Basi la kampuni ya Sumry limetumbukia mtoni na kuua watu tisa na kujeruhi wengine hamsini na tatu.
Ajali hiyo imetokea katika kijiji cha Sitalike wilaya ya Mlele mkoani Katavi
Tukio
hilo la kusikitisha lilitokea saa sita usiku kuamkia Julai 5, 2013 basi
hilo lilipokuwa likitokea mjini Sumbawanga kuelekea Mpanda mkoani
Katavi likiwa na abiri waliokuwa wametoka Mbeya.
Kaimu
Kamanda wa Polisi mkoani Katavi Emanuely Nnley alisema jana kuwa ajali
hiyo ilihusisha basi aina ya Nissan Diesel lenye namba T909 AZT mali ya
kampuni ya Sumry lililokuwa likiendeshwa na dereva aliyetajwa kwa jina na
Stephano Chimane maarufu kwa jina la Ntungu
Alisema
basi hilo lilipofika katika daraja hilo lenye kona kali na mteremko,
dereva wake alishindwa kulimudu na kulenga daraja hali iliyosababisha
tairi za nyuma kupanda juu ya ukingo na kutumbukia mtoni ambapo dereva
wa basi hilo aliweza kutoka na kukimbilia kusikojulikana ...
Mkuu
wa mkoa wa Katavi Dr Rajabu Rutengwe alitoa rambi rambi kwa wafiwa wote
na kuwapa pole wahanga wa ajali hiyo mbaya kutokea tangu mkoa huo
uanze.
No comments:
Post a Comment