Mashindano
   ya Urembo ya Redd’s Miss Tanzania 2012 yanaendelea kwa kasi kubwa na 
  kwa wiki hii kutakuwa na shindano moja kubwa hapa jijini Dar es salaam
   ambapo kituo cha Ubungo yaani “REDD’S MISS UBUNGO 2012”  kitakuwa kikifanya shindano lake.
Shindano hili litafanyika Ijumaa hii ya tarehe 29 / 06 / 2012  katika Ukumbi wa Hotel ya LANDMARK iliyopo ubungo kuanzia saa mbili usiku..
kiingilio katika shindano hili kimepangwa kuwa tsh. 10,000/= tu na burudani itakayosindikiza shindano hili itatoka kwa bendio ya FM ACADEMIA (wazee wa ngwasuma)
kituo
   hiki cha miss ubungo ndicho kilichomtoa Miss Tanzania 2004 FARAJA   
KOTTA, hivyo ni mategemeo yetu tutatoa tena Miss Kinondoni na hatimae   
ndie atakaekuwa REDD’S MISS TANZANIA 2012.
Jumla
   ya warembo kumi na sita wamejitokeza kuwania taji hili wakiwa chini 
ya   mwalimu wao BEATRICE JOSEPH ambaye alikuwa Miss Ruvuma 2004 na kwa 
  upande wa shoo ya ufunguzi wanafundishwa na BOKILO ambaye ni 
mwanamuziki   kutoka TOT BAND.
 
 

No comments:
Post a Comment