
Mwandishi wa habari hizi alifika kwenye msiba huo maeneo ya Kinondoni, na kukutana kuna umati mkubwa wa watu ambao walifulika kumpa pole msanii huyo ambaye ni kipenzi cha watu.
Hata hivyo mwandishi wa habari hizi, alizungumza na Madaha ingawa hakuweza kuzungumza sana zaidi ya kutokwa machozi huku akisema kuwa amempoteza mama yake kipenzi ambaye alikuwa akimsapoti kwenye vitu vingi ndani ya maisha yake.
“Naumia sana lakini najua yote ni mipango ya Mungu kwani kila kitu kimepangwa, hivyo tunamuombea mama yetu aweze kwenda salama mbele za haki kwani sote hiyo ndiyo njia yetu,” alisema kwa maskitiko makubwa sana.
No comments:
Post a Comment