Pages

BRAND NEW MUSIC

metty magese

metty magese

Listen & Download

http://mdundo.com/a/32626

Sunday, September 15, 2013

MAYWEATHER AMDUNDA SAUL ALVAREZ

Alfajiri ya leo Bondia Mayweather amefanikiwa kumshinda Saul Alvarez wa Mexico ambaye kabla ya hapo alikuwa hajapoteza pambano hata moja.
Jaji wa kwanza alitoa sare ya pointi 114-114, lakini wawili wakatoa ushindi kwa Mayweather kwa pointi 116-112, 117-111.
Mayweather alitawala karibia raundi zote kuanzia ya tatu akipiga ngumi moja moja za kudokoa ambazo zilimzidi Mmexico huyo.
Kwa upande wa raundi, Mayweather alishinda kila raundi kuanzia ya kwanza hadi ya 12.
Alvarez alionyesha uwezo kwa kupambana hadi mwisho, hata hivyo Mayweather alionyesha ni bora zaidi yake kiufundi.
Namna alivyokuwa anakwepa na kupiga, alimpa wakati mgumu Alvarez ambaye pia alionyesha atakuwa tishio zaidi.
Hilo lilikuwa ni pambano la kwanza la Alvarez kupoteza baada ya kucheza mapambano zaidi ya 40, huku Mayweather akiendelea na rekodi ya kutopoteza.
 Still champion: Floyd Mayweather was hugely impressive in beating Saul Alvarez over 12 rounds in Las Vegas

No comments: