Pages

BRAND NEW MUSIC

metty magese

metty magese

Listen & Download

http://mdundo.com/a/32626

Thursday, September 29, 2011

MBUNGE WA CCM TUMBO JOTO

  Wachambuzi wa mambo ya kisiasa wanasema kuwa mbunge wa mtera(ccm) Mh. Livingsote Lusinde atakuwa na wakati mgumu kutekeleza ahadi yake ya kunywa sumu endapo CCM itashindwa katika uchaguzi mdogo wa Jimbo la Igunga.
   Lusinde ambaye anambipu mungu kwa kutoa ahadi ya kunywa sumu akiwa na maana ya kujiua endapo CCM itashindwa uchaguzi huo unaofanyika jumapili hii.Ahadi hii aliitoa wakati anamnadi Peter Kafumu(mgombea ubunge jimbo la Igunga) kijiji cha Ugaka kata ya Nkinga.
   Mbunge huyo mfia chama amefanya watu wasubiri matokeo kwa hamu ili tuone kama kweli atakunywa sumu ama laa,angali hali ya nani atashinda ishaanza kujitokeza waiwazi.
   Wadodosaji wa habari za kichokonozi wanasema Lusinde amekata tamaa kwani kitendo cha kudiliki kunywa sumu ni hali ya kushindwa kuhimili kitu,mwanajeshi anafia vitani mwanajeshi ajiui,Lusinde vipi mbona unatuangusha....?.
   Kama mbunge utajiua kwa matokeo mabovu je wananchi wa jimboni kwako wanaolala na njaa wanyweshe familia zao sumu kwa kushindwa kumudu milo mitatu na mahitaji ya kila siku?...Hatuombi CCM kushindwa ila kama itashindwa tafadhali Mh.Lusinde tuite na waandishi wa habari tupate picha unapokunywa kikombe cha kwanza...cha pili...cha tatu.... mpaka unapokata roho...utakuwa umekufa kishujaa kwa kutekeleza ahadi yako mwenyewe.....aaaah Lusindeee..


MASHINDANO YA HELKOPTA IUGUNGA

Helikopta iliyokodishwa na CHADEMA                   Helikopta iliyokodishwa na CCM   helkopta iliyokodishwa na CUF.
 
          
MIAKA 50 YA UHURU WA TANZANIA
      Halisi ya upatikanaji maji ni mgumu katika kata ya Kibirizi Bukoba vijijini ambapo wakazi takribani 6325 wanakabiliwa na uhaba wa maji katika kata nzima hawana kisima hata kimoja,Upatikanaji wa maji ni mpaka kipindi cha mvua,ambapo huchmbwa madimbwi katika miteremko ili yatunze maji,maji hayo ndio hutumika kwa matumizi ya nyumbani na mifugo.

     Katika kipindi cha Kiangazi wananchi wa maeneo hayo hulazimika kutembea urefu wa Km 16-32 katika eneo la Lake Ikimba au Rugaze Izimbya au katika Runch iliyoko Kibirizi...Hivi huku mbunge yupo kweli au anahudhuria tu vikao bungeni?

No comments: