Pages

BRAND NEW MUSIC

metty magese

metty magese

Listen & Download

http://mdundo.com/a/32626

Sunday, September 14, 2014

TB Joshua awakosoa waandishi walioandika ghorofa 6 za kanisa lake zimeporomoka, aeleza kilichotokea

Picha: TB Joshua awakosoa waandishi walioandika ghorofa 6 za kanisa lake zimeporomoka, aeleza kilichotokea

Kanisa la mhubiri maarufu wa Nigeria, TB Joshua linalojulikana kama The Synagogue Church of All Nations limetoa tamko rasmi kuhusu tukio la kuporomoka kwa jengo la ghorofa sita la kanisa hilo, tukio lililoripotiwa kuua watu kadhaa na kujeruhi, Ijumaa.
Katika tamko hilo lililowekwa kwenye ukurasa wao wa Facebook, wamewakosoa waandishi walioripoti kuwa kanisa zima limeporomoka na kwamba sio kanisa wanalotumia kwa ibada bali ni jengo.
“Hili ni tamko rasmi kutoka The Synagogue, Church Of All Nations kuhusu habari zinazoripotiwa hivi sasa na vyombo vya habari kufuatia tukio lililotekea leo. Ni jengo na sio kanisa (tunalotumia kwa ibada) kama ilivyoripotiwa. Watu wachache waliokuwa mule wameokolewa. Unachotaka kitokee kwa wenzako, Mungu anakutakia wewe. Hakuna kinachotufanya sisi kumpenda mtu kama kumuombea. Kadiri navyokupenda, ndivyo kadiri nitakavyokuombea.” Limesomeka tamko hilo.

Ingawa hawakuzungumzia kabisa kuhusu watu kupoteza maisha au la..taarifa za awali zimeeleza kuwa watu makumi wamepoteza maisha. Baadhi ya mashuhuda walisema kuwa wameona miili ya watu waliopoteza maisha ikitolewa katika jengo hilo.

Hata hivyo bado hakuna uthibitisho wa daktari kuhusu taarifa hizo za watu kupoteza maisha.
Inaelezwa kuwa zaidi magari ya wagonjwa (ambulance) 20 yalionekana yakitoka katika eneo hilo yakiwa na majeruhi.

No comments: