MREMBO
atakayetwaa taji la Redds Miss Temeke 2013, linalofanyika Ijumaa Julai
5, mwaka huu ataondoka na zawadi za jumla ya Sh. Milioni 3,250,000 ikiwa
ni zawadi kubwa zaidi kutolewa katika mashindano yote ya urembo,
yaliyofanyika mwaka huu.
Mshindi
huyo, atapata ofa ya mwaka mzima kutoka RIO gym & Spa, iliyopo
Quality Center, kutumia vifaa vyote ndani ya gym hiyo ambayo gharama
yake ni Milioni 1,400,000, pia atajinyakulia simu ya kiganjani yenye
thamani ya Sh 700,000 , dinner set kutoka AKO Catering yenye thamani ya
Sh,150,000 sanjari na pesa taslim Sh. Milioni 1, hiyo jumla yake ni
Milioni 3,250,000.
Mshindi
wa pili katika mashindano hayo ambayo mgeni rasmi atakuwa Mbunge wa
Jimbo la Temeke, Abas Mtemvu atajinyakulia kitita cha Sh.800,000 pesa
taslim na dinner set ambayo thamani yake ilikuwa bado haijathibitishwa
na mdhamni wa zawadi hiyo wakati mshindi wa tatu ambao wote kwa pamoja
ni wawakilishi wa Miss Temeke, yeye atajipatia fedha taslimu Sh 700,000.
Sh
, 400,000 zitakwenda kwa mshindi wa nne na atakayeshika nafasi ya tano
yeye ataibuka na Sh 300,000. Washiriki wengine ambao hawatabahatika
kuingia katika nafasi ya tano bora, wote watapewa Sh,200,000 kwa maana
ya kifuta jasho. Tumelenga zawadi za fedha zaidi, hii ni kutokana na
ugumu wa maandalizi kwa warembo ambao hugharamika zaidi, kiasi nasi
kuona kuna kila namna ya kuwapunguzia maamivu hayo.
Shindano
hilo, linatarajiwa kuwa na burudani ya kipekee kutoka kwa mshindi wa
tungo bora ya Bongo Fleva ya Kili Music mwaka huu, Ben Paul sanjari na
Twanga Pepeta ambayo mwishoni mwa wiki, ilizindua albamu yake ya 13 kwa
mafanikio makubwa.
Warembo
watakaopanda jukwaani Julai 5 ni kutoka Kigamboni, Kurasini na
Chang'ombe ambao wanawania taji linaloshikiliwa na Miss Tanzania namba
tatu, Edda Sylvester walikuwa chini ya wakufunzi Suzy Mwenda na Shadya
Mohamed wakati kwenye kucheza nako walikuwa na walimu wawili Super
Bokilo na Charles.
Warembo hao ni pamoja na Axsaritha Vedastus, Darling Mmary, Esther Muswa, Hyness
Oscar, Irene Rajab, Jamila Thomas, Latifa Mohamed, Margreth Gerald,
Margreth Olotu, Mey Karume, Mutesi George, Naima Ramadhan, Narietha
Boniface , Stella Mngazija na Svtlona Nyameyo .
Shindano
hilo limedhaminiwa na kinywaji cha Redd's, Dodoma Wine, Gazeti la Jambo
Leo, Cloud’s Media, Blogu ya Wananchi (Le Mutuz), Fredito
Entertainment, CXC Africa tours & Safaris, RIO Gym& Spa, 100.5
Times FM na Kitwe General Traders. Mbali ya wadhamini hao pia Redds Miss
Temeke imechangiwa katika ufanikishaji na Mbunge wa Jimbo hilo, Abbas
Mtemvu na mwanamichezo maarufu nchini Geofrey Nyange Kaburu hasa kwa
upande wa zawadi.
Temeke,
imewahi kutoa warembo kadhaa miaka ya nyuma waliopata mafanikio katika
mashindano hayo, mitindo na kazi nyingine hasa kupata uzoefu wa
kujiamini katika njanja mbalimbali. Miongoni mwao ni Miriam Odemba(1997)
aliyepata kuiwakilisha Tanzani katika fainali za mitindo zilizofanyika
Nice Ufaransa na kupata mkataba wa Elite Model Look, baadaye
kufakinikiwa kutwaa nafasi ya pili ya Miss Earth World, zilizofanyika
China.
Pia,
Temeke ilimtoa Happines Millen Magesse(2001), na kutwaa taji la Miss
Tanzania na kwa sasa anang'ara sana katika tasnia ya mitindo katika nchi
za Marekani, Afrika Kusini na barani Afrika kwa ujumla. 2003 Temeke
ilimtoa Miss Tanzania, Sylvia Bahame na 2006 kuwatoa Jokate Mwegelo na
Irene Uwoya.
Jokate
alitwaa taji la Miss Temeke mwaka huu na pia kushika nafasi ya pili
Miss Tanzania na pia kushinda taji la ubalozi wa Redd's na gazeti la
Citizen. Uwoya ambaye alikuwa mshindi wa pili Temeke alishika nafasi ya
nne kwenye Miss Tanzania mwaka huo. Genevieve Mpangala mwaka 2010
alitwaa taji la Miss Temeke baadaye kushinda taji la Miss Tanzania.
Nafasi
nyingine za juu zilizowahi kutwaliwa na warembo kutoka Temeke ni pamoja
na Irene Kiwia, mshindi wa nne Miss Tanzania mwaka 2000, Regina Mosha
mshindi wa nne Miss Tanzania mwaka 2002, Cecylia Assey mshindi wa pili
Miss Tanzania 2004, Queen David mshindi wa tatu mwaka 2007 na Edda
Sylvester mshindi wa tatu Miss Tanzania akiwa anashikilia taji la Redds
Miss Temeke.
BMP
Promotions inayoandaa mashindano haya kwa mwaka wa 18 sasa,
inatanguliza shukrani zake wadhamini wetu kwa miaka hiyo, sanjari na
vyombo vyote vya habari kwa ujumla wake, kwani ndio waliofanikisha
kuandaa Miss Temeke kwa ufanisi katika muda wote huo, shukrani sana.
No comments:
Post a Comment