Pages

BRAND NEW MUSIC

metty magese

metty magese

Listen & Download

http://mdundo.com/a/32626

Friday, September 20, 2013

PENZI LA LINAH NA AMINI CHALI

Msanii wa muziki wa bongo fleva ambaye sasa ni mjasiriamali pia Anasteria Sanga Linah au muite Ndege Mnana amefunguka kuwa producer wa studio ya Bhitz Pancho Latino ndiye mwenye siri nzito ya penzi lake na msanii mwenzake Amini ambaye kwasasa penzi lao limekuwa stori ya kale baada ya kuachana.
Linah amesema tokea wanaanza mapenzi yao Pancho ndiye alikuwa mtu pekee anayejua mambo mengi kuwahusu wao na jinsi walivyotumbukia katika penzi ambalo anasema yeye binafsi ndiye hasa alikuwa akimpenda Amini kupita kiasi japo baadaye akagundua kuwa hata mwenzake naye anamzimika na hivyo penzi likawa linasonga.
"Yaani we muulize Pancho yule ndio ana siri kubwa sana ya penzi langu na Amini,yaani jamani nilimpenda sana Amini mpaka nikakubali kuingia kwenye mapenzi na nilimpenda hasa kutoka moyoni,kuna vitu vingi nyuma yake ambavyo Pancho anajua",alisema Linah.
Msanii huyo mwenye sauti tamu kiasi cha kupachikwa jina la Ndege Mnana na msanii mkongwe Patricia Hillary ameendelea kufunguka kuwa wakati ameangukia katika penzi la Amini alikuwa anawachomolea wanaume wengi waliokuwa wanamtokea tena wenye pesa zao na wengine ni watu wazito lakini aliamua kutoka moyoni kwa dhati kuwa na Amini kwahiyo akawa anamtunzia heshima yake.
Anasema kama angekuwa macho juu kuna uwezekano mkubwa asingeendelea kuwa na Amini au angekuwa anamsaliti kwa kiasi kikubwa lakini moyo wake usio na tamaa ndio ulikuwa unamfanya aendelee kumpatia penzi la kweli.
Akavujisha siri kuwa Amini ndiye aliyemtibua na ndipo akapitisha uamuzi wa kujiweka pembeni kwasababu ambazo ni ngumu kuziweka hadharani lakini mpenzi wake huyo wa zamani anazijua na ni sababu ambazo haziwezi tena kulirudisha penzi lao japo anakiri kuwa aligundua kuwa mpenzi wake huyo wa zamani anampenda siku alipomtamkia kuwa mapenzi yameisha kila mmoja ashike lake.
Anasema katika kuonesha kuwa ameachana na Amini lakini hana bifu naye wakaamua kutoa wimbo wa pamoja wa Mtima wange.
Akizungumzia show anazofanya na Amini jukwaani wakiwa kama wapenzi anasema ni kuonesha kuwa hakuna bifu na hata mabusu anayopigwa na zilipendwa wake huyo anayapokea kwasababu anashindwa kuyapotezea jukwaani akiogopa kumtia aibu jamaa huyo mbele ya mashabiki na watu wengine.

No comments: