Pages

BRAND NEW MUSIC

metty magese

metty magese

Listen & Download

http://mdundo.com/a/32626

Friday, May 10, 2013

YALIOJILI MISS SHINYANGA 3013

Katikati ni Redds Miss Shinyanga 2012/2013 Maiya Mohamed, akiwa katika furaha mara baada ya kutangazwa kuwa mshindi katika  shindano la kumsaka mrembo wa mkoa wa Shinyanga lililofanyika Usiku wa kuamkia Jumapili katika uwanja wa Halmashauri mjini Kahama. Kulia kwake ni Mshindi wa Pili Sylvia Joseph na kushoto kwake ni Mshindi wa tatu Happyness Joseph.
Huyu ndiye Maiya Mohamed, Redds Miss Shinyanga 2012/2013
Kutoka kushoto ni Happyness Boniface akishika nafasi ya tatu, katika ni mshindi wa kwanza Maiya Mohamed na kulia ni Sylvia Joseph mara baada ya kutangazwa kuwa washindi wa Miss Shinyanga 2012/13
Redds Miss Shinyanga 2012/13 Maiya Mohamed akivishwa taji mara baada ya kuatngwazwa kuwa mshindi
Malkia wa mipashoTanzania Bi. Khadija Kopa akiwa jukwaani
Khadija Kopa, akiwajibika jukwaani katika shindano la Miss Shinyanga 2012/13 katika uwanja wa Halmashauri mjini Kahama
Robert kutoka TBL, mdhamini mkuu wa Miss Shinyanga 2012/13 akitoa neno la shukrani
Majaji wakikagua matokeo kabla ya kutangazwa mshindi
Mrembo Maiya Mohamed akiulizwa swali na MC wa shughuli Masanja Mkandamizaji kutoka kundi la Orijino Komedi
DJ Rammy akisababisha vilivyo
Mrembo Happyness Boniface katika vazi la Usiku la kutokea
Mrembo Sylvia Joseph katika pozz, vazi la Usiku
Mrembo Diana Dickson katika Pozz, vazi la Usiku
Tano bora ya Miss Shinyanga 2012/13
Mrembo Maiya Mohammed katika Pozz, vazi la Usiku
Chegge na Temba walisababisha vilivyo
Pendo na Happy ni warembo kutoka wilaya ya Nyamagana Mwanza, nao walikuwepo kushuhudia shindano la Miss Shinyanga 2012/13
Kumi Bora ya Miss Shinyanga 2012/13
MC wa shughuli ni Masanja Mkandamizaji wa Orijino Komedi
Warembo wakipita na vazi Ufukweni
Vazi la Ufukweni
Washiriki wa Miss Shinyanga 2012/13 katika vazi la Usiku
Asela Magaka muandaaji wa Miss Shinyanga 2012/2013, akiwa pamoja na Malkia wa mipasho Tanzania Bi. Khadija Kopa
Hawa ni washindi wa Mkoa wa Mara, nao walikuwepo kushuhudia shindano hilo

LADY JAYDEE MATATIZONI TENA

165976_10151281153065025_1521636074_n
Bado joto ya show ya mika 13 ya Lady JayDee inazidi kupanda kutokana na mengi yanayohofiwa kutokea siku hiyo. Kwanza kulikuwa na tetesi kuwa huenda Clouds Fm wakafanya show nyingine siku hiyo, kitu ambacho Ruge Mutahaba alikifafanua vizuri kwa kusema mtu ukiwa na shughuli haimaanishi kuwa wengine wasifanye shughuli nyingine kama hiyo.
Lakini sasa kuna jingine ambalo limejitokeza, na amelisema mwenyewe Lady JayDee, hii haijathibishwa, huenda ni maneno tu ya kizushi or??.. Na hivi ndivyo alivyoandika kupitia ukurasa wake wa twitter muda mchache uliopita…
ji

Thursday, May 9, 2013


MWANAUME aliyefahamika kwa jina la baba Salome, mkazi wa Tandika jijini Dar es Salaam, hivi karibuni alimdhalilisha mkewe (mama Salome) baada ya kufumaniwa gesti akiwa na mwanaume mwenzake ambapo madai yalisema, walikuwa katika hatua za mwisho za kuingiliana kimwili...
 
Aibu hiyo ya mwaka ambayo ilionekana pia kama kituko ilijiri Mei 3, mwaka huu ndani ya gesti moja maarufu iliyopo Devi’s Corner –Tandika, jijini Dar es Salaam. Awali ilidaiwa kuwa, mwanaume huyo na baba Salome mwenye mke na watoto wawili wanaomtegemea kwa kila kitu, walionekana wakiingia kwenye gesti moja ambayo pia ipo maeneo hayo hali iliyozua maswali kwa watu waliokuwa wakiwafahamu. 
 
“Unajua tatizo lilianzia wapi? Baba Salome na yule mwanaume mwenzake walionekana wakiingia gesti moja kisha wakatoka, wakaingia nyingine pia wakatoka, ndipo watu wanaowafahamu wakajiuliza kulikoni wawili hao kutembelea gesti siku hiyo, wakawafuatilia,” alisema mnyetishaji mmoja. 
Akaendelea: Lakini watu waliwafahamu kwa namna mbili tofauti, baba Salome ni mtulivu, mwadilifu, mwenzake watu wanasema ana ‘katabia’ ka kutaka kuwa faragha na  wanaume wenzake bila kujulikana nini anakitaka katika usiri huo. 
 Madai zaidi yakawekwa wazi kwamba, baadhi ya watu walikwenda kwenye gesti walizokwenda wawili hao na kuulizia nini walikuwa wanakitaka, ndipo siri ikawekwa wazi kwamba wanatafuta chumba cha kupumzika kwa siku hiyo lakini kwa sheria za Jiji la Dar es Salaam (kama siyo za nchi nzima), wanaume wawili hawaruhusiwi kulala chumba kimoja.
  
Chanzo kikasema: Wambeya wakawaona wakiingia kwenye gesti ya tukio, wakapewa chumba. Ndipo wakakimbia nyumbani kwa baba Salome na kumtonya mkewe, mama Salome kwamba mumewe ameingia gesti. 

Kichekesho zaidi kinaangushwa kwamba, baada ya kuambiwa mumewe amezama gesti, mama Salome ambaye ndiyo kwanza alikuwa amefika kutoka  kwenye mikopo ya Finca, alitoka mbio huku akisema anakwenda kumtoa sikio la kulia Kidawa akiamini mumewe ameingia gesti na mwanamke huyo. “Watu walimwambia mumewe hakuingia gesti na Kidawa bali mwanaume mwenzake. Kwanza mama Salome aliomba asitaniwe juu ya hilo, lakini akasisitiziwa,” alisema mtoa habari huyo. 
Akizungumza kwa jazba na waandishi wetu nje ya gesti hiyo, mama Salome alisema kwamba alipata taarifa siku nyingi mumewe ana ukaribu na mwanaume huyo ambaye mitaani watu wanasema  anajihusisha na vitendo vya ushoga. 
 
“Nilipozipata taarifa hizi sikuziamini, nilidhani ni Kidawa ndiyo kaingia gesti na mume wangu, maana Kidawa ndiye mbaya wangu,” alisema mwanamke huyo kisha akazama ndani ya gesti akiwa na polisi ambao haikujulikana walikotokea. 
Huku mumewe na mwanaume mwenzake wakiwa hawana hili wala lile kule chumbani, mlango ulisukumwa na kufunguka ambapo mwanamke huyo aliwakuta wawili hao wakiwa wameshavua baadhi ya nguo. 
Wote walishtuka kuona wameingiliwa!  “Yaani roho inauma sana, sijui ni kitu gani umekosa kwangu mpaka unakuja kwa mwanaume mwenzako jamani baba Salome,” alisema huku akilia mama Salome. 
Baada ya kugundua wamenaswa, mwanamke aliyekuwa na baba Salome aliangua kilio huku  akiomba kusamehewa kwa vile yeye ni mume wa mtu, lakini kilio chake hakikusikika kwa polisi ambapo waliwafunga pingu na kuwataka kuelekea katika kituo cha polisi. 
Wakati wakitoa maelezo kwenye kituo cha polisi, mwanaume aliyekuwa na baba Salome alijitambulisha kwa jina la  Julius Mwita, mkazi wa Devi’s Corner ana  mke na watoto wawili na aliwaomba sana waandishi wamhifadhi kwani wakwe zake wakimuona ‘itakula  kwake’. 

ALIBINO AFUKUZWA SHULE KWA MADAI NI MCHAWI JIJINI MBEYA


.

KATIKA Hali isiyokuwa ya Kawaida Uongozi wa Shule ya Sekondari Hollwood iliyoko Mlowo Wilayani Mbozi Mkoa wa Mbeya imemsimamisha shule Mwanafunzi wa kidato cha tatu kwa takribani Miezi Miwili kwa madai kuwa anajihusisha na imani za Kishirikina.
  
Mwanafunzi huyo aliyejulikana kwa jina la Amina Mwankinga(20) ambaye ni mlemavu wa ngozi(Albino) alisimamishwa shule na uongozi wa Shule hiyo tangu Machi 9, Mwaka huu baada ya uongozi wa Shule hiyo kupata taarifa kutoka kwa Wanafunzi wakimtuhumu Mwenzao huyo kuwa ni Mshirikina.
  
Uongozi wa Shule hiyo baada ya kupata taarifa hizo ulimwamuru mhanga wa tukio hilo kuondoka Shuleni hapo pasipo kufuatilia na kujua ukweli wa jambo hilo na kupata udhibiti hivyo kumwacha Mwanafunzi huyo akizurura mitaani asijue hatma ya maisha yake.
  
Mhanga wa tukio hilo Amina Mwankinga alisema tangu tarehe tisa alipofukuzwa bwenini na wanafunzi wenzie wakitaka aondoke shuleni hapo majira ya usiku hali iliyomlazimu kuomba hifadhi kwa mlinzi aliyemkubalia na kukesha naye hadi asubuhi  hali iliyopelekea kupigwa na baridi kali kutokana na kukosa nguo za kujisitiri kama Shuka nk.

Anasema kutokana na hali hiyo Walimu pamoja na uongozi wa Shule hiyo haukuchukua hatua yoyote jambo lililomlazimu kuondoka Shuleni hapo  baada ya kukosa msaada ambapo alirejea Jijini Mbeya anakoishi na Binamu yake.
  
Binti huyo anayesomeshwa na Shirika la Under the SameSun  iliyoko Jijini Dar Es Salaam aliwaambia waandishi wa habari kuhusu mkasa uliompata huku akiomba msaada kwa wasamaria wema kumtafutia Shule ili aendelee na masomo kwa ajili ya kujiandaa na mtihani wa kidato cha nne Mwakani.
  
Kwa upande wake Mkuu wa Shule ya HollyWood Ambukeghe Mtafya, alipopigiwa simu kuhusu tuhumahizo alikiri kulijua suala hilo na kwamba walimrudisha mwanafunzi huyo nyumbani ili kumnusuru na kipigo kutoka kwa wanafunzi wenzie na kuongeza kuwa aliambiwa atafute shule nyingine ili ahamie.
  
Naye katibu wa Chama cha Albino Mkoa wa Mbeya, Wiliamu Simwale  alisema alikuwa  halijui suala hilo na kwamba kama lingekuwa suala liko nyeti angejulishwa yeye juu ya hatua zilizofikiwa ambapo Uongozi wa Shule umeendelea kupokea fedha za malipo ya Mwanafunzi pasipo kutoa taarifa kwenye shirika linalolipa.

