Pages

BRAND NEW MUSIC

metty magese

metty magese

Listen & Download

http://mdundo.com/a/32626

Tuesday, October 23, 2012

MSHINDI MISS TANZANIA KUONDOKA NA GARI

 
Kampuni ya TBL kupitia kinywaji chake cha Redds Original ambao ndio Mdhamini mkuu wa shindano la Redds Miss Tanzania 2012, leo tunatangaza zawadi kwa washiriki wote wanaowania taji la Redds Miss Tanzania 2012.

Akizungumza na waandishi wa Habari Jijini Dar Es Salaam Mkurugenzi wa kampuni ya LINO AGENCY Hashim Lundenga alisema katika fainali za shindano la Redds Miss Tanzania 2012 zitafanyika tarehe 3 Novemba 2012 katika ukumbi wa Blue Pearl Hotel,  (Ubungo Plaza) jijini Dar es salaam ambapo ni shindano linaloshirikisha washiriki 30 kutoka mikoa mbalimbali ya Tanzania.

Leo hii tunapenda kuchukua nafasi hii kuwatangazia rasmi kuwa katika fainali ya Redds Miss Tanzania mwaka zawadi zitakuwa kama ifuatavyo

Mshindi wa Kwanza atapata zawadi ya pesa taslimu shs: 8,000,000/- pamoja na gari
Mshindi wa pili atapata zawadi ya pesa taslimu shs: 6,200,000/-
Mshindi wa tatu atapata zawadi ya pesa taslmu shs: 4,000,000/-
Mshindi wa nne atapata zawadi ya pesa taslimu shs; 3,000,000/-
Mshindi wa tano atapata zawadi ya pesa taslimu shs: 2,400,000/-
Mshindi wa sita hadi wa 15 kila mmoja atapata shs: 1,200,000/-
Washiriki wengine wote waliobaki kila mmoja atalipwa shs: 700,000/-
Katika shindano hilo ambalo ndani yake kuna mashindano mengine madogo [Fast Tract] tayari washiriki 3 wameshajipatia tiketi ya kuingia katika [Top 15 Finalist]

Washiriki hao ni  Lucy Stephano – Miss Photogenic
                          Magdalena Roy – Top Model
                          Mary Chizi – Top Sport Woman

Shindano dogo lingine limepangwa kufanyika siku ya Ijumaa tarehe 26 Oktoba 2012 la kumtafuta mrembo wenye Kipaji. Miss Talent.

Na tarehe 28 Oktoba 2012 atapatikana Miss Personality.
Nae Meneja wa kinywaji cha Redds Original Bi Victoria Kimaro amesema huu ni wakati sahihi wa kumpata mshindi biomba mwenye vigezo sahihi hivyo kuwataka wapenzi wote wa tasnia ya urembo na wapenda maendeleo kote nchini kujianda kupata tiketi za kushudia fainali hiyo mapema ili kuweza kupata fursa ya kupata burudani mbalimbali.Kwa kweli shindano la mwaka huu tunatarajia kuwa litafana sana hasa kwa kuzingatia kuwa maandalizi yote yameshakamilika kwa kiwango kikubwa na sisi kama wadhamini wakuu tunahakikisha kuwa mwaka huu kila atakaefika kwenye ukumbi wa Ubungo Plaza atakuwa na jambo la kusimulia kwa sababu ni shindano la kipekee.
Baadhi ya warembo wanaowania taji hilo la Redds Miss Tanzania 2012 wakiwa ukumbini hapo wakisikiliza kutangazwa kwa zawadi yao.

No comments: