Mratibu wa Tamasha la RAHA ZA JANA NA
LEO Bw.Kahabi Ng'wendesha akilitambulisha rasmi Tamasha hilo kwa
waandishi wa habari leo jijini Dar katika hoteli ya Chichi iliyopo
manispaa ya kinondoni jijini Dar.
Bw. Kahabi alizungumzia namna kampuni
ya Yuneda namna ilivyojiandaa kufanikisha tamasha hilo linalosubiriwa
kwa hamu na wakazi wa jiji la Dar jumamosi hii katika viwanja vya posta
kijitinyama.
Baadhi ya viongozi wa bendi tofauti
wakiwa katika mkutano na waandishi wa habari kuthibitisha ni namna gani
wamejiandaa naTamasha hilo linalokutanisha bendi sita za muziki wa
dansi nchini Tanzania.Bendi hizo ni Mashujaa,Bantu group,Twanga
pepeta,Msondo,Sikinde na king kikii"wazee sugu".
Mwanamuziki Bichuka(Sikinde)
akifafanua namna watakavyoiburuza Msondo Ngoma jukwaani ikiwa ndiyo
waasimu wao wa siku nyingi kwa mara nyingine wanakutana jukwaa moja
viwanja vya posta.Pia kutakuwa na silent moment kuwakumbuka wanamuziki wote wa mziki wa dansi waliotangulia mbele ya haki nchini Tanzania.
King Kikii(kushoto) akielezea namna
alivyojipanga kuteka mashabiki siku ya jumamosi hii katika viwanja vya
posta .kulia ni mwanamuziki mkongwe Hamza Kalala.Milango ya uwanja
itakuwa wazi kuanzia saa tano asubuhi hadi usiku mnene,Watoto bureeee
wakubwa Tssh 8,000/= tu.
No comments:
Post a Comment