Monday, May 6, 2013

BLOGGERS TULIVYOJIACHIA NA TIGO NEW AFRICA HOTEL

Baadhi ya wamiliki wa Mitandao ya Kijamii (BLOGGERS), wakishindana kucheza muziki kuwania Ipad na simu wakati wa hafla waliyoandaliwa na Kampuni ya Tigo jana kwenye Hoteli ya New Africa, Dar es Salaam.
Mmiliki wa Kajuna Blog, akikabidhiwa zawadi ya IPAD, na Ofisa wa Biashara  na masoko wa Tigo, Gaudance Mushi (kulia)  baada ya kuwa mshindi wa kwanza wa kucheza muziki katika hafla hiyo.
Blogger mwanamke aliyeshinda kucheza muziki akipatiwa zawadi ya Ipad mpya
Mablogger wanawake wakishindana kucheza muziki katika hafla hiyo
Mmiliki wa Blogu ya Kamanda wa Matukio, Kamanda Richard Mwaikenda (aliyevaa shati la drafti kushoto) akiwa na mabloga wenzake wakishuhudia mpambano huo
 Mablogger, Kutoka kushoto ni Adam Mzee (CCM Blog), William Malecela (Wananchi Blog) na John Bukuku wa Fullshangwe Blog wakiwa na furaha wakati wa hafla hiyo.
 Mhariri wa gazeti la Michezo la StaaSpoti, Julius Kihampa (kushoto) akiwa na John Kitime (katikati) pamoja na
 Mmiliki wa Blog ya Habari Mseto, Francis Dande (katikati) akiwa na mablogger wengine.
 Mablogger wakibadilishana mawazo pamoja na maofisa wa Tigo
 Tanzanite Band ikitumbuiza katika hafla hiyo ya kukata na shoka
 Mablogger wakisikiliza wakati mtoa mada Raymond Maganga akielezea jinsi ya kuboresha Blog kibiashara
 Boss wa kampuni ya DeSiaMore I.T & Arts, Raymond Maganga (kushoto), akitoa mada ya jinsi ya kuboresha Blog.
Boss wa kampuni ya DeSiaMore I.T & Arts, Raymond Maganga (kushoto) na Emmanuel Feruz ambaye ni Google Student Ambassador wa IFM, wakifurahia jambo wakati wa hafla hiyo.
                                    Akina dada mablogger wakishindana kucheza muziki


 Blogger wa kike akipatiwa zawadi ya simu baada ya kuwa mshindi wa pili
Mablogger wanaume wakishindana vikali kucheza muziki kuwania zawadi za IPAD na Simu

Sunday, May 5, 2013

NANCY MOSHI NDIYE REDD'S MISS ARUSHA CITY CENTRE 2013


Redd’S Miss Arusha City Centre 2013, Nancy Moshi akipunga mkono mara baada ya kutawazwa mshindi wa Taji hilo katika shindano lililofanyika Usiku wa kuamkia jana jijini Arusha. Nancy aliwashinda warembo wenzake 10 waliokuwa wakiwania nae taji hilo.

Redd’S Miss Arusha City Centre 2013, Nancy Moshi (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na mshindi wa pili Glory Steven (kushoto) na mshindi wa tatu Neema Kessy mara baada ya warembo hao kutangazwa kuwa ndio washindi wa shindano hilo lililofanyika usiku wa kuamkia jana jijini Arusha.

Warembo wanaliokuwa wakiwania taji la Redd’s Miss Arusha City Centre 2013 wakicheza show ya ufunguzi wa shindano hilo jijini Arusha usiku wa Kuamkia leo.
 Wadau mbalimbali wa sanaa ya Urembo mjini Arusha wakifuatilia Onesho hilo la Redd's Miss Arusha 2013.
Mwandaaji wa shindano hilo Bi Upendo (kulia) na rafiki yake.
 Warembo walimfanyia tukio la kipekee Mwandaaji wao kwa Keki ya Birthday, na hapa Upendo akizima mishumaa hiyo...
 Warembo wa tano kati ya 11 waliokuwa wanawania taji la Redd’s Miss Arusha City Centre 2013 wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kutangwaza kufuzu hatua hiyo. Kutoka kushoto ni Minael Anderson, Neema Joel, Nancy Moshi, Neema Kessy na Glory Steven.
Mwana dada Rachel ndiye aliyekuwa msanii kinara wa show hiyo na hapa akicheza na mashabiki wake.

Friday, May 3, 2013

REDD'S MISS KIBAHA WAENDELEA KUJIFUA

Mkufunzi wa Warembo wa Miss Kibaha Rehema Uzuwiya akizungumza na warembo hawo wakati wa mazoezi yao yanayo endelea katika ukumbi wa Vijana Kinondoni 
Warembo wa miss kibaha wakiwa katika pozi wakati wa mazoezi yao
Warembo watakao wania taji la Miss Kibaha wakiwa katika pozi wakati wa mazoezi yao yanayoendelea katika ukumbi wa vijana Kinondoni Dar es salaam. Picha