Pages

BRAND NEW MUSIC

metty magese

metty magese

Listen & Download

http://mdundo.com/a/32626

Thursday, May 9, 2013

ALIBINO AFUKUZWA SHULE KWA MADAI NI MCHAWI JIJINI MBEYA


.

KATIKA Hali isiyokuwa ya Kawaida Uongozi wa Shule ya Sekondari Hollwood iliyoko Mlowo Wilayani Mbozi Mkoa wa Mbeya imemsimamisha shule Mwanafunzi wa kidato cha tatu kwa takribani Miezi Miwili kwa madai kuwa anajihusisha na imani za Kishirikina.
  
Mwanafunzi huyo aliyejulikana kwa jina la Amina Mwankinga(20) ambaye ni mlemavu wa ngozi(Albino) alisimamishwa shule na uongozi wa Shule hiyo tangu Machi 9, Mwaka huu baada ya uongozi wa Shule hiyo kupata taarifa kutoka kwa Wanafunzi wakimtuhumu Mwenzao huyo kuwa ni Mshirikina.
  
Uongozi wa Shule hiyo baada ya kupata taarifa hizo ulimwamuru mhanga wa tukio hilo kuondoka Shuleni hapo pasipo kufuatilia na kujua ukweli wa jambo hilo na kupata udhibiti hivyo kumwacha Mwanafunzi huyo akizurura mitaani asijue hatma ya maisha yake.
  
Mhanga wa tukio hilo Amina Mwankinga alisema tangu tarehe tisa alipofukuzwa bwenini na wanafunzi wenzie wakitaka aondoke shuleni hapo majira ya usiku hali iliyomlazimu kuomba hifadhi kwa mlinzi aliyemkubalia na kukesha naye hadi asubuhi  hali iliyopelekea kupigwa na baridi kali kutokana na kukosa nguo za kujisitiri kama Shuka nk.

Anasema kutokana na hali hiyo Walimu pamoja na uongozi wa Shule hiyo haukuchukua hatua yoyote jambo lililomlazimu kuondoka Shuleni hapo  baada ya kukosa msaada ambapo alirejea Jijini Mbeya anakoishi na Binamu yake.
  
Binti huyo anayesomeshwa na Shirika la Under the SameSun  iliyoko Jijini Dar Es Salaam aliwaambia waandishi wa habari kuhusu mkasa uliompata huku akiomba msaada kwa wasamaria wema kumtafutia Shule ili aendelee na masomo kwa ajili ya kujiandaa na mtihani wa kidato cha nne Mwakani.
  
Kwa upande wake Mkuu wa Shule ya HollyWood Ambukeghe Mtafya, alipopigiwa simu kuhusu tuhumahizo alikiri kulijua suala hilo na kwamba walimrudisha mwanafunzi huyo nyumbani ili kumnusuru na kipigo kutoka kwa wanafunzi wenzie na kuongeza kuwa aliambiwa atafute shule nyingine ili ahamie.
  
Naye katibu wa Chama cha Albino Mkoa wa Mbeya, Wiliamu Simwale  alisema alikuwa  halijui suala hilo na kwamba kama lingekuwa suala liko nyeti angejulishwa yeye juu ya hatua zilizofikiwa ambapo Uongozi wa Shule umeendelea kupokea fedha za malipo ya Mwanafunzi pasipo kutoa taarifa kwenye shirika linalolipa.

No comments: