Wema Sepetu.
Gari inayomilikiwa na Wema Sepetu kwa madai ya habari za udaku kununuliwa na kibopa huyo.
Gari inayomilikiwa na Wema Sepetu kwa madai ya habari za udaku kununuliwa na kibopa huyo.
Baada
ya kuletewa fujo weekend iliyopita na mwanamke anaedai muigizaji Wema
Sepetu amemuibia mume, leo mrembo huyo (Wema) ameamua kuzungumzia
upande wake ambapo kama haukuingia. juzi march 5 kulikua na stori ya
huyo mwanamke kumfanyia fujo Wema baada ya kumkuta yeye na wasanii
wenzake ndani ya Pub ambayo inamilikiwa na mwanamke huyo.
Wema
amesema “kwanza mimi mwenyewe nilishtuka sana, nilikua natafuta
location ya kucheza movie yangu kwenye mgahawa, nikawa nimepaki nje
kutoka na kurudi nikamkuta mwanamke ndani ya gari jeupe limepaki
pembeni yangu siijui wala huyo mwanamke simjui nikamchukulia kama mmoja
wa haters, akaanza kufanya fujo wakati mimi huwa siwezi fujo,
nikajitahidi kutoka eneo la tukio na kupiga simu polisi na kuja
kumchukua huyo mwanamke na kwenda polisi Osterbay”
“Kiukweli
sitembei na mwanaume wake, sitembei na mume wa mtu……. alafu yule ni
mwanamke mtu mzima sana hawezi kugombana na mimi, mi mtoto mdogo
akitaka aje na uthibitisho, alafu anasema gari ninayotembela ni yake?
gari ni yangu mpaka kazi ninazo mimi huo ni ujinga na ndio maana siwezi
nikaachia hii kitu iende hivyo hivyo tu kama anavyotaka yeye” – Wema
“Kama
kweli ningekua namchukulia mwanaume wake sidhani kama ningekua
nimefikishana nae hapa tulipofika manake ningekua namuogopa, sasa simuogopi na afanye chochote anachotaka kufanya,
waniache na maisha yangu nimekaa kimya mtoto wa watu wananifatafata,
nikisema watasema nimesema, waniache basi mi mwenyewe nina maisha yangu
ya kuishi” hayo ni maneno ya Wema ambae pia amekataa na kuapa kwamba
hajawahi kutumia bili za milioni 1.5 mpaka mbili kwenye baa ya huyo
mwanamke, huku ikidaiwa kwamba bili hizo zimekua zikilipwa na huyo
pedeshee ambae ni mume wa mwanamke mwenye pub.
Jana
mmoja kati ya marafiki wa Wema akiwa ni mdogo wake na mke wa pedeshee
huyo, alikiri kwamba urafiki wake na Wema umevunjika baada ya kugundua
anatoka kimapenzi na mume wa dada yake (yani mume wa mwanamke
aliemfanyia Wema fujo)
No comments:
Post a Comment