Kila kukicha
vita dhidi ya biashara haramu ya dawa za kulevya inazidi kupamba moto,
wakati mataifa mbalimbali yakizidi kuimarisha udhibiti wa biashara
hiyo, na wafanyabiashara hiyo wanazidi kuja na mbinu mpya za
kusafirisha dawa hizo.
Huko Colombia
mwanamke mmoja raia wa Canada amekamatwa uwanja wa ndege akiwa na
tumbo la ujauzito wa bandia ambalo ndani yake alificha kilo mbili za
dawa za kulevya aina ya Cocaine.
Polisi wa
uwanja wa ndege wa Bogota Colombia alimshtukia mwanamke huyo raia wa
canada Tabitha Leah Ritchie aliyeonekana kuwa na tumbo lisilo la
kawaida ndipo baada ya kumkagua wakakutana na dawa hizo.