Mfanyabiashara maarufu na msanii nyota wa bongo muvi ambae ni mtoto wa
Waziri Mkuu mstaafua aliyefahamika kwa jina la Libart Msuya katika ya
wiki hii alionja joto ya jiwe baada ya kuhenyeshwa masaa kadhaa kwa
kupekuliwa alipokuwa anareja toka nchini Uingereza huku msanii mwenzake
Manaiki Sanga akihangaika kumnusuru.
Habari za uhakika zilizonaswa na Xdjz ambayo ilikuwepo kwenye viwanja
hivyo kwa ajili ya kumpokea mzanii Azonto ambapo Libart alisafiri ndege
moja na Azonto wakitokea Uingereza ilishuhudia jambajamba hiyo aliyokuwa
akipewa Libert kwenye sehemu ya kutokea wageni wanaokuwa wanawasili.
Libert Msuya ambae ana uaraia wa Ungereza licha ya kwamba ni mtanzani
siku za hivi karibuni alikuwa nchini huko ndio familia yake ilipo na
siku hiyo ya tukio alikuwa anarejea Tanzani huku akiwa na mabegi kibao
na baada ya kufika Air Port ya Dar mabegi hayo alifanyiwa uchunguzi
mkubwa kiasi cha kusababisha askari wote kumzunguka.
Hata hivyo hali hiyo iliyodumu kwa dakika 40 ilimlazimu rafiki wa karibu
na mtoto huyo Manaiki Sanga “The Don” kuanza kuchanganyikiwa akizani
labda huenda ni kweli rafiki yake huyo alikuwa na mzigo.
Aidha baada ya kuachiwa huru Libert alitoka nje huku akipokelewa na
Manaiki, hata hivyo mwandishi wetu alifanikiwa kuongea na Libert ambae
alisema “ Ni utaratibu ambao upo kila
nchi wa kusachiwa hivyo mimi sikuona tatizo pele na wala mimi
sijihusishi na biashara yoyote haramu” Alisema Libert
Hata hivyo nae msanii Manaiki Sanga” The Done” aliiambia blog hii kuwa
biashara ya madawa sio rahisi kama inafanywa na watu wenye mioyo migumu
huku wakiwa wamekula viapo kwamba lolote litakalotokea poa na sio kazi
rahisi ni kama sanaa wanayoifanya wasanii wote.
No comments:
Post a Comment