Dereva
 kutoka  nchini Ujerumani Rainer Zietlow (katikati) akizungumza na 
wanahabari kuhusiana na rekodi yake ya kusafiri umbali mrefu Duniani 
mara baada ya kuwasili nchini Tanzania kwenye Ofisi za Alliance Autos, 
Kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya CFAO Motors,  Bw.Wayne 
McIntosh na kushoto ni Meneja Masoko wa CFAO Motors, Tharaia Ahmed.
Na Mwandishi Wetu
DEREVA
 raia wa Ujerumani Rainer Zietlof yuko mbioni kuvunja rekodi ya dunia ya
 kuendesha gari kwa kilometa 17,000 kutoka Ulaya hadi Afrika.
Akizungumza
 na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, Zietlof alisema kuwa hiyo 
itakuwa ni rekodi yake ya tatu baada ya zile za awali alizovunja mwaka 
2011 na 2012.
Awali
 alivunja rekodi baada ya safari iliyojulikana kama `Panamerica’ambayo 
ilimchukua kutoka Tierra del Fuego hadi Alaska kwa siku 11 na saa 17 
wakati ile ya `Russtralia’ ilimtoa Melbourne, Australia hadi 
St.Petersburg nchini Urusi ambako alitumia saa 18.
Zietlof
 anayetumia gari aina ya VW Touareg V6 TDI alianza rasmi safari yake 
Septemba 21 mwaka huu huko North Cape nchini Norway na anatarajia 
kuikamilisha nchini Afrika Kusini, ambako atakuwa ametembea kwa kilometa
 17,000.
Kwa
 mujibu wa dereva huyo, safari hiyo ndefu imempitisha katika nchi za 
Norway, Finland, Sweden, Denmark, Ujerumani, Jamhuri ya Czech, Slovakia,
 Hungary, Serbia, Bulgaria, Uturuki, Misri, Sudan, Ethiopia, Kenya na 
sasa Tanzania.
Dereva
 huyo alizungumza na wandishi wa habari katika makao makuu ya CFAO 
Motors yaliyopo barabara ya Nyerere jijini Dar es Salaam, na kusema kuwa
 atachangia  kiasi cha senti 20 za euro kwa kila kilomita, kwa vijiji 
vya watoto wanaoishi katika mazingira hatarishi (SOS) nchini Tanzania na
 Zambia.
Mbali na kuahidi kuvichangia vijiji hivyo, Zietlot pia amesisitiza kuvitembelea vijiji hivyo atakavyo vichangia.
Aidha,
 amelisifia gari hilo  kutokana na uwezo wake wa kukabiliana na 
mazingira tofauti tofauti ya hali ya hewa kama baridi kali na joto 
pamoja na barabara mbovu.
Mradi
 huu wa kuzunguka sehemu mbalimbali za dunia kwa gari hilo umedhaminiwa 
na makampuni ya Tehama, magari ya Volkswagen ya Ujerumani, Slovakia na 
Afrika Kusini.
Katika
 safari hiyo Zietlow yuko na wasaidizi wake wawili, Marius Biela ambaye 
ni mpiga picha na mchukua video; Matthias Prillwitz ambaye ni mzoefu wa 
mbio za magari nchini Ujerumani.
Dereva huyo alianza safari zake za barabarani mwaka 2005 na ameoa na ana mtoto mmoja.
  Dereva
 kutoka  nchini Ujerumani Rainer Zietlof (wa kwanza kulia )akiwaelezea 
jambo wanahabari hawapo pichani Kushoto kwake ni Meneja Masoko wa CFAO 
Motors Ltd. Tharaia Ahmed
Mkurugenzi
 Mtendaji wa kampuni ya CFAO Motors,  Bw.Wayne McIntosh akielezea ni kwa
 namna gani magari yao yako imara kuhimili masafa marefu akitolea mfano 
gari ya Volkswagen aliyosafiri nayo dereva kutoka  nchini Ujerumani 
Rainer Zietlof.
Dereva kutoka nchini Ujerumani Rainer Zietlof akioyesha cheti cha rekodi ya dunia mbele ya wanahabari
Dereva toka  nchini Ujerumani Rainer Zietlof akitoa maelekezo ya gari yake aina ya Volkswagen Touareg V6 TDI
Dereva
 toka  nchini Ujerumani Rainer Zietlof akitoa maelekezo ya injini ya 
gari yake aina ya Volkswagen Touareg V6 TDI aliyosafiri nayo kwenye nchi
 zaidi ya 19 Duniani.
Dereva
 toka  nchini Ujerumani Rainer Zietlof akitoa maelekezo ya bodi ya gari 
yake aina ya Volkswagen Touareg V6 TDI aliyosafiri nayo kwenye nchi 
zaidi ya 19 Duniani.
Dereva
 Toka  Nchini Ujerumani Rainer Zietlof akitoa maelekezo ya sehemu ya 
kuweka vifaa vya akiba kwenye gari yake aina ya Volkswagen Touareg V6 
TDI
Dereva Toka  Nchini Ujerumani Rainer Zietlof akiendelea kutoa maelekezo ya Gari yake hiyo aina ya Volkswagen Touareg V6 TDI
 Gari aina ya Volkswagen Touareg V6 TDI inavyoonekana kwa ndani.
Dereva
 kutoka  nchini Ujerumani Rainer Zietlof akiwa na Mkurugenzi Mtendaji wa
 kampuni ya CFAO Motors,  Bw.Wayne McIntosh (wa pili toka kulia) 
wakipata picha ya pamoja na wanahabari.
 Mkurugenzi
 Mtendaji wa kampuni ya CFAO Motors,  Bw.Wayne McIntosh (kushoto) 
akipata picha na Dereva toka  nchini Ujerumani Rainer Zietlof
Meneja Masoko wa CFAO Motors Ltd. Tharaia Ahmed(kushoto) akipata picha na Dereva Rainer Zietlof.
 Mkurugenzi
 Mtendaji wa kampuni ya CFAO Motors,  Bw.Wayne McIntosh akisoma cheti 
cha rekodi ya dunia alichopewa dereva toka Ujerumani.
 
 
No comments:
Post a Comment