Ile  tu michuano inaanza na mamiss wakipita jukwaani kwa ufunguzi tayari  hali ilikuwa ngumu kwa majaji kutokana na uwiano na vigezo kuonekana  kushabihiiana kama si kulandana kwa ukaribu saana. Miss  Kagera 2011 Miss Janeth Abdul akivujwa taji mara tu baada ya kutangazwa  mshindi.Na mshindi wa pili ni Denise Apondi na mshindi wa tatu ni Miss  Beatrice Marwa ambae ni mshiriki aliye iwakilisha Bukoba mjini.
Mshindi wa kwanza na wapili ni wawakilishi wa wilaya ya Muleba. Mzuka  ulimpanda mtu mzima 20% wakati wa show ya kuwasindikiza warembo  alimanusura jukwaa lididimie kutokana na wadau kumpokea vizuri msanii  huyu nguri mwenye staili ya kuimba kwa majonzi ile hali anafurahisha. Mgeni wa heshima RPC mkoa wa kagera Ndg Enery Selewi (katikati|)akifatilia mchakato mzima wa kumsaka mlimbwende wa mkoa. Niwashiriki  wa Miss Kagera wakipita jukwaani kwa mavazi mbalimbali kama ya ufukweni  na vazi la ubunifu.Mshindano haya ya vodacom Miss Kagera yalifanyika  jana kwenye ukumbi wa linas Night club.Na yameandaliwa na Angers  Entertaiment chini ya mkurugenzi wake Mr Josephat Rwebangira. Msimamizi  wa shamba la kahawa akijaribu kuwaelekeza mamiss wetu juu ya kilimo cha  kahawa na faida zake,Shamba hili lipo chini ya Kiroyera tours ambao  niwadhamini wakubwa wa Miss Kagera 2011. Mamiss  wakiwa kwenye Pango la kyamnene sambamba na wadau wengine kutoka  kushoto ni Dj Sley na wa pili kutoka kulia ni Emanuel Ernest  Mbaule(doctor)wote wa 88.5 kasibante FM Radio ambao pia niwadhamini wa  miss kagera 2011. Wadau  katika picha ni mratibu wa shughuli nzima ya Miss Kagera na Mkurugenzi  wa Angels Entertaiment kutoka kushoto ni Mr Joseph Rwebangira  na wa  pili ni Mr Abdulmarick Tungaraza(Dj Max).
Angels Entertaiment kama tunavyo elewa ni mabingwa wa kuandaa matamasha  mbalimbali kama ilivyo kuwa mwaka 2009 Miss Dar City Center na kuwapata  warembo watatu bora walio ibuka Wwashindi miss Tanzania,nA mwaka jana  2010 ndio waandaaji wa  Miss Mwanza na 2011 wamevuka sasa wapo mkoani  Kagera. Anaonekana Mr Hadam (Dj Wabago) kwenye mapolomoko ya Msitu wa Kyamnene Maruku. Ni Mr Joseph(Jose)wa Angels Entertaiment na Dj Slay wa 88.5 Kasibante Fm Radio.Mtu mzima magese ntarudi jumatano bado niko Bukoba mkiona kimya nilikuwa bize kidogo pande hizi.
 
 
No comments:
Post a Comment