Pages

BRAND NEW MUSIC

metty magese

metty magese

Listen & Download

http://mdundo.com/a/32626

Monday, December 10, 2012

TAMKO LA DCPC JUU YA MWANDISHI KUPIGWA RISASI


Kufuatia kupigwa risasi, kujeruhiwa begani na kulazwa katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili kwa mwandishi wa Tanzania Daima Bwana Shabani Matutu (30) ambaye pia ni mwanachama hai wa Dar City Press Club(DCPC), uongozi wa Klabu uliamua kufuatilia tukio hilo kwa karibu ili kujua na kuhakiki kwa kina yaliyotokea na sababu zilizopelekea hayo kutokea.

Kutokana na hayo DCPC imebaini yafuatayo. 

1. Ni kweli kwamba Shabaan matutu(30) alipigwa risasi na askari wa jeshi la Polisi mwenye namba F.8991 D/C Idrissa nyumbani kwa Shabaan kimakosa baada ya askari huyo na wenzake wanne kufungua kwa nguvu na bila ya kujitambulisha kwa mwenye nyumba (Shabaan na Mkewe) licha ya kuombwa kufanya hivyo kabla.

2. Kuna maelezo yanayokinzana katika kuelezea jinsi tukio hilo lilivyotokea kwa pande mbili zinazohusika yaani maelezo ya shabaan na ya polisi

3. Kwamba sababu za askari polisi hao kufanya hivyo hazikuwa zimefanyiwa uchunguzi wa kutosha hadi kujiridhisha kuchukua hatua hiyo hivyo hata wao walikiri kukosea pamoja na kueleza kwamba Shabaan ndiye aliyeaanza kuwashambulia askari Polisi kabla ya wao kumjeruhi kwa risasi.

4. Shabaan mpaka sasa anaendelea na matibabu licha ya kuuguza majeraha aliyosababishiwa na polisi na kwamba ameshauriwa kitaalamu kupumzika nay eye binafsi ameomba asibughudhiwe ili afya yake irejee haraka na kwamba pindi atakapokuwa katika hali nzuri zaidi ya sasa kwa mujibu wa ushauri huo wa kitabibu, atawasiliana na yeyote wakiwemo polisi ambao wamekuwa wakimmghasi kwa kuja kumhoji mara kwa mara.

Kwa sababu hizo basi Dar es salaam City Press Club

1. Tunaiomba Serikali na mamlaka za juu zaidi ya jeshi la Polisi hususan Wizara ya mambo ya ndani ifanye uchunguzi wa kina na huru wenye kuhusisha taasisi wakilishi katika jamii juu ya tukio hilo na kulichunguza jeshi la polisi linavyofanya kazi zake kwa kuzingatia kanuni na sheria.

2. Tunalitaka Jeshi la Polisi liache mara moja kutuma askari wake kwenda kwa Shabaan kwa lengo la kumhoji ama kutaka atoe maelezo yake kwa viongozi wa jeshi hilo ilhari walishamtuhumu na kueleza kuwa aliwashambulia Polisi kwa Panga kabla ya wao kumfyatulia risasi. Tunasema hivi kwa kuzingatia kanuni za afya na haki za msingi za binadamu.

3. Tunalitaka Jeshi la Polisi liueleze umma bila kuficha ukweli na kwa jinsi ile ile ambayo lilitoa taarifa mara baada ya tukio, lieleze kwa nini linatumia habari na vyanzo dhanifu kujeruhi na kuhatarisha maisha ya raia wasio na kosa huku likitoa maelezo yasiyofanyiwa uchunguzi.

4. Mwisho tunalitaka jeshi la Polisi lenyewe lijitafiti na kujipanga upya ili liweze kufanya kazi kisayansi na weledi kama ambavyo viongozi wake wamekuwa wakijinadi mbele ya vyombo vya habari. Tamko hili limetolewa leo Tarehe 08/Desemba/2012.

Joseph Kayinga 
Katibu Mkuu-DCPC

No comments: