiudereva sababu iko tambarare na kona si kali eneo hilo.
Chanzo
cha habari kinaendelea kufafanua kuwa baada ya gari kuacha njia ilienda
kugonga mti mkubwa na kuung'oa baada ya kuuchana katikati kutokana na
gari ilivyokuwa mwendo kasi.
Mwili
wa marehemu ulitupwa nje ya gari baada ya kugonga mti huo ambapo gari
hiyo iliharibika vibaya kuanzia kwenye roof hadi vioo vyote kupasuka
japo vizuizi vilifunguka lakinini havikusaidia.
Baada
ya kishindo kikubwa cha mlio wa pancha kilisikika kwa wakazi wa kijiji
hiko na kuamua kujitokeza kujua nini kimejili pale na wakati wanafika
hapakuwa na mwili wa marehemu katika eneo la tukio,ndipo mama mmoja
aligundua mwili wa msanii huyo mita chache kutoka gari ilipogonga mti na
kuharibika vibaya.
Mganga
mkuu wa hospitali teule ya Muheza amesema kuwa chanzo cha kifo cha
Sharo ni kubonyea kwa kichwa ikiambatana na majeraha yaliopo kichwani na
sehemu ya mabega ndiyo yalipelekea msanii huyo kupoteza maisha papo
hapo.
Hata
hivyo jeshi la polisi lilikuja masaa mawili baada ya kutokea ajali
hiyo,ambapo gari la Tanesco ndilo lililotumika kuvuta gari hiyo hadi
kituo cha polisi wilayani humo.
habari zaidi endelea kuchungulia hapahapa .
Mwili wa Sharo utazikwa kesho saa saba mchana .
No comments:
Post a Comment