Dereva
kutoka nchini Ujerumani Rainer Zietlow (katikati) akizungumza na
wanahabari kuhusiana na rekodi yake ya kusafiri umbali mrefu Duniani
mara baada ya kuwasili nchini Tanzania kwenye Ofisi za Alliance Autos,
Kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya CFAO Motors, Bw.Wayne
McIntosh na kushoto ni Meneja Masoko wa CFAO Motors, Tharaia Ahmed.
Na Mwandishi Wetu
DEREVA
raia wa Ujerumani Rainer Zietlof yuko mbioni kuvunja rekodi ya dunia ya
kuendesha gari kwa kilometa 17,000 kutoka Ulaya hadi Afrika.
Akizungumza
na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, Zietlof alisema kuwa hiyo
itakuwa ni rekodi yake ya tatu baada ya zile za awali alizovunja mwaka
2011 na 2012.
Awali
alivunja rekodi baada ya safari iliyojulikana kama `Panamerica’ambayo
ilimchukua kutoka Tierra del Fuego hadi Alaska kwa siku 11 na saa 17
wakati ile ya `Russtralia’ ilimtoa Melbourne, Australia hadi
St.Petersburg nchini Urusi ambako alitumia saa 18.
Zietlof
anayetumia gari aina ya VW Touareg V6 TDI alianza rasmi safari yake
Septemba 21 mwaka huu huko North Cape nchini Norway na anatarajia
kuikamilisha nchini Afrika Kusini, ambako atakuwa ametembea kwa kilometa
17,000.
Kwa
mujibu wa dereva huyo, safari hiyo ndefu imempitisha katika nchi za
Norway, Finland, Sweden, Denmark, Ujerumani, Jamhuri ya Czech, Slovakia,
Hungary, Serbia, Bulgaria, Uturuki, Misri, Sudan, Ethiopia, Kenya na
sasa Tanzania.
Dereva
huyo alizungumza na wandishi wa habari katika makao makuu ya CFAO
Motors yaliyopo barabara ya Nyerere jijini Dar es Salaam, na kusema kuwa
atachangia kiasi cha senti 20 za euro kwa kila kilomita, kwa vijiji
vya watoto wanaoishi katika mazingira hatarishi (SOS) nchini Tanzania na
Zambia.
Mbali na kuahidi kuvichangia vijiji hivyo, Zietlot pia amesisitiza kuvitembelea vijiji hivyo atakavyo vichangia.
Aidha,
amelisifia gari hilo kutokana na uwezo wake wa kukabiliana na
mazingira tofauti tofauti ya hali ya hewa kama baridi kali na joto
pamoja na barabara mbovu.
Mradi
huu wa kuzunguka sehemu mbalimbali za dunia kwa gari hilo umedhaminiwa
na makampuni ya Tehama, magari ya Volkswagen ya Ujerumani, Slovakia na
Afrika Kusini.
Katika
safari hiyo Zietlow yuko na wasaidizi wake wawili, Marius Biela ambaye
ni mpiga picha na mchukua video; Matthias Prillwitz ambaye ni mzoefu wa
mbio za magari nchini Ujerumani.
Dereva huyo alianza safari zake za barabarani mwaka 2005 na ameoa na ana mtoto mmoja.
Dereva
kutoka nchini Ujerumani Rainer Zietlof (wa kwanza kulia )akiwaelezea
jambo wanahabari hawapo pichani Kushoto kwake ni Meneja Masoko wa CFAO
Motors Ltd. Tharaia Ahmed
Mkurugenzi
Mtendaji wa kampuni ya CFAO Motors, Bw.Wayne McIntosh akielezea ni kwa
namna gani magari yao yako imara kuhimili masafa marefu akitolea mfano
gari ya Volkswagen aliyosafiri nayo dereva kutoka nchini Ujerumani
Rainer Zietlof.
Dereva kutoka nchini Ujerumani Rainer Zietlof akioyesha cheti cha rekodi ya dunia mbele ya wanahabari
Dereva toka nchini Ujerumani Rainer Zietlof akitoa maelekezo ya gari yake aina ya Volkswagen Touareg V6 TDI
Dereva
toka nchini Ujerumani Rainer Zietlof akitoa maelekezo ya injini ya
gari yake aina ya Volkswagen Touareg V6 TDI aliyosafiri nayo kwenye nchi
zaidi ya 19 Duniani.
Dereva
toka nchini Ujerumani Rainer Zietlof akitoa maelekezo ya bodi ya gari
yake aina ya Volkswagen Touareg V6 TDI aliyosafiri nayo kwenye nchi
zaidi ya 19 Duniani.
Dereva
Toka Nchini Ujerumani Rainer Zietlof akitoa maelekezo ya sehemu ya
kuweka vifaa vya akiba kwenye gari yake aina ya Volkswagen Touareg V6
TDI
Dereva Toka Nchini Ujerumani Rainer Zietlof akiendelea kutoa maelekezo ya Gari yake hiyo aina ya Volkswagen Touareg V6 TDI
Gari aina ya Volkswagen Touareg V6 TDI inavyoonekana kwa ndani.
Dereva
kutoka nchini Ujerumani Rainer Zietlof akiwa na Mkurugenzi Mtendaji wa
kampuni ya CFAO Motors, Bw.Wayne McIntosh (wa pili toka kulia)
wakipata picha ya pamoja na wanahabari.
Mkurugenzi
Mtendaji wa kampuni ya CFAO Motors, Bw.Wayne McIntosh (kushoto)
akipata picha na Dereva toka nchini Ujerumani Rainer Zietlof
Meneja Masoko wa CFAO Motors Ltd. Tharaia Ahmed(kushoto) akipata picha na Dereva Rainer Zietlof.
Mkurugenzi
Mtendaji wa kampuni ya CFAO Motors, Bw.Wayne McIntosh akisoma cheti
cha rekodi ya dunia alichopewa dereva toka Ujerumani.
No comments:
Post a Comment