Basi bwana kuna jamaa mmoja bwana nimejuana nae miezi ya karibuni..ofisi zetu zipo jirani so tunakutana saaana lunch time..basi kila siku ananiomba tukutane jioni tupate hata lunch na story mbili tatu!kiukweli nimemtolea nje toka siku nyingi unajua huyu jamaa sio type yangu na mimi sitaki kuingia majaribuni si mnajua tena roho i radhi ila mwili ni dhaifu!
yaani the guy ni bonge la hb!financial yupo vizuri magari mazuri ! former mbeba box nk! mimi napenda mwanaume simple hata kama ni kulala nae kwenye mkeka hawa masuperbrand mimi nawaogopa kwa kweli!tuachane na hayo!
sasa alhamisi kiukweli akanibembeleza sana toka asubuhi dinner! dinner! !!!!!! basi nikaona ngoja nijiachie wkend nirefresh mind na huyu kijana from obama land nibadilishie mwili vitamin!
basi bwana huyu jamaa kama nilivosema ni mjanja mjanja na kuishi mbele huko nikajua nitapata bonge la meal kwa jioni ya jana! kwa hiyo mchana sikula ila tumbo liwe vizuri kupokea vitu vya ukweli!sikutaka kuchafua tumbo langu na ubwabwa wa bongo!
so nikatoka ofsini ,nikaingia zoezi kutafuta njaa vizuri ...then huyoo nikamwambia jamaanipo ready huyo akaja tukaanza safari kuelekea hotelini kupata hiyo dinner!
sasa tulivofika hotelini jamaa akaingiza gari parking akaniambia wait usishuke
akaanza ooh ujue nimeshafanya booking ya chumba...tutafanya hivi ..i love uuu na blah blah kibao za ..........
nikakakataa nikamsomea principle zangu nikamwambia nirudishe tu home maana naweza kukujeruhi sasa hivi!
huyoo akanirudisha hata maji ya kunywa ya uhai sijanywa mwenzenu halafu hapo ilikuwa saa tatu tatu hivi sijaweza hata kupika tena!...nimejilalia njaa hivi hivi !
No comments:
Post a Comment