Pages

BRAND NEW MUSIC

metty magese

metty magese

Listen & Download

http://mdundo.com/a/32626

Thursday, August 30, 2012

MISS EAST AFRICA KURUKA LIVE












Mashindano ya Miss East Africa mwaka huu yataonyeshwa LIVE kupitia Mnet ambapo yanatarajiwa kutuizamwa na watu wanaokadiliwa kufikia million 200 kupitia televison na kwa njia ya internet Dunia nzima.

Aidha maandalizi ya mashindano hayo yanaendelea kwa kasi ambapo yamepangwa kufanyika tarehe 07 December, 2012 katika ukumbi wa Mlimani City,  jijini Dare s salaam, Tanzania badala ya mwezi September kama ilivyokuwa imetangazwa awali ili kutoa muda zaidi kwa Nchi ambazo hazijapata wawakilishi wao kuweza kukamilisha zoezi hilo.

Mashindano ya Miss East Africa mwaka huu yanatarajiwa kuwa na mvuto wa aina yake ambapo yatashirikisha warembo kutoka katika Nchi 16 za ukanda wa afrika mashariki.

Nchi zilizothibitisha kushiriki mashindano hayo ni wenyeji Tanzania, Kenya, Uganda, Rwanda na Burundi. Nchi zingine zilizoalikwa kushiriki ni pamoja na Ethiopia, Eritrea, Somalia, Djibouti, Southern Sudan, Malawi, pamoja na visiwa vya Seychelles, Madagascar, Reunion, Comoros, na Mauritius.

Mashindano ya Miss East Africa yanalenga kukuza ushirikiano na kutangaza utamaduni wa Afrika mashariki, pamoja na kutangaza utalii wa Tanzania kama Nchi wenyeji wa mashindano hayo makubwa katika ukanda huu wa Afrika.

Tayari baadhi ya Nchi zinazoshiriki mashindano hayo zimeshatangaza wawakilishi wake ambazo ni Eritrea, Ethiopia, Uganda, Southern Sudan, Malawi na Seychelles. Nchi zilizosalia zinatarajiwa kutangaza wawakilishi wao kabla ya tarehe ya mwisho ambayo ni tarehe 28 mwezi September. Mashindano ya Miss East Africa yanamilikiwa na kuandaliwa na kampuni ya Rena Events Ltd ya jijini Dar es salaam,.

Monday, August 27, 2012

Warembo Redds Miss Kanda ya mashsriki kuingia kambini leo

Miss Morogoro 2012 Joyce Baluhi katikati akiwa na washindi wenzake, Salvina Kibona mshindi wa pili kushoto na Irene Thomas mshindi wa tatu. Warembo hawa ni miomngoni mwa wanaoingia Kamoni hii leo.
*******
JUMLA ya warembo 14 wanaotaraji kuwania taji la Miss Redd's Kanda ya Mashariki 2012 Wanataraji kuiongia kambini mjini Morogoro jioni ya leo tayari kwa maandalizi ya shindano hilo.
Shindano la Redds Miss Kanda ya Mashariki 2012 linataraji kufanyika Septemba 1, 2012 katika Hoteli ya Kisasa ya Nashera iliyopo mjini Morogoro.
Aidha wanyange hao walichelewa kunza kambi yao kupisha warembo hao kuhesabiwa makwao kabla ya kuingia kambini.
Akizungumza na Father Kidevu Blog, mratibu wa shindano hilo Alexander Nikitas alisema warembo hao pia walishiriki kuhamasisha zoezi la sensa katika maeneo mbalimbali wanayotoka Huku wale wa Mkoa wa Morogoro wakihamasisha mjini hapo watu kushiriki kuhesabiwa.
Kanda ya Mashariki inaundwa mna mikoa mine katika shindano hilo dogo la Miss Tanzania 2012 ambayo ni mikoa ya Morogoro, Lindi, Mtwara na Pwani.
Nikitas aliwataja washiriki watakao ripoti kambini katika Lodge ya Usambara Safari Resort iliyopo nane nan mkoani Morogoro kuwa ni Zuhura Gora,Alice Adam na Shakila Hassan kutoka Mtwara.
Wengine mikoa yao kwenye mabano ni Maria Peter,Irene Mweleko na Rose Lucas(Pwani) Irene Veda,Stella Bartazary na Darina Athumani(Lindi) na kutoka Morogoro ni pamoja na Salvana Kibano,Joyce George,Irene Thomas,Betina Msofe,na Nafia waziri.
Taji la Miss Kanda ya Mashariki linashikiliwa na Loveness Flavian ambaye pia ni Miss Sport Woman wa Miss Tanzania 2011. Warembo hao watakuwa chini ya Mwalimu Asha Salehe Miss Eastern Zone namba tatu. 
Kwa mujibu wa Nikitas wadhamini wa shindano hilo Mbunge wa Kilosa Mustafa Mkulo,Redd's, Dodoma wine, Father Kidevu Blog, Auckland Travel Safairi Tour, Clouds Fm, Usambara Safari Lodge, Chilakale Resort, Endepa Event Planner, Jambo Leo, Kitwe General Traders na Simple Easy Car Renta

Thursday, August 23, 2012

Kiongozi Mstaafu wa Freemasons Afrika Mashariki,Sir Andy Chande atinga clouds Media Group

Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Clouds Media Group,Joseph Kusaga akizungumza na Kiongozi Mstaafu wa Freemasons Afrika Mashariki,Sir Andy Chande ofisini kwake mapema leo mjengoni hapo,ambapo baadaye pia alifanya ziara fupi na kujionea vitengo mbalimbali vya kampuni hiyo namna ambavyo vinafanya kazi.
Mazungumzo yakiendelea ya hapa na pale.
Kiongozi Mstaafu wa Freemasons Afrika Mashariki,Sir Andy Chande akisikiliza jambo kwa umakini.
Mkurugenzi wa Clouds Media Group,Joseph Kusaga akiagana na wageni wake mara baada ya kufanya mazungumzo nao mapema leo,kwenye ofisi za kampuni hiyo,Mikocheni jijini Dar.
Mkurugenzi wa Clouds Media Group,Joseph Kusaga akiagana na mgeni wake Kiongozi Mstaafu wa Freemasons Afrika Mashariki,Sir Andy Chande.
Kiongozi Mstaafu wa Freemasons Afrika Mashariki,Sir Andy Chande akiondoka taratiibu mjengoni Clouds Media Group mapema leo mara baada ya kufanya ziara fupi kwenye ofisi hizo na kujionea mambo lukuki yanayofanywa na kampuni hiyo

Sunday, August 19, 2012

HUYU NDIO MISS WORLD 2012


Huyu ni Yu Wenxia (23) kutoka China ambae ndio ametangazwa mshindi katika Miss World 2012 ambapo hii inakua mara ya pili kwa China kushinda Miss World, mara ya kwanza ilikua 2007.
.


Alie mbele kushoto ndio Miss World 2012 namba mbili kutoka Wales, wa katikati ndio Miss World 2012 kutoka China na mshindi wa tatu alie kulia ni kutoka Australia.

.

.
Picha za chini zinazofata ni wakati wakiwa backstage.

.

Mamiss kutoka nchi mbalimbali.

Miss Lebanon.

Miss Hungary 2012 na Miss Slovania 2012.

Miss Cyprus 2012.

Miss Kazakstan.

Miss South Sudan.

Thursday, August 16, 2012

AMERICA'S FABULOUS FLOWER GIRLS ..GOOD JOB GIRLS

  The girls looked glamorous as the appeared on the David Letterman Show
If you thought they were loved at the London Olympic Games, the U.S. gymnastics teams is adored back on American soil. Gabby Douglas, McKayla Maroney, Jordyn Wieber, Kyla Ross, and Aly Raisman had a field day in new York on Tuesday, culminating in an appearance on the David Letterman Show. The team, dubbed the 'Fierce Five' were on the couch with Letterman discussing what sports they would like to compete in.

Relaxed: The team enjoyed a sit down after a day of touring the city
Relaxed: The team enjoyed a sit down after a day of touring the city on Tuesday

McKayla Maroney is impressed: As she joins the David Letterman Show Beaming: Jordyn Wieber couldn't stop smiling as she appeared on the David Letterman Show

The best five look glamorous as they appear on the David Letterman Show
As sweet as a rose: Gabby Douglas beams as she appears on the David Letterman Show         Blossoming: Aly Raisman looks glamorous as she appears on the David Letterman Show

Posing: The girls playfully bit their medals as they smiled for the cameras
They posed with their trophies round their necks, having brought home an impressive array of gold and silverware from the London Games. The girls playfully bit their medals and grinned for the cameras, posting the photographs online on Twitter.
Kitted out: Aly Raisman, Gabby Douglas, McKayla Maroney, Kyla Ross and Jordan Wieber posed with their medals on top of the Empire State Building

On top of the empire state building.. AMAZING!!!' Team captain Aly tweeted. 'This day keeps getting better and better! Having soooo much fun with the girls.' With beaming smiles they looked to be literally on top of the world, no doubt reliving their successes from the past two weeks.

Wednesday, August 15, 2012

WAZIRI MKUU PINDA ATOA CHANGAMOTO KWA WANAFUNZI KUWA NA NIDHAMU ILI WAFAULU...!

Waziri Mkuu Mizengo Pinda akitoa wosia kwa wanafunzi 20 waliofanya vizuri katika mitihani ya kidato cha sita kwa mwaka 2012 bungeni leo mjini Dodoma. Wanafunzi hao 10 wasichana na 10 wavulana wamepewa cheti , kopyuta ya pakato (laptop) na fedha taslimu shilingi laki mbili kwa kila mmoja.
 
Wanafunzi 20 waliofanya vizuri katika mitihani wa kidato cha sita kwa mwaka 2012 wakiwa katika picha ya pamoja nje ya ukumbi wa Bunge leo mjini Dodoma. Wanafunzi hao 10 wasichana na 10 wavulana wamepewa cheti na Waziri Mkuu, kopyuta ya pakato (laptop) na fedha taslimu shilingi laki mbili kwa kila mmoja.
****
WAZIRI Mkuu, Mizengo Pinda amewataka wanafunzi wote nchini kuwa na nidhamu , kujituma na kufuata maelekezo vizuri ya walimu wao na kuepuka makundi mabaya ili kuweza kupata mafanikio katika masomo yao.

Aidha Waziri Mkuu Pinda amewaasa wanafunzi waliofanya vizuri katika mtihani wa kuhitimu kidato cha sita wa mwaka huu kutumia uhuru vizuri watakaoupata kwenye maisha ya vyuo vya elimu ya juu bila kurudi nyuma katika maendeleo ya masomo yao.

Kauli hiyo ilitolewa leo na Waziri Mkuu, Pinda Bungeni mjini Dodoma kabla ya kuwatunuku vyeti vya kuwapongeza wanafunzi hao 19 kati 20 waliofanya vizuri katika mtihani huo,kutoka shule mbalimbali nchini, ambapo mmoja wao, Jamal Juma yuko nje ya nchi.

Wanafunzi hao ambao wote walipata ufaulu wa daraja la kwanza katika mtihani huo, saba kati yao wanatoka katika shule ya wasichana ya Marian, watatu Mzumbe, wawili Fedha na wengine wawili Kibaha. Waliobakia mmoja mmoja anatoka Kilakala, Ufundi Ifunda, Tabora girls, Tabora boys, Minaki na Mpwapwa.
Mmefanya vizuri. Mnastahili ! Hongereni Sana. Tunataka ufaulu wenu uwe mzuri zaidi kwa vile sasa ninyi mnakweda kujenga weledi. Mnakuwa wataalamu wa fani Fulani. Tumieni muda wenu kujifunza zaidi kutafuta maarifa zaidi na kuvumbua mambo makubwa zaidi yatakayowasaidia ninyi wenywe na jamii kwa ujumla kujiletea maendeleo alisema Waziri Mkuu Pinda.

Aliongeza kuwa ni vizuri utaratibu huo wa kuwatambua wanafunzi bora uwe endelevu na ikiwezekana wapatiwe fursa ya kuendelezwa katika vyuo vikuu vya kipekee nje ya nchi hususan kwenye fani zitakazojenga uwezo kwa taifa

Waziri Mkuu alisema kati ya shule 10 ,ambazo wanafunzi hao wanatoka, wawili ni kutoka shule za kata, ambao ni Ester Marcel toka shule ya sekondari ya wasichana ya Olele Kilimanjaro na Brighton Lema toka shule ya sekondari ya Kitangiri, Mwanza.

Napenda niwape pongezi za pekee wanafunzi hawa kwa jihudi kubwa walizozionesha. Kufaulu kwao kunadhihirisha kwamba shule hizi za kata tukiweka bidii kwa kuziwezesha zaidi zitafanya vizuri zaidi kama ilivyo katika shule nyingine.

Waziri Mkuu pia aliwataka walimu wote nchini kushirikiana na wazazi na serikali kwa pamoja kufundisha watoto kwa bidii ili waweze kufanya vizuri katika masomo yao kama wanafunzi hao waliotunukiwa vyeti hivyo.

Kwa upande wake Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Dk. Shukuru Kawambwa alisema wanafunzi hao watazawadiwa pakato (laptop) na sh. 200,000, pia kila shule iliyotoa mwanafunzi bora itazawadiwa sh. milioni moja katika hafla maalum itakayofanyika jioni.

Wanafunzi hao wanatoka katika mchepuo wa PCM ambao ni 16 na mmojammoja toka mchepuo wa PGM, CBA, ECA na HKL.

Naye Spika wa Bunge la Jamhuri, Anna Makinda aliwataka wanafunzi hao kuwa makini na makundi kwa kuyasilikiza huku wakitumia akili zao huku akitoa changamoto shule nyingine kujitahidi kufanya vizuri.

TAIFA STARS YAWASILI SALAMA GABORONE TAYARI KUUMANA NA WABOTSWANA




Kikosi cha timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars) kikiwa na wachezaji 17 kimewasili leo asubuhi jijini Gaborone tayari kwa mechi ya kirafiki ya kalenda ya Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA) dhidi ya wenyeji Botswana 'Zebras' itakayochezwa kesho (Agosti 15 mwaka huu).
Stars ilitua kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Sir Seretse Khama saa 5.45 asubuhi kwa saa za hapa ambapo nyumbani ni 6.45 na kupokewa na viongozi wa Chama cha Mpira wa Miguu Botswana (BFA) na Watanzania wanaoishi hapa Botswana.
Baadhi ya wachezaji walioko kwenye kikosi hicho ni Frank Domayo, Ramadhan Singano na Simon Msuva ambao walijiunga na Stars saa chache baada ya kurejea kutoka Nigeria ambapo walikuwa na timu ya vijana wenye umri chini ya miaka 20 (Ngorongoro Heroes) ambayo Jumapili ilicheza mechi ya mashindano ya Afrika dhidi ya Nigeria (Flying Eagles).

Sunday, August 12, 2012

DK.ULIMBOKA AREJEA MZIMA DAR ES SALAAM

Kiongozi wa jumuiya ya madaktari nchini Tanzania, Dk. Steven Ulimboka, amerejea leo nyumbani akitoka Afrika Kusini katika matibabu. Dk Ulimboka amepokelewa leo na madaktari wenzake, ndugu jamaa na marafiki, alipowasili Jumapili Agosti 12, 2012, kwenye uwanja wa ndege wa kiamataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam akitokea kwenye matibabu Afrika Kusini. Alisema yuko fiti na anaweza kufanya shughuli zozote atakazopewa kuanzia sasa.akiwasili jana Agosti 12, 2012 akitokea kwenye matibabu Afrika Kusini
Kiongozi wa jumuiya ya madaktari nchini Tanzania, Dk. Steven Ulimboka, akiwa amebeba maua, nakuzungukwa na amadaktari wenzake na wananchi wa kawaida, alipowasili Jumapili Agosti 12, 2012, kwenye uwanja wa ndege wa kiamataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam akitokea kwenye matibabu Afrika Kusini. Alisema yuko fiti na anaweza kufanya shughuli zozote atakazopewa kuanzia sasa. 

RASH SPORTSAND ENTERTAINMENT(RSE) KUDHAMINI MISS UTALII 2012

HATIMAYE Shindano la Miss Utalii mwaka 2012 linaloshirikisha Wilaya mbili za Kinondoni na Ilala limepata mdhamini ambaye ni Kampuni ya ‘Rash Sports and Entertainment’ (RSE).
Shindano hilo litafanyika Agosti 14 mwaka huu, kwenye Ukumbi Hoteli ya Serena, jijini Dar es Salaam ambako litashirikisha warembo 30 kutoka katika wilaya hizo mbili.
 
Akizungumza na Fullshangweblog jijini leo, wakati akimnadi mfadhili huyo, Mkurugezi wa Shindano hilo, Methuselah Magese alisema kujitokeza kwa mfadhili huyo, kutasaidia kuamsha ari ya washiriki kwa kuutangaza vizuri mkoa wa Dar es Salaam kiutalii.
 
Alisema mfadhili huyo, ameahidi kusaidia kipindi cha mazoezi kilichobaki cha wanyange hao, ambako awali mazoezi hayo yalikuwa yakifanyika katika hoteli ya Traventine na hivi sasa kuhamia Lamada.
 
“Lengo la shindano hili ni kutaka kuligeuza jiji la Dar es Salaam kuwa kivutio cha utalii kama ilivyo kwa mikoa ya Kilimanjaro na Arusha”alisema Magese.
 
Akizungumzia maandalizi kuhusu warembo hao, Magese, alisema warembo wote 30 wanafanya mazoezi kwa juhudi pia wako vizuri kiakili katika kuchambua mada mbalimbali walizojiandalia kwa ajili ya siku fainali.
 
Naye Mkurugenzi wa RSE, Rashid Mrisho, alisema kwa kuwa biashara nyingi zimekuwa zikiendelea kupitia matangazo, hivyo kuwasaidia warembo hao ni moja ya fursa itakayoleta chachu katika  kuvitangaza viashiria vyote vya utalii vilivyoko katika jiji hilo.

Wednesday, August 8, 2012

MAPOKEZI YA PREZZO KENYA AKITOKEA BBA, HUYU NDIO MAMA MZAZI

CMB PREZZO ambae ni mshindi wa pili wa Big Brother Afrika 2012 akihojiwa na waandishi wa habari baada ya kutua kwenye uwanja wa ndege wa Jomo Kenyatta
.
.
.
Mama na mwana.

Monday, August 6, 2012

MZISHI YA MAMA YAO P SQUARE JISI YALIVYOFANYIKA


Hili ndio gari lililobeba jeneza la mwili wa marehemu.

.

Kwa mbele ya gari waliwekwa hii picha ya Marehemu.

Mabango ya msiba mpaka barabarani.

.

Pater na Paul wakiwa kwenye upande wa kulia na kushoto mwa jeneza la mama yao mzazi.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

Marehemu mama mzazi wa Peter na Paul wa P Square.
Mama mzazi wa waimbaji Peter na Paul Okoye wanaounda kundi la P-Square alifariki dunia july 11 2012 baada ya kuugua kwa muda mrefu, na alipelekwa India miezi michache iliyopita baada ya kuzidiwa.
Mrs Okoye alikua mmoja kati ya watu waliowasaidia sana P Square kufanya vizuri kwenye muziki ikiwemo kuwapa ushauri watoto wake hao ambao sasa hivi wamepanda ngazi na kufanikiwa mpaka kufanya kazi na wakali wa dunia kama Akon pamoja na Rick Ross.