Mwenyekiti wa CHADEMA UK Mr Christopher Lukosi amevuliwa madaraka na kusitishwa uanachama.
Ikiwa
ni takribani miezi minne tangu tawi la CHADEMA UK lifunguliwe rasmi na
Mr Godbless Lema, kumekuwepo na maendeleo makubwa ya ujenzi wa tawi hili
lakini vile vile kumekuwepo na changa moto mbali mbali kutokana na
uelewa wa watu ktk dhana nzima ya M4C. M4C ikiwa na maana ya Movement
for Change, ni sharti mtu yeyote anayeingia ktk movement hii kwenye
ngazi ya uongozi aelewe haya machache ya msingi:
1) Kwanza aone matatizo yanayomgusa yeye na jamii yake
2) Ajue na kutambua fika chimbuko la matatizo haya
3) Awe tayari kuwa kiini cha mabadiliko ya kweli anayoyataka kwa jamii
4) Aweze kutoa ufumbuzi kwa kukemea maovu, kuelimisha na hata yeye binafsi kuelimika
5) Ili afanikiwe ktk kipengele cha (4) ni sharti ajitambue yeye binafsi ya kwamba ni:
i) Lazima awe safi na mwenye sifa za kukemea waovu
ii) Aweke maslahi ya jamii mbele na si yake binafsi
iii) Awe na sifa za uongozi zinazotakiwa, nidhamu ikiwa nambari moja ktk orodha.
iv) Awe na msimamo wa kiitikadi
Kwa
hiyo, uongozi wa CHADEMA UK kwa baraka za watetezi wa haki ya kweli
(CHADEMA TZ) unawatangazia umma watanzania kokote mlipo kwamba kuanzia
leotarehe 12/12/12, Mr Christopher Lukosi amevuliwa rasmi uongozi na amesitishwa uanachama kutokana na kutokidhi mengi ya yaliyotajwa hapo juu.
Uongozi
wa CHADEMA UK unamshukuru sana kwa mchango na ushirikiano wake mkubwa
kwa kipindi ambacho matundu ya chujio yalikuwa makubwa. Tutaendelea
kumkumbuka na hata kutumia misemo yake yenye maana nzito kwa jamii ya
kitanzania, kama vile: -
i) Sisi sote ni ndugu, tatizo ni CCM
ii) Kila kwenye msafara wa mamba na kenge wamo
Uongozi
unamwakikishia Mr Christopher Lukosi kwamba mamba wote wa CHADEMA UK
kwa kushirikiana na wote wenye kuelewa mageuzi ya kweli, tutaliondoa
tatizo ifikapo 2015. Tunamtakia kila la kheli katika maisha na ni imani
yetu tutaendelea kuwa ndugu yake baada ya tatizo kutatuliwa !!!!.
“We fail in most of our endeavours because we too often underestimate People’s Power” [M4C UK, 2012]
Na christina George
Na christina George
No comments:
Post a Comment