Pages

BRAND NEW MUSIC

metty magese

metty magese

Listen & Download

http://mdundo.com/a/32626

Tuesday, June 5, 2012

BODI MPYA YA MISS UTALII KUANZA KAZI KWA KASI YA AJABU

MISS UTALII TANZANIA 2005 ,KILY JANGA BAADA YA KUSHINDA TAJI LA DUANIA LA MISS TOURISM WORLD SADIC 2006, HUKO CHINA
· Sasa ni Taasisi ya Kutangaza na kuhamasisha Utalii, Utamaduni, Bidhaa za Ndani,Utalii wa Ndani,Utalii wa Kitamaduni,Utalii wa Michezo na Utalii wa Mikutano, Mazingira,Elimu,Afya ya Jamii,Kilimo, Madini na Maliasili kitaida na kimataifa.
·         Vitengo vya Miss Tourism Tanzania International, National Parks Marathon, Tanzania Great Safari & Tour, Tanzania Beach Soccer na Tanzania Cultural Carnival, Festival & Conference vyaanzishwa.
·         Fainali na Uongozi Ngazi za Majimbo, Wilaya, Mikoa, Mikoa maalumu ya Vyuo Vikuu, Kanda, Kanda maalumu za Vyuo Vikuu na Taifa.
·         Waandaaji,Viongozi na washiriki mamaluki 40 yao imefika, Kila Mbunge, Mkuu wa Wilaya,Mkuu wa Mkoa kuwa na Miss /Binti Utalii katika jimbo lake
·         Kuswahili sasa Lugha Rasmi ya Mashindano hayam wawakilishi katika mashindano ya dunia kutumia Kiswahili jukwaani.
·         Wakaribisha mawakala wapya, na kuwataka wa zamani kuomba upya.

Bodi ya Mashindano ya Miss Utalii Tanzania, imeanza kuonyesha cheche zake kwa kishindo, kwa kufumua mfumo mzima wa uongozi na mashindano haya makubwa na yenye mafanikio nchini.Katika kikao chake kilichofanyika mwishoni mwa wiki,chini ya makamu mwenye kiti wa bodi hiyo Ndugu Abubari Omari Abubakari, bodi imechukua hatua mbalimbali kwa lengo la kuboresha na kimarisha Mashindano haya lenye manufaa makubwa kiuchumi,kitamaduni na kijamii kitaifa na kimataifa.

Bodi imeazimoa kuchukua hatua katika Nyanja mbalimbali za mashindano haya, kuanzia mfumo wa mashindano,uongozi,utawala na uendeshaji mzima wa mashindano. Bodi imeazimia kufanya mabadiliko haya, na kuwa Miss Tourism Tanzania Organisation, ni taasisi ambayo kuanzia sasa itaendeshwa kwa mfumo wa kitaasisi, ambayo sasa badala ya kuwa taasisi ya mashindano ya urembo pekee, inakuwa ni taasisi ya kuhamasisha na kutangaza  Utalii, Utamaduni, Mazingira, Elimu, Afya ya Jamii, Bidhaa za Tanzania, Uvuvi, Wanyama Pori, Madini, Hifadhi za Bahari, sera za Taifa za Utalii, Utamaduni, Kilimo, Mazingira, Umasikini, Vijana, Wanawake na watoto, Utalii wa Ndani,Utalii wa Kitamaduni, Utalii wa Michezo na Utalii wa Mikutano. 

Pia kupiga vita Uvuvi haramu, Uwindaji Haramu, Umasikini, Maradhi, Ujinga, Tamaduni kongwe na Potifu kitaifa na kimataifa.Malengo haya yatafikiwa kupitia mashindano ya Miss /Binti Utalii Tanzania, Miss tourism Tanzania International, Miss Tourism University World, Miss Heritage World, Tanzania Beauty and Model Management, National Parks Marathon, Tanzania Great Safari and Tour na Tanzania Cultural Carnival and Festival kila mwaka.

Aidha kuanzia mwaka huu, pamoja na Shindano la kitaifa la Miss Utalii Tanzania, fainali za Taifa zitakwenda sambamba na Miss Tourism Tanzani International, ambapo washiriki wa Tanzania watapanda jukwaani kuwania taji la taifa sambamba na washiriki waalikwa kutoka nchi mbalimbali Duniani wakiwania taji la Miss Tourism Tanzania International,ambapo washindi wake watakuwa mabalozi wa Tanzania katika mabra na nchi zao. 

Kwa kuwa na washiriki kutoka katika mabara yote duniani ikiwemo Ulaya,Marekani,Asia,India,Marekani Kusini,Afrika na Urusi Shindano la Miss Utalii Tanzania sasa litakuwa ni la kimataifa na lenye uwezo mkubwa wa kuitangaza Tanzania, Utalii ,Utamaduni na mali asili zake kimataifa, kwani fainali za taifa kuanzia mwaka huu, zitaonyeshwa LIVE duniani kote kupitia Televisheni na mitandao ya Internet. Bodi pia imepitisha azimio la kutumia lugha ya Kiswahili kwa wawakilishi wote wa mashindano haya katika mashindano ya dunia na mengine ya kimataifa, ili kukitangaza vyema Kiswahili ambayo ni lugha ya limataifa na ya Afrika, kama ambavyo washiriki kutoka mataifa mengine wanavyo tumia lugha zao na kushinda mataji ya Dunia.

Bodi imefanya uchambuzi wa kina wa wakurugenzi na waandaaji wa ngazi mbalimbali, na kupitisha azimio la kuwataka waandaaji wa Majimbo (Vitongoji) ,Wilaya, Mikoa, Mikoa maalum ya Vyuo Vikuu, Kanda na Kanda maalum za Vyuo Vikuu kuomba upya na kutoa fulsa kwa watu na makampuni mbalimbali kuomba kuandaa katika ngazi yoyote nchini, isipokuwa waandaaji wake katika mabano Dar es Salaam, Ilala na Temeke (Film Directors Association) Katavi (KATABI CO. LTD & COUNTRY WIDE ENTERTAINMENT) Arusha na Mara  (NAMAN 201O LIMITED ),Tanga ( Kambi Mbwana Entertainment),Vyuo Vikuu Mkoa wa Dar es Salaam ( ERIADO POINT VIEW) Kanda ya Kusini (MOD INTERGRATED SOLUTION AND AWARENESS) na Kanda ya Ziwa (FANIA BEAUTY ENTERTAINMENT) ambako waandaaji wake wanabaki kama walivyo. Ambako waandaaji wapya wanatakiwa na wazamani wanaruhusiwa kuomba ni:
1.    Miss Utalii Tanzania – Kanda ya Kaskazini, Mashariki, Mgharibi na Kati.
2.    Miss Utalii Tanzania – Kanda za vyuo Vikuu – Kaskazini, Kusini, Kati, Magharibi, Ziwa na Mashariki.
3.    Miss Utalii Tanzania –Mikoa ya Dodoma, Singida, Tabora, Kigoma, Kagera, Rukwa, Shinyanga, Geita, Simiyu, Mwanza, Ruvuma, Lindi, Mtwara, Lindi, Pwani, Morogoro, Manyara, Kilimanjaro ,Iringa, Mbeya, Njombe.
4.    Miss Utalii Tanzania Vyuo Vikuu – Mikoa ya Dodoma, Morogoro, Tanga, Mwanza, Kagera, Mbeya, Iringa, Kilimanjaro, Arusha na Tabora.
5.    Miss Utalii Tanzania – Majimbo yote ya Wabunge na Wilaya.

Mwisho wa kupokea maombi ya waandaaji wapya na wa zamani ni tarehe 12 Juni 2012, waombaji wanaweza kutuma maobi yao kupitia anuani zetu barua pepe ambazo zina patikana katika website (www.misstourism/utaliitanzania.com, blogspoti (misstourismorganisation.blogspot.com na mitandao yetu ya facebook, twitter na Skype (misstourismtanzania au missutaliitanzania). 

Kwa mfumo huu mpya unalenga kufikisha kwa umakini na ustadi mkubwa Shindano hili hadi ngazi za cheni kabisa za wananchi, na kufanya kila mbunge wa jimbo , mkuu wa Wilaya, mkuu wa Mkoa na Rais wa nchi kuwa na mabalozi wao wa Utalii kupotia mashindano haya, ambao watasaidia na kuwa na jukumu la kuhamasisha Utalii, Utamaduni, Utalii wa Ndani, Utalii wa kitamaduni, mazingira, Elimu, Afya ya Jamii, Kilimo, na Mianya ya uwekezaji katika ngazi zao , sambamba na mamlaka za umma na binafsi za ngazi hizo, huku wakitafsiri kwa vitendo sera husika za taifa. Aidha bodia imeazimia kuimarisha umakani na kitengo cha uchunguzi na intelijensia cha Shindano ili kubaini njama,hujuma na mamluki katika Shindano hili, kabla hawaja leta madhara na kuwachukulia hatua kali ikiwemo kuwafikisha katika Vyombo vya dola.

Akizungumza na waandishi wa Habari, Abubakari alisema kuwa, pamoja na sababu za kukosa umakini na ufanisi, waandaaji hao wa ngazi za mikoa na kanda wamekuwa wakiruhusu warembo wasio na viwango na hata vigezo kushiriki katika mashindano, jambo ambalo ni kinyume kabisa na kanuni na taratibu za mashindano haya, ambayo kwa miaka mitano mfulizo yamekuwa yaki fanya vyema katika mashindano mbalimbali ya Dunia na kimataifa.

 “Tumelazimika kuchukua hatua mapewa, ili kulinda hadhi ya mashindano haya kitaifa na kimataifa. Ni mkakati wa bodi ya mashindano sasa kuwaondoa mashindanoni washiriki wote ambao hawakidhi viwango bila kujali mataji watakayo kuwa wametwaa katika ngazi zao. Fainali za Taifa mwaka 2012 zitafanyika mwezi Novemba 2012 ,ili kutoa fuksa kwa waandaaji wa kanda na mikoa iliyo salia kufanya fainali zao,pia kuzingatia kalenda mpya za mashindano ya Dunia na kimataifa.
Asante,
Abubakari Omari Abubakari
Makamu Mwenyekiti Bodi ya Mashindano ya Miss/ Binti Utalii Tanzania
Nakala Rais Miss Tourism Tanzania Organisation

No comments: