Pages

BRAND NEW MUSIC

metty magese

metty magese

Listen & Download

http://mdundo.com/a/32626

Monday, September 9, 2013

PENNY AWACHIMBA BITI AKINA WEMA,LINAH NA LULU KUHUSU DIAMOND

Mtangazaji nyota nchini ambae ni mchumba wa kupika na kupakua wa mwanamuziki Diamond Penny amevunja ukimya na kutoa onyo kali kwa wasanii wa kike na wasio wasanii kumlaia mbali baby boy wake Diamond.

Habari za uhakika toka kwa mtu wa karibu na Penny anaeishi nae maeneo ya Mwananyamala ambae pia aliomba hifadhi ya jina lake alisema “ Jamani Penny amejipanga kuolewa na Diamond kwani sasa hivi amecharuka na kutoa onyo kali kwa mwanamke yeyote atakae msogelea mchumbaake huyo la sivyo ataroka mtu” Alisema dada huyo ambae anafanyakazi nyumba ya jirani na anapoishi Penny
Penny amepiga mkwara huo hasa akimlenga zaidi msanii Lulu na Linah nk huku akitahadharisha kuwa anawaomba wote wenye tabia ya kuchukua wanaume za watu kwani yeye katika maisha yake hajawahi kuchukua mume wa mtu hivyo kama akihisi kuna ajenda yoyote ya siri kati ya mchumbaake na wasanii hao hakika ataroga mtu kwani yeye ni mtoto Mdigo halisi.

Aidha chanzo hicho kiliongeza kusema kuwa penzi la Penny na Diamond limefikia pazuri kiasi cha familia zao kutembelea na kula pamoja kama wakwe. Hata hivyo ilielezwa kuwa Familia ya Diamond imeshampa Baraka zote mtoto wao ili amuoe kabisa Penny na huku nae Penny akihimizwa kudumisha upendo wa dhati kwa Diamond ambae tangu aanze kuishi na mtangazaji huyo Diamond amebadilika sana kitabia kiafya nk.

No comments: