Mashindano ya Miss East Africa mwaka huu yataonyeshwa LIVE kupitia Mnet ambapo yanatarajiwa kutuizamwa na watu wanaokadiliwa kufikia million 200 kupitia televison na kwa njia ya internet Dunia nzima.
Aidha maandalizi ya mashindano hayo yanaendelea kwa kasi ambapo yamepangwa kufanyika tarehe 07 December, 2012 katika ukumbi wa Mlimani City, jijini Dare s salaam, Tanzania badala ya mwezi September kama ilivyokuwa imetangazwa awali ili kutoa muda zaidi kwa Nchi ambazo hazijapata wawakilishi wao kuweza kukamilisha zoezi hilo.
Mashindano ya Miss East Africa mwaka huu yanatarajiwa kuwa na mvuto wa aina yake ambapo yatashirikisha warembo kutoka katika Nchi 16 za ukanda wa afrika mashariki.
Nchi zilizothibitisha kushiriki mashindano hayo ni wenyeji Tanzania, Kenya, Uganda, Rwanda na Burundi. Nchi zingine zilizoalikwa kushiriki ni pamoja na Ethiopia, Eritrea, Somalia, Djibouti, Southern Sudan, Malawi, pamoja na visiwa vya Seychelles, Madagascar, Reunion, Comoros, na Mauritius.
Mashindano ya Miss East Africa yanalenga kukuza ushirikiano na kutangaza utamaduni wa Afrika mashariki, pamoja na kutangaza utalii wa Tanzania kama Nchi wenyeji wa mashindano hayo makubwa katika ukanda huu wa Afrika.
Tayari baadhi ya Nchi zinazoshiriki mashindano hayo zimeshatangaza wawakilishi wake ambazo ni Eritrea, Ethiopia, Uganda, Southern Sudan, Malawi na Seychelles. Nchi zilizosalia zinatarajiwa kutangaza wawakilishi wao kabla ya tarehe ya mwisho ambayo ni tarehe 28 mwezi September. Mashindano ya Miss East Africa yanamilikiwa na kuandaliwa na kampuni ya Rena Events Ltd ya jijini Dar es salaam,.