Miss
Morogoro 2012 Joyce Baluhi katikati akiwa na washindi wenzake, Salvina
Kibona mshindi wa pili kushoto na Irene Thomas mshindi wa tatu.
Warembo hawa ni miomngoni mwa wanaoingia Kamoni hii leo.
*******
JUMLA
ya warembo 14 wanaotaraji kuwania taji la Miss Redd's Kanda ya
Mashariki 2012 Wanataraji kuiongia kambini mjini Morogoro jioni ya leo
tayari kwa maandalizi ya shindano hilo.
Shindano
la Redds Miss Kanda ya Mashariki 2012 linataraji kufanyika Septemba 1,
2012 katika Hoteli ya Kisasa ya Nashera iliyopo mjini Morogoro.
Aidha wanyange hao walichelewa kunza kambi yao kupisha warembo hao kuhesabiwa makwao kabla ya kuingia kambini.
Akizungumza
na Father Kidevu Blog, mratibu wa shindano hilo Alexander Nikitas
alisema warembo hao pia walishiriki kuhamasisha zoezi la sensa katika
maeneo mbalimbali wanayotoka Huku wale wa Mkoa wa Morogoro wakihamasisha
mjini hapo watu kushiriki kuhesabiwa.
Kanda
ya Mashariki inaundwa mna mikoa mine katika shindano hilo dogo la Miss
Tanzania 2012 ambayo ni mikoa ya Morogoro, Lindi, Mtwara na Pwani.
Nikitas
aliwataja washiriki watakao ripoti kambini katika Lodge ya Usambara
Safari Resort iliyopo nane nan mkoani Morogoro kuwa ni Zuhura Gora,Alice
Adam na Shakila Hassan kutoka Mtwara.
Wengine
mikoa yao kwenye mabano ni Maria Peter,Irene Mweleko na Rose
Lucas(Pwani) Irene Veda,Stella Bartazary na Darina Athumani(Lindi)
na kutoka Morogoro ni pamoja na Salvana Kibano,Joyce George,Irene
Thomas,Betina Msofe,na Nafia waziri.
Taji
la Miss Kanda ya Mashariki linashikiliwa na Loveness Flavian ambaye
pia ni Miss Sport Woman wa Miss Tanzania 2011. Warembo hao watakuwa
chini ya Mwalimu Asha Salehe Miss Eastern Zone namba tatu.
Kwa
mujibu wa Nikitas wadhamini wa shindano hilo Mbunge wa Kilosa Mustafa
Mkulo,Redd's, Dodoma wine, Father Kidevu Blog, Auckland Travel Safairi
Tour, Clouds Fm, Usambara Safari Lodge, Chilakale Resort, Endepa Event
Planner, Jambo Leo, Kitwe General Traders na Simple Easy Car Renta
No comments:
Post a Comment