Shindano
 la Miss Kilimanjoro Ambassador 2015 limepamba moto kwa kuchukua sura 
mpya kwenye vyombo vya habari likiwa na mvuto wa aina yake.
Warembo
 wanaowania taji hilo wako kambini kwa sasa wakinolewa vilivyo ikiwa ni 
maandalizi ya fainali za shindano hilo litakalofanyika julai 24 katika 
ukumbi Kili Home mjini Moshi.
Habari
 za kuamianika toka kamati ya maandalizi imesema kuwa kamati imejipanga 
kisawasawa kuhakikisha wanakidhi kiu ya wapenzi wa tasnia ya urembo 
katika mikoa ya kaskazini  ikiwemo Arusha ,manyara na Kilimanjaro kwa 
ujumla.
Pamoja na burudani toka kwa washiriki hao kutakuwa na burudani ya wasanii wa bongo flava,ngoma za asili na saplaizi ambayo haijawahi kutokea katika mkoa wa Kilimanjaro katika anga za burudani.
Kiingilio
 cha siku hiyo V.I.P(A) ni Tsh 200,000/= ikijumuisha chakula na 
vinywaji, V/I.P(B) ni Tsh 100,000/= pamoja na vinywaji, SILVER ni Tsh 
50,000/= na REGULAR ni 30,000/= 
 
 




No comments:
Post a Comment